Baadhi ya Wanahabari wazuiwa kuingia kwenye Kesi ya Lissu; waambiwa wameruhusu 10 pekee

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
photo_2025-06-02_09-40-01.jpg

Waandishi wa habari zaidi 15 kwa nyakati tofauti wamezuiwa kuingia Mahakamani na kuamriwa kukaa mbali na viunga vya Mahakama ya Kisutu, ambapo wameambiwa kuwa wameruhusu waandishi wa habari 10 pekee kuingia ndani.

Mmoja ya waandishi ambaye amekumbana na changamoto hiyo ameeleza "Wanasema ni watu 10 tu ambao wameshaingia kwa hiyo ondokeni kafuatilien mtandaoni. Tena wanafukuza wanasema mkakae mbali"

Ikumbukwe Mahakama ilitoa uamuzi wa kuruhusu umma kwenda Mahakamani kwenye kesi zinazomkabili Tundu Lissu, hata hivyo taarifa ambayo imetolewa na Mahakama na kuenea kwenye vyombo vya habari inaeleza kuwa kesi zinazomkabili Lissu zitarushwa live kupitia kurasa rasmi za Mahakama.
photo_2025-06-02_09-39-57.jpg
 
Wanaharakati kutoka Kenya na Uganda wapo ?🐼
 
View attachment 3353283
Waandishi wa habari zaidi 15 kwa nyakati tofauti wamezuiwa kuingia Mahakamani na kuamriwa kukaa mbali na viunga vya Mahakama ya Kisutu, ambapo wameambiwa kuwa wameruhusu waandishi wa habari 10 pekee kuingia ndani.

Mmoja ya waandishi ambaye amekumbana na changamoto hiyo ameeleza "Wanasema ni watu 10 tu ambao wameshaingia kwa hiyo ondokeni kafuatilien mtandaoni. Tena wanafukuza wanasema mkakae mbali"

Ikumbukwe Mahakama ilitoa uamuzi wa kuruhusu umma kwenda Mahakamani kwenye kesi zinazomkabili Tundu Lissu, hata hivyo taarifa ambayo imetolewa na Mahakama na kuenea kwenye vyombo vya habari inaeleza kuwa kesi zinazomkabili Lissu zitarushwa live kupitia kurasa rasmi za Mahakama.
View attachment 3353284
Kwani hawakuona kwenye taarifa hyo hyo kuwa wanaruhusiwa kuingia watu 80 tu, na waandishi wa habari ni 10 tu..taarifa ilitolewa jana na mahakama!
 
Waandishi wa habari wa Tz hbr km hzo wameshaambiwa waachane nazo ,watengenezee habar za kumsifiaa mama tu🤔
 
Back
Top Bottom