A
Anonymous
Guest
Usafiri huo umekuwa kimbilio kwa Watu wengi, sababu kuu ikiwa ni muda ni kutokana na kutumia muda mfupi kufika maeneo husika.
Lakini nimefika pale mara kadhaa hasa Wikiendi kuna jambo nimeligundua, kuna mchezo mchafu unafanywa na baadhi ya Watendaji hasa wanaokata tiketi.
Wahusika hao wanatumia Watu wao wa karibu kununua tiketi wanapohisi kuna abiria wengi zaidi hasa Wikiendi, baada ya kufanya, hivyo Wanunuzi wa hizo tiketi wanajifanya kughairi safari, kinachoenda kufanyika zile tiketi zinauzwa kwa bei ya juu zaidi, mfano tiketi ya Dar-Moro ya 13,000 inauzwa mpaka 30,000.
Baadhi ya wahudumu wa ndani wakishakata tiketi kupitia jamaa zao zile tiketi wanawapatia wahudumu wa nje ya madirisha ambao jukumu lao ni kutoa maelekezo na usaidizi kwa abiria namna ya kupata tiketi.
Wakishapewa hizo tiketi wanafuata abiria mmojammoja aliyekosa wanakwambia ujiongeze wakupe tiketi, wanakuandaa kuna Mtu kaghairi kusafiri, ukishindwa kufikia kiwango wanachokitaka wanakutosa wanaenda kwa mwingine.
Wale wahudumu ambao wanafanikisha mchezo huo wakiona uwezekano wa kushutukiwa wanakwambia kaa subiri mpaka Treni ikikaribia kuondoka, ikija wanakupa tiketi unawapa chao na kupanda.
Bila mamlaka kuchukua hatua mapema mradi huu utakuja kuwatajirisha baadhi ya Watu kupitia njia na taratibu ambazo hazina uhalali.
Kama kuna mabehewa ambayo tayari yameshawasili nchini ni muhimu ukafanyika mchakato wa haraka yakaongezwa hasa siku za weekend kwa lengo la kuondoa mazingira ya upigaji.
Lakini pia ikiwezekana mchakato wa kupata wawekezaji uharakishwe ili waweze kuingiza mabehewa zaidi kwa kuwa kwa mwenendo huu uenda kuna Watu wachache wananufaika na hali hii.
Pia soma:
~ Ukitaka kukata tiketi SGR unaambiwa treni imejaa, muda wa kuondoka treni inakuwa wazi
~ Online booking SGR haifanyi kazi, nifanyaje?
~ TRC: Tumewakamata Watu kadhaa waliokuwa wanafanya ulanguzi wa tiketi za SGR na kufanya udanganyifu