Baadhi ya Waumini wa Kanisa Katoliki waonekana wakinywa Konyagi nje ya Kanisa la Mt. Joseph

Baadhi ya Waumini wa Kanisa Katoliki waonekana wakinywa Konyagi nje ya Kanisa la Mt. Joseph

Kwa wakatoliki unywaji wa pombe yoyote (hata gongo!) sio dhambi. Na wakatoliki wanajivunia kunywa pombe popote ikiwemo hata kanisani, wao wanasema wanakunywa kistaarabu.

Pale ukatolikini hakuna ukristo halisi, ni upagani wa Kiitaliano ulioboreshwa kwa tamaduni zilizoupokea ukristo wa kale na kuueneza duniani chini ya mwamvuli wa kanisa.
Unywaji wa pombe: Katoliki hawauoni unywaji wa pombe kama dhambi, lakini wanasisitiza kiasi na matumizi ya pombe kwa staha. Divai hutumika pia katika ibada za Ekaristi.
Nkupe mfano ,!Harusi ya Kana (Yohana 2:1-11) inashuhudia Yesu akibadilisha maji kuwa divai, akionesha kuwa divai inaweza kutumika katika sherehe na furaha. Hii inathibitisha kwamba unywaji wa divai si dhambi, lakini inapaswa kutumika kwa kiasi na katika muktadha wa sherehe au ibada.
 
.
 
Attachments

  • images - 2025-01-01T143902.575.jpeg
    images - 2025-01-01T143902.575.jpeg
    32.9 KB · Views: 1
View attachment 3189715
Gazeti la Mwananchi limeonyesha kabisa Waamini wa Kanisa la Mtakatifu Joseph Dar es Salaam wakinywa Konyagi Kanisani.
Ni safii kabisa, kusherekea mwaka mpya, ilikuwa nje ya kanisa.

Jaribu kuelewa kanisa katoliki halina marufulu yoyote kuhusu pombe.

Pombe ni hiari ya mtu.Usitakake wakristu waishi marufuku ya pombe kama waislamu au walokole.

Kama unaona wivu batizwa nawe uanze kunywa Pombe!!

Mtoa uzi utakuwa mwislamu au mlokole, batizwa ugonge beer!! Unakunywa maji wewe umekuwa rejeta vya gari??😅😅🚴🚴🚴
 
Hatuachi ng'ooooooooooo kula vyomboo na tunazidi kubarikiwa
 
Hata wewe YESU KRISTO atakugeuza siku si nyingi utaanza kumwabudu. AMINA
Mimi nilizaliwa katika familia ya kikatoliki, sio wale mambulula wanaouziwa mafuta pale kwa Mwamposa wanaambiwa pokea gari lako na wao eti wanaweka mikono kwa ishara ya kupokea hilo gari halafu wakitoka hapo wanakwenda kugombea madaladala pale Morocco!.

Nauamini ukatoliki wangu nikijua kila kitu chema kipo katika kanisa langu.
 
Mada hapa ni tafrija ya kunywa gongo katika kanisa katoliki.
Hii imekaaje?
Huyo mpuuzi kaona gongo kati ya pombe zote zinazouzwa mjini?. Walokole mna taabu sana huwa mnasumbuliwa na ile roho ya upingaji (protesting) hata radio zenu huwa na mada za kipuuzi kama huu ujumbe wa huu uzi.

Yesu alisema kibaya ni kile kinachomtoka mtu kinywani sio kile kinachoingia. Hatuna unafiki katika suala la kumuabudu Mungu.
 
Unywaji wa pombe: Katoliki hawauoni unywaji wa pombe kama dhambi, lakini wanasisitiza kiasi na matumizi ya pombe kwa staha. Divai hutumika pia katika ibada za Ekaristi.
Nkupe mfano ,!Harusi ya Kana (Yohana 2:1-11) inashuhudia Yesu akibadilisha maji kuwa divai, akionesha kuwa divai inaweza kutumika katika sherehe na furaha. Hii inathibitisha kwamba unywaji wa divai si dhambi, lakini inapaswa kutumika kwa kiasi na katika muktadha wa sherehe au ibada.
Hawa wajinga wanajifanya kuijua vizuri Biblia kuliko mtu yoyote wanatakiwa wafahamu kwamba Padre wa kanisa katoliki anausomea upadre kwa miaka zaidi ya nane akijikita kwenye Theolojia.

Wakipata elimu ndogo tu za masuala ya Biblia wanahisi wamemaliza kila kitu, wakatoliki ni waungwana ni watu wa kujishusha huwa hatupendi kujibizana kwani ni kuendeleza roho ya uasi ambayo inawasumbua karne na karne.
 
Huyo mpuuzi kaona gongo kati ya pombe zote zinazouzwa mjini?. Walokole mna taabu sana huwa mnasumbuliwa na ile roho ya upingaji (protesting) hata radio zenu huwa na mada za kipuuzi kama huu ujumbe wa huu uzi.

Yesu alisema kibaya ni kile kinachomtoka mtu kinywani sio kile kinachoingia. Hatuna unafiki katika suala la kumuabudu Mungu.
Baba akili kabisa
 
Sawa 😹
 
Attachments

  • IMG_4168.jpeg
    IMG_4168.jpeg
    767.4 KB · Views: 1
Mkuu!

Itizame video vizuri umeona mtu akinywa pombe ndani ya Kanisa?jengo kabisa la Kanisa watu wakinywa pombe ndiyo video inachoonyesha?hapo ni nje ya jengo la Kanisa sehemu ambayo kuna wakati zinafanyika pia shughuli za kijamii tatizo watu wasiojua waandika vitu vya hovyo.
Mkuu Nenda Page ya St.Joseph Instagram kwenye Insta story utaamini nachokuambia watu wanapost mpaka Cocktails na Glass za Taquela Suala la kusingiziwa ni Uongo tena usilee dhambi Kumbuka hata kama ni nje ya Kanisa pale
Wewe ni shahidi Tukipita nje ya Kanisa kwa Wakatoliki Wanainama kidgo kwa ajili ya Kuabudu Sakramenti Takatifu na Msalaba Mtakatifu unaenda kufanya hayo makaramu ya Pombe mbele ya Kanisa Nafikiri hujui maandiko yanavyosema kwenye Mt 21:13 akawaambia, Imeandikwa, Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala; bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi.
 
Hivi najiuliza ni nani aliyeasisi huu Ushetani wa kufanya makaramu mbele ya Kanisa? Kama Kuna viongozi wa kikatoliki niambieni
 
Attachments

  • Screenshot_20250101-163517.png
    Screenshot_20250101-163517.png
    950.6 KB · Views: 1
Back
Top Bottom