Baadhi ya Wanawake ni Binadamu wa pekee sana, nawapa Pongezi muishi miaka mingi ya Kobe

soma vizuri bandiko langu.
ktk hao jamaa zangu kuna mmoja nilimuazima pesa na mpaka leo hajanirudishia.
 
Sikuhuzi mwanamke haachwi kwa ugomvi.. mkiachana kwa amani mambo kama hayo ni rahisi kusaidiana
 
kuna mtu nilishawahi kumpa milioni moja na ushee kipindi ana shida hana mbele wala nyuma, amepata ajira na hawajamwingizia hela za kwenda kuanzia maisha huko kwenye ofisi mpya. nilikuja kukwama kitu fulani enzi hizo, nikasema huyu ni mtu wa karibu aniazime laki tano ilikuwa ya haraka sana hata kwa wiki moja tu nitamrudishia, hela yangu ilikuwa inaingia muda si mrefu. alinijibu kwamba hana hela, gari zake mbili zipo gereji ndio anashughulikia ili azitengeneze. kipindi kile ananikopa hela amechoka amekonda na hana mwingine wa kumkopa, hizo gari alikuwa hana hata moja. ilinishangaza sana, nilimsamehe ila pamoja na kwamba alikuwa mtu wangu wa karibu mno tangu tunasoma primary, niliona huyu hana faida kwangu nikamfuta mazima. huwa tunawasiliana kwa miaka miwili mara moja au bila bila, nilimtupa mbali kistaarabu lakini. wanaume kusaidiana ni kitu kigumu sana, ila wanawake anaweza kukupatia hata mshahara wote.
 
Sijasoma bandiko lote ila nachoweza kusema baadhi ya wanawake niwepesi sana kumsaidia mtu ....sisi wanaume badhibyetu wazito sana cjui kwanini .... pia tujifunze tujitahidi kuwa na urafiki wenye faida ... marafiki wengi wasio na msaada ni hasara hasa kwa hapa mjini
 
Mwanamke huyo si mpaka awe na tabia za kizungu. Gombana na demu wa Tandika au Keko kama hajakuitia Vigoma vya kukunyali baada ya kuachana.[emoji23][emoji23][emoji23] Yani gomvi lazma liwe kubwa.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Hebu tuache kidogo..
Tunanunuaga na Vijora....Hiyo kitu utaitiwa hapo hutakaa Usahau
 
Mwanamke huyo si mpaka awe na tabia za kizungu. Gombana na demu wa Tandika au Keko kama hajakuitia Vigoma vya kukunyali baada ya kuachana.πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Yani gomvi lazma liwe kubwa.
Mbona Mimi mtoto wa Tandika jamani Sio woteπŸ˜…πŸ˜…
 
Alhamdullilah leo tumesifiwa.
Ubarikiwe.
kwa kweli mnastahili kusifwa. siku za hivi karibuni nimeona mnaandamwa sana na nyuzi zinazowazungumzia vibaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…