Baadhi ya Waumini wa Kanisa Katoliki waonekana wakinywa Konyagi nje ya Kanisa la Mt. Joseph

Baadhi ya Waumini wa Kanisa Katoliki waonekana wakinywa Konyagi nje ya Kanisa la Mt. Joseph

Kwa wakatoliki unywaji wa pombe yoyote (hata gongo!) sio dhambi. Na wakatoliki wanajivunia kunywa pombe popote ikiwemo hata kanisani, wao wanasema wanakunywa kistaarabu.

Pale ukatolikini hakuna ukristo halisi, ni upagani wa Kiitaliano ulioboreshwa kwa tamaduni zilizoupokea ukristo wa kale na kuueneza duniani chini ya mwamvuli wa kanisa.
Yaani kanisa lililouanzisha huo ukristo na mifumo yote ya ukristo mnawaita wapagani? Na wakati huo huo mnatumia mafundisho Yao, kalenda Yao, maandiko Yao, ktk hivyo vijidhehebu vyenu vilivyomsaliti mroma?

Akili huwa mnaweka wapi, kama mmeamuwa kuukataa upagani wa roma, basi anzisheni maandiko yenu na mifumo yenu ya kikanisa, maana hizo biblia zimehaririwa na mrumi ambaye mnamuona hayuko sahihi, what if ninyi ndie ambaye hamko sahihi?

Anyway Mungu wenu mnamuabudu kwa tabu sana maana Kila kanisa na mambo yake, Kila dini na mambo yake, alafu mnataka kutuaminisha tusiofuata dini zenu kuhusu wema na utukufu wa huyo Mungu mdhaifu asiyeweza ku-organize kanisa lake
 
Wapi nimesema mlevi?
sasa huo ulevi maendekeza hapo kwenye viunga vya eneo la ibada hatimae kuleta uzinzi ndivyo Yesu alivifanya baada ya huo unaita mujiza wa kubadili maji kua divai
 
1 Wakorintho 6:9-10​

Au je, hamjui kwamba watu wabaya hawataurithi ufalme wa Mungu?Msijidanganye! Watu wanaoishi maisha ya uasherati, wanaoabudu sanamu, wazinzi, au walawiti, wezi, wachoyo, walevi, wasengenyaji, wanyanganyi, hao wote hawatashiriki ufalme wa Mungu.
 
Kwa wakatoliki unywaji wa pombe yoyote (hata gongo!) sio dhambi. Na wakatoliki wanajivunia kunywa pombe popote ikiwemo hata kanisani, wao wanasema wanakunywa kistaarabu.

Pale ukatolikini hakuna ukristo halisi, ni upagani wa Kiitaliano ulioboreshwa kwa tamaduni zilizoupokea ukristo wa kale na kuueneza duniani chini ya mwamvuli wa kanisa.
Yesu mwenyewe alikuwa anakunywa pombe hata maandiko yanathibitisha hilo
 
Hakuna Mbingu Ya Walevi.
Wagalatia 5:19-21
” Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa MUNGU.’‘
 
sasa huo ulevi maendekeza hapo kwenye viunga vya eneo la ibada hatimae kuleta uzinzi ndivyo Yesu alivifanya baada ya huo unaita mujiza wa kubadili maji kua divai
Uzinzi wanafanya walevi tu,,,,,hao walokole wanaokatazwa pombe na huko misikitini wangekua watakatifu kama shida ni pombe tu
 
Mithali 23:29-35
”Ni nani apigaye, Yowe? Ni nani aliaye, Ole? Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye mguno? Ni nani aliye na jeraha zisizo na sababu? Ni nani aliye na macho mekundu?
Ni wale wakaao sana kwenye mvinyo; Waendao kutafuta divai iliyochanganyika. Usiitazame mvinyo iwapo ni nyekundu; Iitiapo bilauri rangi yake, ishukapo taratibu; Mwisho wake huuma kama nyoka; Huchoma kama fira. Macho yako yataona mambo mageni; Na moyo wako utatoa yaliyopotoka. Naam, utakuwa kama alalaye katikati ya bahari; Au kama yeye asinziaye juu ya mlingoti. Utasema, Wamenichapa wala sikuumia; Wamenipiga wala sina habari; Nitaamka lini, nitazidi kuitafuta tena.”.
 
Neno divai n pembo itokanayo na mvinyo ambayo n uzao wa mzabibu,rejea muujiza wa harusi ya kana,
Rudi upya ukafunze upya.
Divai ni neno lenye kumaanisha kinywaji kinachotokana na Zabibu. Kinaweza kutengeneza kinywaji baridi (juice), kinywaki kilichosindikwa (togwa), kinywaji kilichochachushwa (bia), kinywaji kikali (gongo), Dawa nk.
Yesu hakufanya muujiza wa kutengeneza pombe (bia au gongo).
 
Warumi 13:13-14
” Kama ilivyohusika na mchana na tuenende kwa adabu; si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu. Bali mvaeni BWANA YESU KRISTO, wala msiuangalie mwili, hata kuwasha tamaa zake. ”
 
Para yako ya mwisho ndio umechemka. Pombe sio upagani. Yesu Kristu alitengeneza pombe nzuri sana kwenye Harusi ya Kana ukiwa ndio muujiza wake wa kwanza!

Mungu alimwambia Nuhu atengeneze Safina na aingiemo kwani anakwenda kuwaangamiza watenda dhambi. Nuhu pamoja na vitu vingine aliingia Safinani na pombe akawa anagonga mdogomdogo hadi maji yalipopungua akaenda kugongea nje. Akalaaniwa mtoto aliyemchungulia na sio Nuhu aliyekuwa amegonga mvinyo!

Niendelee?
Acha kutaja mitume wa Allah kama unataja list ya mamonitor wako wa darasa wa shule ya msingi, huyo nuhu aliefanya hilo tukio labda nuh mziwanda, mafundisho yaliyobadilishwa kwenye biblia yamewatusi sana mitume.
 
Rudi upya ukafunze upya.
Divai ni neno lenye kumaanisha kinywaji kinachotokana na Zabibu. Kinaweza kutengeneza kinywaji baridi (juice), kinywaki kilichosindikwa (togwa), kinywaji kilichochachushwa (bia), kinywaji kikali (gongo), Dawa nk.
Yesu hakufanya muujiza wa kutengeneza pombe (bia au gongo).
Rejea yhn 2:1-11
 
Kwani kwenye amri 10 Kuna ulevi au kunywa pombe au mimi sielewi ukiristo.Utashangaa Kuna watu wanashupalia kunywa pombe ni dhmbi wakati hawakemei vitu vilivyoorodheshwa kwenye amri 10.ambavyo ndivyo vinavyo angamiza Dunia.Ubaya wa pombe ni kuwa ukilewa unatoa au unaondoa kujitambua hivyo nafsi yako inaweza kushambuliwa na vitu Vibaya ikiwemo hasira ,uzinzi nk ndio maana dini nyingi zinaona dhambi.
 
Hivi kunywa pombe ndiyo dhambi au kulewa ndiyo dhambi? Na kwanini katika dhambi zote inayotolewa macho sana ni dhambi inayohusisha unywaji na ulevi wa pombe? Dhambi zingine kama ushirikina, uzinzi, uchoyo, uwizi nk havizungumzwi sana.
 
Isaya 5:11
” Ole wao waamkao asubuhi na mapema, wapate kufuata kileo; wakishinda sana hata usiku wa manane mpaka mvinyo imewaka kama moto ndani yao! ”
 
Kwani kwenye amri 10 Kuna ulevi au kunywa pombe au mimi sielewi ukiristo.Utashangaa Kuna watu wanashupalia kunywa pombe ni dhmbi wakati hawakemei vitu vilivyoorodheshwa kwenye amri 10.ambavyo ndivyo vinavyo angamiza Dunia.Ubaya wa pombe ni kuwa ukilewa unatoa au unaondoa kujitambua hivyo nafsi yako inaweza kushambuliwa na vitu Vibaya ikiwemo hasira ,uzinzi nk ndio maana dini nyingi zinaona dhambi.
Isaya 5:11 ”
Ole wao waamkao asubuhi na mapema, wapate kufuata kileo; wakishinda sana hata usiku wa manane mpaka mvinyo imewaka kama moto ndani yao! ”
 
Back
Top Bottom