Baba ake Ommy Dimpoz alalamika kutengwa na mwanae

Huyo baba aache kulalamika, kwani yeye alimjengea msingi gani wa maisha mwanae
 
Kama hakumlea wala kumjali Ommy Hana obligation yoyote ila ya kujihusisha nae. Mzee apambane na hali yake tu Kama kijana alivyopambana na yake bila ya Baba
 
Mkuu umenena vyema, chukua bia nakurushia muamala
 
Kama mzee asingekuwepo kwenye picha yangu hakika ningemtelekeza acha hiyo laana nadharia inipate.

Ushenzi namba Moja ni kuikimbia damu yako afu bdae atoke ndo uanze kutaka akulee, laana inabidi impate yeye kwanza kabla yangu
 
Mbona anatudhalilisha wala mihogo wengine? Kwanza sio kushindia mihogo, ni kula mihogo, kama una matatizo na mwanao deal nayo mwenyewe achana na mihogo yetu. We mzee vipi?
Mkuu umenichekesha sana nashukuru
 
Uyo baba atafute pesa zake asimfanye mtoto kitega uchumi
 
hakuna kitu kinaitwa laana.
Nashangaa great thinker unawaza low hv
 
Point
 
Kumlea Mtoto ni jukumu la mzazi na wala sio hisani, yeye ndio aliamua kunileta duniani sikujileta mwenyewe, matunzo anayonipatia mzazi sio mkopo kwamba baadae niurudishe, ni wajibu wake..

Asilimia kubwa ya wazazi ndio chanzo kikubwa cha umasikini wa familia, wewe fikiria, hadi unakuwa mtu mzima kwenu hakuna hata nyumba ya maana ya kuishi, huyo mzazi wako unaemuonea huruma sana alikuwa bize na nini kwa miaka yote sitini aliyonayo?!, kama siyo uvivu na upuuzi tu.
 
Dah Hii kali! Yaani nitafute mali kwa ajili ya kumuachia mtoto urithi. Minajua mzazi wajibu wake ni kumsomeaha mtoto tu, mali zangu ni kwa maiaha yangu,huyo mtoto atatafuta za kwake.
Hapo ni sawa, kumuachia mtoto urithi sio lazima wala sheria, ila kwa sababu wew ndio uliemleta duniani, inamake sense kidogo kumpa walau msingi wa kuanzia maisha, asio wewe mzazi kuza mtoto halafu unaanza kusumbua ukitaka huyo mtoto akulee wewe.
 
Wazee wengine bhana pasua kichwa tu.
 
Urithi si lazima, ila mzazi kutaka kutunzwa na wanao ndio akili ya kipuuzi, yeye huyo dingi naekula mihogo hapo anawatunza wazazi wake?, au yeye anataka kutunzwa tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…