DOKEZO Baadhi ya Wahudumu wa Treni ya SGR (Dar) wanalangua tiketi kisha wanaziuza kwa bei ya juu

DOKEZO Baadhi ya Wahudumu wa Treni ya SGR (Dar) wanalangua tiketi kisha wanaziuza kwa bei ya juu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
hiv tunaanza kuhujumu mapema hiv? sasa vitu vizur tutakua tunaskia kwa wenzetu.jana tumerushwa mpaka na jamaa wa first post iliyopo India wanasifia tanzania electric train. yan ni ndoto kuwa na treni.tukiitunza tutakua mbali sana.sasa wanaanza kulangua?
 
Ni kweli huduma inapatikana katika simu, computer online n.k,

Ila kila mara treni imejaa, na ukibahatisha inaonekana seat moja au mbili ndio zimebakia, ajabu ukipanda treni unalala seat wima kabisa hakuna watu. Ukiingia online kila behewa no Seat ila ukiwa ndani ya behewa zinatembea tupu. Kuna namna mahali iangaliwe na tupewe ufafanuzi
Treni kwenda ikiwa tupu wakati umeambiwa ilijaa haimaniishi kuwa ni hujuma. engine nitatizo la abiria kuchelewa au kughairi safari. Cha kuangalia zaidi ni je, wanaposema terni imejaa, fedha zinazopatikana zinaendena na idadi ya abiria waliojaza treni?
 
Yaani nitoke kulipa 13 hadi 30...kwani mabus hayapo?
Hiyo michezo ya mjini,watu wanataka maokoto,niwape uzoefu,Dar es salaam Huwa haipoi,hata mfanyaje watapiga tuu,shida wanajua huko juu kinachoendelea na wao wanafanya yao.Wale wamachinga wa mtaa wa Congo na Agrey wote wanachukua kwa mchina na wanapata kitu,Hilo ni Jiji,kesho mtakuta watu wanaendesha vx hapo posta kwa pesa hiyohiyo,mikoani tuwe wapole kwa DSM kila kitu ni fursa.
 
Wewe unayo tool ya kuverify hilo?
Treni kwenda ikiwa tupu wakati umeambiwa ilijaa haimaniishi kuwa ni hujuma. engine nitatizo la abiria kuchelewa au kughairi safari. Cha kuangalia zaidi ni je, wanaposema terni imejaa, fedha zinazopatikana zinaendena na idadi ya abiria waliojaza treni?
 
Hiyo michezo ya mjini,watu wanataka maokoto,niwape uzoefu,Dar es salaam Huwa haipoi,hata mfanyaje watapiga tuu,shida wanajua huko juu kinachoendelea na wao wanafanya yao.Wale.wamachinga wa mtaa Congo na Agrey wote wanachukia kwa mchina na wanapata kitu,Hilo ni Jiji,kesho mtakuta watu wanaendesha vx hapo post kwa pesa hiyohiyo,mikoani tuwe wapole.kwa DSM kila kitu ni fursa.
Ujinga wa uongozi na kuleana ndio tatizo
 
Ni siku chache zimepita tangu Huduma za Usafi wa Treni ya SGR uanze na juzi tulishuhudia Rais Samia Suluhu Hassan akiongoza zoezi la uzinduzi.

Usafiri huo umekuwa kimbilio kwa Watu wengi, sababu kuu ikiwa ni muda ni kutokana na kutumia muda mfupi kufika maeneo husika.

Lakini nimefika pale mara kadhaa hasa Wikiendi kuna jambo nimeligundua, kuna mchezo mchafu unafanywa na baadhi ya Watendaji hasa wanaokata tiketi.

Wahusika hao wanatumia Watu wao wa karibu kununua tiketi wanapohisi kuna abiria wengi zaidi hasa Wikiendi, baada ya kufanya, hivyo Wanunuzi wa hizo tiketi wanajifanya kughairi safari, kinachoenda kufanyika zile tiketi zinauzwa kwa bei ya juu zaidi, mfano tiketi ya Dar-Moro ya 13,000 inauzwa mpaka 30,000.

Baadhi ya wahudumu wa ndani wakishakata tiketi kupitia jamaa zao zile tiketi wanawapatia wahudumu wa nje ya madirisha ambao jukumu lao ni kutoa maelekezo na usaidizi kwa abiria namna ya kupata tiketi.

Wakishapewa hizo tiketi wanafuata abiria mmojammoja aliyekosa wanakwambia ujiongeze wakupe tiketi, wanakuandaa kuna Mtu kaghairi kusafiri, ukishindwa kufikia kiwango wanachokitaka wanakutosa wanaenda kwa mwingine.

Wale wahudumu ambao wanafanikisha mchezo huo wakiona uwezekano wa kushutukiwa wanakwambia kaa subiri mpaka Treni ikikaribia kuondoka, ikija wanakupa tiketi unawapa chao na kupanda.
Huu mchezo mchafu uenda baadhi hawajaubaini maana unafanyika kwa siri na Watu wanapiga hela hasa kipindi cha wikendi, ni mamlaka nifuatilie suala hilo haraka ili kuondoa mazingira ya upigaji.

Bila mamlaka kuchukua hatua mapema mradi huu utakuja kuwatajirisha baadhi ya Watu kupitia njia na taratibu ambazo hazina uhalali.

Kama kuna mabehewa ambayo tayari yameshawasili nchini ni muhimu ukafanyika mchakato wa haraka yakaongezwa hasa siku za weekend kwa lengo la kuondoa mazingira ya upigaji.

Lakini pia ikiwezekana mchakato wa kupata wawekezaji uharakishwe ili waweze kuingiza mabehewa zaidi kwa kuwa kwa mwenendo huu uenda kuna Watu wachache wananufaika na hali hii.

Pia soma:
~ Ukitaka kukata tiketi SGR unaambiwa treni imejaa, muda wa kuondoka treni inakuwa wazi
~ Online booking SGR haifanyi kazi, nifanyaje?
Waajiri Wahindi ndiyo wasimamie kila kitu. Hao Waswahili ni watu wa hovyo kabisa hawawezi kuwa na maadili na mwisho wataiua kabisa hiyo huduma
 
Umeelewa alichoandika lakini?

Hata ukifika pale na cheti Cha ubatizo utaambiwa tren imekaa hivyo jiongeze Kuna abiria kaghaili kusafiri ndo unapigwa Cha juu

Hivyo vitambulisho havitasaidia lolote
Usichoelewa hapa ni kuwa hakuna abiria atakayeruhusiwa kuwa na ticket isiyo na namba yake ya NIDA,kitambulisho cha taifa,Leseni au barua ya serikali ya mtaa,kwahiyo hao walanguzi hawataweza kumuuzia mtu asiehusika na hiyo ticket...
 
Ni siku chache zimepita tangu Huduma za Usafi wa Treni ya SGR uanze na juzi tulishuhudia Rais Samia Suluhu Hassan akiongoza zoezi la uzinduzi.

Usafiri huo umekuwa kimbilio kwa Watu wengi, sababu kuu ikiwa ni muda ni kutokana na kutumia muda mfupi kufika maeneo husika.

Lakini nimefika pale mara kadhaa hasa Wikiendi kuna jambo nimeligundua, kuna mchezo mchafu unafanywa na baadhi ya Watendaji hasa wanaokata tiketi.

Wahusika hao wanatumia Watu wao wa karibu kununua tiketi wanapohisi kuna abiria wengi zaidi hasa Wikiendi, baada ya kufanya, hivyo Wanunuzi wa hizo tiketi wanajifanya kughairi safari, kinachoenda kufanyika zile tiketi zinauzwa kwa bei ya juu zaidi, mfano tiketi ya Dar-Moro ya 13,000 inauzwa mpaka 30,000.

Baadhi ya wahudumu wa ndani wakishakata tiketi kupitia jamaa zao zile tiketi wanawapatia wahudumu wa nje ya madirisha ambao jukumu lao ni kutoa maelekezo na usaidizi kwa abiria namna ya kupata tiketi.

Wakishapewa hizo tiketi wanafuata abiria mmojammoja aliyekosa wanakwambia ujiongeze wakupe tiketi, wanakuandaa kuna Mtu kaghairi kusafiri, ukishindwa kufikia kiwango wanachokitaka wanakutosa wanaenda kwa mwingine.

Wale wahudumu ambao wanafanikisha mchezo huo wakiona uwezekano wa kushutukiwa wanakwambia kaa subiri mpaka Treni ikikaribia kuondoka, ikija wanakupa tiketi unawapa chao na kupanda.
Huu mchezo mchafu uenda baadhi hawajaubaini maana unafanyika kwa siri na Watu wanapiga hela hasa kipindi cha wikendi, ni mamlaka nifuatilie suala hilo haraka ili kuondoa mazingira ya upigaji.

Bila mamlaka kuchukua hatua mapema mradi huu utakuja kuwatajirisha baadhi ya Watu kupitia njia na taratibu ambazo hazina uhalali.

Kama kuna mabehewa ambayo tayari yameshawasili nchini ni muhimu ukafanyika mchakato wa haraka yakaongezwa hasa siku za weekend kwa lengo la kuondoa mazingira ya upigaji.

Lakini pia ikiwezekana mchakato wa kupata wawekezaji uharakishwe ili waweze kuingiza mabehewa zaidi kwa kuwa kwa mwenendo huu uenda kuna Watu wachache wananufaika na hali hii.

Pia soma:
~ Ukitaka kukata tiketi SGR unaambiwa treni imejaa, muda wa kuondoka treni inakuwa wazi
~ Online booking SGR haifanyi kazi, nifanyaje?
saa shida iko wap biashara n kuchangamka
 
Siku kadhaa zilizopita mtoa mada fulani aliandika " Treni zinaondoka kwenye vituo behewa zikiwa tupu huku wakiambiwa zimeshajaa" na mwingine akasema "bites (vyakula) wanauziwa..

TRC ni suala la muda itakua kama mwendokasi . Itakufaa

Fukuza wafanyakazi wote wanaonyesha hali za wizi
Hapo unakuta wameajiri kwa kigezo cha uchama wala sio uwezo wala uadilifu hivyo kama wanavyoiona serikali ni ya chama chao basi wanajiona wako huru kuiba.
Tatizo la uendeshaji wa miradi ya serikali ni management tu. Hata bandari ilihitaji management sio mwekezaji kwa sababu pesa ya kuwekeza serikali inayo.
 
Umeelewa alichoandika lakini?

Hata ukifika pale na cheti Cha ubatizo utaambiwa tren imekaa hivyo jiongeze Kuna abiria kaghaili kusafiri ndo unapigwa Cha juu

Hivyo vitambulisho havitasaidia lolote

Shida ya ajira za upendeleo ndio hayo .Wanaajiriwa wasio na maadili kabisa

Kwenye mfumo WA kukata Tiketi WA TRC waweke sehemu ya jina kamili na MTU aje na kitambulisho wakati WA kupandia

Mbona mabasi Hilo mfumo wao umeweza

Hata ndege mbona wameweza

Latra huo mfumo wanao waupeleke TRC

LATRA pelekeni mfumo wenu TRC
 
Walishaweka wazi kuwa abiria akighairi kusafiri hawi refunded… kwa maana hiyo sidhani kama system yao imeruhusu ticket kuwa replaced ..
Kwa misingi hiyo najaribu kufikiria kwamba mwanzoni huyo wa kupandishiwa dau alikuwa anatumia ticketi iliyokatwa isiyo na jina lake .. Maana kuingia kwenye treni ni kuscan QR code unaingia bila kuangalia jina.
Utaratibu wa kukagua Jina Vs kitambulisho utasaidia kucontrol hilo .

Kama walikuwa wanapandisha dau na system inaruhusu kureplace tiketi kwa jina lingine then that’s another issue ..,

I stand to be corrected

Na kama walikuwa wanareplace ni rahisi kuwakata na kuwachukulia hatua stahiki
You nailed it...
 
Ndugu abiria,
Shirika la Reli Tanzania linapenda kukutaarifu ya kwamba kuanzia tarehe 10/08/2024 unapokata tiketi,hakikisha unakitambulisho kimoja wapo kati ya NIDA, kiambulisho cha Kura, bima ya Afya, leseni ya Udereva, hati ya Kusafiria,au kitambulisho cha kazi. Kama hauna basi uje na barua ya Serikali za mtaa yenye picha yako iliyogongwa muhuri. Kwa mtoto anayekatiwa nusu tiketi kuanzia miaka 4 hadi 12 tafadhali fika na nakala moja wapo kati ya cheti cha Kuzaliwa, bima ya Afya, hati ya Kusafiria au kitambulisho cha Shule.Na siku ya kusafiri hakikisha unakuja na kitambulisho chenye jina sahihi ambalo lipo katika tiketi yako.
Kwa mawasiliano zaidi piga simu ya Huduma kwa Wateja namba 0800110042

Labda hii ya kukagua jina Vs Vitambulisho itasaidia kudeal na changamoto hiyo .
Mbona kuchoshana hivi?
 
Treni kwenda ikiwa tupu wakati umeambiwa ilijaa haimaniishi kuwa ni hujuma. engine nitatizo la abiria kuchelewa au kughairi safari. Cha kuangalia zaidi ni je, wanaposema terni imejaa, fedha zinazopatikana zinaendena na idadi ya abiria waliojaza treni?
Tusubiri Audit ya hiyo computer System na ya fedha.itakapokuja kufanyika

Kama kuna hako.kamchezo ni rahisi Tu watu kwenda jela na kupoteza kazi

Mifumo ya computer haidanganyi ulisema train full halafu taarifa za fedha za mkaguzi WA fedha isiseme full na Tiketi zilizokatwa zisiseme full na taarifa ya safari ya siku hiyo isitoe ripoti kuwa treni haikuwa full kuna watu kupoteza kazi na kufungwa Kwa uhujumu uchumi mchana kweupe na mapema sana
Kuna watu kesi ya uhujumu uchumi inaeanyemelea
 
Labda hii ya kukagua jina Vs Vitambulisho itasaidia kudeal na changamoto hiyo .
Kwa ile nyomi ya watu sidhani km wataweza kuangalia hvy vyote zaid ya kuangalia uhalali wa tiket. Suruhu;
1. Kupunguza muda wa kushikilia siti kwenye mfumo kutoka dak 40 hadi 5 au 10.
2. Kwa sbb huko ni kuhujumu uchumi, wahusika washitakiwe kwa kosa la kuhujumu uchumi, wengine hawatathubutu.
 
Back
Top Bottom