CHADEMA imemaliza uchaguzi ikiwa imegawanyika sana. Jambo ambalo kila mtu alitarajia kutokea kwa sababu waliendesha siasa za kuchafuana ,kupakana matope, kuumizana,kujeruhiana na kudhalilishana wakitegemea kuwa ndio ilikuwa njia ya kupata ushindi. Wakasahau kuwa kuna kazi kubwa ya kujenga chama ambayo ilikuwa inakuja mbele yao. Kazi ya muda mrefu kuliko hata ya uchaguzi wenyewe. Sasa wamebakia na majeraha yasiyopona na yasiyowezwa kuponywa. Chama hakitaweza tena kusimama kwa umoja na mshikamano kama uliokuwepo awali. Ndio sababu kwa sasa wengi wameamua kujikalia kimya