View attachment 3353283
Waandishi wa habari zaidi 15 kwa nyakati tofauti wamezuiwa kuingia Mahakamani na kuamriwa kukaa mbali na viunga vya Mahakama ya Kisutu, ambapo wameambiwa kuwa wameruhusu waandishi wa habari 10 pekee kuingia ndani.
Mmoja ya waandishi ambaye amekumbana na changamoto hiyo ameeleza "Wanasema ni watu 10 tu ambao wameshaingia kwa hiyo ondokeni kafuatilien mtandaoni. Tena wanafukuza wanasema mkakae mbali"
Ikumbukwe Mahakama ilitoa uamuzi wa kuruhusu umma kwenda Mahakamani kwenye kesi zinazomkabili Tundu Lissu, hata hivyo taarifa ambayo imetolewa na Mahakama na kuenea kwenye vyombo vya habari inaeleza kuwa kesi zinazomkabili Lissu zitarushwa live kupitia kurasa rasmi za Mahakama.
View attachment 3353284