Mimi binafsi ndugu zangu wengi ni walokole, na kuna kipindi walishajaribu kunivuta na nikaenda, japo sikuwahi kuingia ile deep sana nikaachana nao.
Nilichojifunza ni kwamba;
1. Walokole wengi hawamtafuti Mungu, wao wanamfata mchungaji. Ndio maana leo utasikia wako kwa mchungaji huyu, kesho wanahamia kwa yule.. hakuna mlokole anaedumu sehemu moja wao kila siku ni kuhama hama kufuata "upepo". Tatizo wakihama sehemu, immediately wanaanza kulaumu na kusema mapungufu ya mchungaji huyo, kanisa lake nk.
2. Walokole wao kwa wao hawapendani hata kidogo! Mlokole anaesali kwa pasta A na anaesali kwa pasta B ni kama maadui. Huwezi kukuta wanashirikiana kwa chochote. Kutwa kusemana mapungufu ya mapasta/makanisa yao tena kwa maneno makali (mf yule anatumia nguvu za giza)
3. Walokole wengi ninaowajua ni wanafki na wana roho mbaya balaa. Yaani wengi wao hata ule upendo wa kawaida wa kibinadamu bado ni changamoto. Unajiuliza kama huyu asingekua mlokole ingekuaje?
4. Wengi wa walokole wanafanya dhambi ZOTE tunazozifanya sisi, kuanzia zinaa, kunywa pombe, wizi/ubadhirifu kazini, ulanguzi, uongo, utapeli nk. Japo sijui kwanini wao wanajiona kuwa ni watakatifu.
5. Suala la kunena kwa lugha ndio lilinifanya nikachoka kabisa. Walokole WOTE wananena kwa lugha moja, maneno ni yale yale na ukisali kule mda mfupi tu nawewe unayakariri. Cha ajabu wenyewe hua wanaona kama kunena kwa lugha ni hatua ya juu kabisa ya maombi!
Kikubwa ninachowalaumu hawa ndugu zangu ni kukaa kwenye ulokole zaidi ya miaka 20 na hawajaweza kufungua hata ka kanisa wapige hela.
Habari.
Haya ni mambo baadhi niliyonifunza kupitia ulokole au kuokoka. Kiukweli miaka 3 iliyopita nilikuwa mkristo mzuri sana na muumini mzuri ninayefuata misingi ya kiimani ya kipentekoste au ulokole.
Mungu anisamehe maana now natimiza mwaka sijui mlango wa kanisa yalinisubu ni mengi ila nimekua ni mtu ninayemuomba Mungu ,nasoma biblia na niaduatilia mahubiri tu kwa Tv ila sio kwenda kanisani.
Nini kilibisibu mpaka nikawa hivi.
1.Baadhi ya waumini wanaitwa walokole ni watu wanaondekeza majungu,kusemana ,umbea na hili nimeliona hadi kwa viongozi wakubwa wa kanisa.
2.Walokole wengi ni watu wanaopenda Mapenzi kiukweli katika miaka ya mwanzo ya ulokole Nikiri nilimuona Mungu kabisa kupitia kusali na kushiriki ibada ila nilipoanza kujichanganya nikajikuta na date na wanakwaya ,mashemasi hadi wake za watu nafanya nao mapenzi na tukiwa kanisani tunakuwa kama waumini wa zuri hii iliniumiza sana.
3.Walokole wengi hawana hali ya kusaidiana nimepata majanga mengi nikiwa nasali niliishia kuombea ila tofauti na watu walokole wanaowaita wa dunia wamenipiga tafu sana hadi hapa nilipo.
4.Walokole ni wabinafsi sana ngumu sana kuwakuta kwa sherehe ,misiba kwa kigezo cha kusema watu wa Dunia ambao hawajaokoka.
5.Baadhi ya makanisa hayakufundisha katika kutafuta maisha zaidi ya kukutana utumike kwa Mungu Muda wote pasipo na kupata hata muda kidogo wa kujitafutia ridhiki.
Kiukweli siusemi ulokole kwa ubaya kuna faida nyingi nimezipata.
Ila nimejikuta nimeacha kabisa kwenda kusali ila nina imani nitarudi tena sijui ni lini.