Baadhi ya wanga ni watumwa na wapagazi

Baadhi ya wanga ni watumwa na wapagazi

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Hatua za kuwa mshirikina (combine ya uchawi, uganga, ulozi, kuwanga, kuroga na kuwanga)...! Haya yote ndio yanatengeneza neno USHIRIKINA!

Hatua ya chini kabisa ni kuweza kupaa na ungo na kuingia kwenye majumba ya watu na kuwachezea... Katika hatua hii pia kuna masomo mengine kama chuma ulete, kuchukua kitu cha mtu mbele yake bila mwenyewe kukuona, kupiga zongo nk

Hatua ya pili ni uwezo wa kujigeuza maumbile, kuvaa sura ya mtu mwingine au kujigeuza kuwa mnyama... Na hii mara nyingi hufanyika bila hata kiza kuingia

Hatua ya tatu ni uwezo wa kufika mbali kwa kitendo cha kufumba na kufumbua macho, kumvuta mtu umtakaye aje mbele yako na uwezo wa kuua ukiwa mbali

Kwahiyo kati ya wanga wanaowasumbueni usiku wengine ni wpagazi wa kutumwa vitu mbalimbali kama kucha, nywele, nguo, kuchanja chale, kwenda kuchukua wafu mahospitalini ama kukusanya damu na nyama maeneo ya ajali ambapo mara nyingi ndio wao wanakuwa wamezisababisha ama aliyewatuma

Wale washirikina makonki wa madaraja ya juu huwa hawajihangaishi kutoka kwenda kutafuta chochote hata kana wana huo uwezo bali huwatumia vijana wanaowafundisha kazi ama wasaidizi wao kwa hiari!

Je na hawa watumwa ni akina nani? Watumwa wa kishirikina namaanisha! Hawa ni watu walioko huko si kwa ridhaa yao bali kwa matendo ya binadamu wengine na wengi wao huwa kiasili ni misukule.. Hawa hutokana na Kukosana na 'wazee wa busara kisha wakakukomoa.

Ugomvi wa familia au ndugu
Kugombea mirathi ama mali
Vyeo na nafasi kazini
Umaarufu na utajiri pia

Kuna namna tatu ya kupata watumwa
1. Kumtia mtu wendawazimu/ kumfanya chizi
2. Kumpoteza asionekane tena
3. Kumchukua msukule/ kumuua kishikirina hasa hasa kupitia ajali

Ushirikina ni sayansi ya ajabu kabisa na iko deep sana...!
Unaenda kumfanyizia mtu kwa mganga kwa nia yoyote ile.. Ukifika unapewa karai lenye maji kisha anaitishwa pale nawe unamuona live kabisa sura yake.. Kisha unapewa kisu umchome! Ukishafanya hivyo tu maji yote kwenye karai yanageuka damu na huko aliko mhusika anapata ajali yoyote na kufa!

Kwanini kuchoma uso? Sio popote bali unatakiwa kuchoma sehemu ya koromeo...
Kwanini huchomi sehemu nyingine za mwili? Inawezekana kabisa ila kama hutaki afe bali apate tu ajali mbaya .. Hapo ataumia zaidi sehemu husika

Magonjwa je?
Washirikina mara nyingi hawatumii magonjwa kwakuwa unaweza kupata tiba na kupona...lakini akikukamia ili akutese muda mrefu anakupiga na maradhi ambayo utamaliza hospital zote bila tatizo kuonekana

Dawa na kinga kwa washirikina ni hizi mbili zisizo na madhara ya baadae

1. Maombi na dua.. Usiache kufanya maombi wala dua kwa kila ufanyacho iwe chakula, iwe kinywaji, iwe ukitoka ndani, iwe ukipanda chombo cha usafiri, iwe ukiingia ofisini, iwe ukiingia nyumbani nknk
2. Tumia chumvi ya mabonge kadiri uwezavyo..itangulize popote unapotaka kwenda au chochote unachotaka kufanya na ukiweza inenee au nuia
Ulimwengu usioonekana una mengi mabaya na washirikina ni sehemu yao!

Laleni salama! Na Mungu awalinde na kuwapigania!

Witchdoctor mstaafu.

1620131699084.png

 
Asante nilihadihiwa na mtukuu wa wanajeshiwa vita vya pili walienda burma na waliweza kuja kusalimianfamilia za kwa just kufumba macho na wakafika mbulu wanakaa na familiazo wanawahadisia yanayoendeleo huko vitani
 
Naomba niwe wazi tu kwako Mshana nakuamini Sana na nakupenda Sana uko makini Sana wewe,the boss na kikulachochako wote nyie ndo nawafuatilia Sana

Ila kwenye Hili la uchawi au ushirikina asee sitakaa niamini Kama Kuna kiumbe ambacho kinaweza kupotea au kupaa na ungo hizo zote kwangu Ni Kama uwongo tu labda useme mtu kulogwa maana unaweza ukawekewa hata kitu flani kwenye chakula ukipata matatizo ya kiafya tutasema umelogwa ila Hilo sijui la kubadilisha sura hawana uwezo huo.

Nina mengi ya kusema itoshe tu kwa kusema yanayosemwa mengi Ni tofauti na ambayo unaweza ukayaona
 
Naomba niwe wazi tu kwako mshana nakuamini Sana na nakupenda Sana uko makini Sana wewe,the boss na kikulachochako wote nyie ndo nawafuatilia Sana

Ila kwenye Hili la uchawi au ushirikina asee sitakaa niamini Kama Kuna kiumbe ambacho kinaweza kupotea au kupaa na ungo hizo zote kwangu Ni Kama uwongo tu labda useme mtu kulogwa maana unaweza ukawekewa hata kitu flani kwenye chakula ukipata matatizo ya kiafya tutasema umelogwa ila Hilo sijui la kubadilisha sura hawana uwezo huo.
Nina mengi ya kusema itoshe tu kwa kusema yanayosemwa mengi Ni tofauti na ambayo unaweza ukayaona
Amini nilichoandika ni halisi na kipo.. Kuna story za kukuza nyingi tu za kusadikika lakini haya mambo yapo katika uhalisia wake na MIMI MWENYEWE ndio shuhuda mkuu
 
Mkuu Mshana hapo kwenye chumvi ya mabonge unaposema utangulize popote unapokwenda au chochote unachotakakufanya unamaanisha nini?
 
Mkuu Mshana hapo kwenye chumvi ya mabonge unaposema utangulize popote unapokwenda au chochote unachotakakufanya unamaanisha nini?
1. Kumumunya kibonge kimoja na kukinenea ulinzi, vikwazo mafanikio, kinga nk
2.Kushika chumvi mkononi kuinenea na kuirusha mbele
3. Kuchukua kibonge cha chumvi kiweke kwenye soksi au kiatu mguu wa kulia na hakikisha ukitoka ndio utangulie
 
Back
Top Bottom