Baba abaka mwanaye wa umri wa miaka 11 mkoani Manyara

Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara limesema linamtafuta mkazi wa Kata ya Magugu wilayani Babati, Frednand Yohana ambaye anatuhumiwa kumbaka mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka 11.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Benjamin Kuzaga ameyasema hayo leo Jumatatu Desemba 13, 2021 mjini Babati wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Kamanda Kuzaga amesema mkazi huyo wa Magugu alikuwa anambaka mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka 11 (jina lake linahifadhiwa) usiku wakati mke wake na watoto wengine wakiwa wamelala.

Amesema tukio hilo limefanyika kwa vipindi tofauti na lilibainika Desemba 6 mwaka huu baada ya mkewe kutoa taarifa Kituo cha Polisi Magugu.

Amesema taarifa za tukio hilo zimetolewa na mke wake, Justina Emmanuel ambapo mtoto huyo alikuwa anafanyiwa vitendo hivyo tangu mwezi Oktoba mwaka huu.

"Walikuwa wanaishi kwenye chumba kimoja mume, mke na watoto wao watatu na uchunguzi umeonyesha Yohana amembaka mtoto wake zaidi ya mara nne," amesema Kamanda Kuziga.

Amesema mtuhumiwa alitoroka baada ya mkewe kubaini kitendo hicho na polisi wanamtafuta ili afikishwe mahakamani.

View attachment 2043074
Unatamani katoto Kako ka miaka 11!!
Hata kama kana uzuri kama maraika!!
Mtoto wa kuzaa mwenyewe!!!
Hii hata shetani anakaa pembeni!!
 
Hata mimi mwenyewe nakubaliana na wewe, inawezekana hawa watu hawajakaa fresh kiakili. Kwa sababu haiingii akilini mzee mtoto wako wa kike, na wewe mzazi badala ya kuwa mlinzi wake wewe ndiyo unakuwa threat.
Hawa watu wapo sana na huwa naamini kabisa kuna kitu hakipo sawa kwenye maisha yao. Nakumbuka nilisoma story ya jamaa mmoja anaitwa Jeffrey Dahmer, huyu mwamba story yake unaweza usiamini. Niliingia mpaka Youtube nikasikiliza mahojiano yake ndiyo nikasema kweli watu psycho wapo na tunaishi nao bila kujua.
Mama amehamua kumshataki baba afungwe miaka 30!!!!!!!

Hapana hapo Kuna Jambo itakuwa huyo baba, mtoto na mama wote makabila tofauti
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara limesema linamtafuta mkazi wa Kata ya Magugu wilayani Babati, Frednand Yohana ambaye anatuhumiwa kumbaka mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka 11.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Benjamin Kuzaga ameyasema hayo leo Jumatatu Desemba 13, 2021 mjini Babati wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Kamanda Kuzaga amesema mkazi huyo wa Magugu alikuwa anambaka mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka 11 (jina lake linahifadhiwa) usiku wakati mke wake na watoto wengine wakiwa wamelala.

Amesema tukio hilo limefanyika kwa vipindi tofauti na lilibainika Desemba 6 mwaka huu baada ya mkewe kutoa taarifa Kituo cha Polisi Magugu.

Amesema taarifa za tukio hilo zimetolewa na mke wake, Justina Emmanuel ambapo mtoto huyo alikuwa anafanyiwa vitendo hivyo tangu mwezi Oktoba mwaka huu.

"Walikuwa wanaishi kwenye chumba kimoja mume, mke na watoto wao watatu na uchunguzi umeonyesha Yohana amembaka mtoto wake zaidi ya mara nne," amesema Kamanda Kuziga.

Amesema mtuhumiwa alitoroka baada ya mkewe kubaini kitendo hicho na polisi wanamtafuta ili afikishwe mahakamani.

View attachment 2043074

na ndo mwanzo wa Mateso ya familia bila Baba; wanaume wengine Ni sawa Na Ma Mbwa!
 
Back
Top Bottom