Baba ake Ommy Dimpoz alalamika kutengwa na mwanae

Baba ake Ommy Dimpoz alalamika kutengwa na mwanae

Huyo baba aache kulalamika, kwani yeye alimjengea msingi gani wa maisha mwanae
 
Kama hakumlea wala kumjali Ommy Hana obligation yoyote ila ya kujihusisha nae. Mzee apambane na hali yake tu Kama kijana alivyopambana na yake bila ya Baba
 
Hapa mimi kidogo huwa nina mtazamo tofauti, naamini kuwa huyo mzazi anatakiwa akomae na hiyo bajaji yake ampatie Ommy Dimpoz pesa, sio pesa tu, atafute mali zaidi ili ikiwezekana Dimpoz aje kurithi... MZAZI MWENYE BUSARA HUACHA URITHI WA MALI KWA WANAWE! LAKINI MPUMBAVU HUTAPANYA MALI KWA POMBE NA UZINZI KISHA HULALAMIKA KUWA WANAWE HAWAMJALI.
Mkuu umenena vyema, chukua bia nakurushia muamala
 
Mzazi ni mzazi regardless alikutenda nini. Hata uwe na justification gani ....ukimtelekeza laana itakutafuna tu one day .... kama unabisha hewala lakini uliza waliokula chumvi kidogo wakupe shuhuda ....mzazi kushindwa kukuachia urithi wowote hiyo itabakia adhabu kwake na pengine ndio anapitia adhabu yenyewe kwa namna nyingine lakini wewe hupaswi kumtelekeza kwa makusudi.
Kama mzee asingekuwepo kwenye picha yangu hakika ningemtelekeza acha hiyo laana nadharia inipate.

Ushenzi namba Moja ni kuikimbia damu yako afu bdae atoke ndo uanze kutaka akulee, laana inabidi impate yeye kwanza kabla yangu
 
Mbona anatudhalilisha wala mihogo wengine? Kwanza sio kushindia mihogo, ni kula mihogo, kama una matatizo na mwanao deal nayo mwenyewe achana na mihogo yetu. We mzee vipi?
Mkuu umenichekesha sana nashukuru
 
Uyo baba atafute pesa zake asimfanye mtoto kitega uchumi
 
Mzazi ni mzazi regardless alikutenda nini. Hata uwe na justification gani ....ukimtelekeza laana itakutafuna tu one day .... kama unabisha hewala lakini uliza waliokula chumvi kidogo wakupe shuhuda ....mzazi kushindwa kukuachia urithi wowote hiyo itabakia adhabu kwake na pengine ndio anapitia adhabu yenyewe kwa namna nyingine lakini wewe hupaswi kumtelekeza kwa makusudi.
hakuna kitu kinaitwa laana.
Nashangaa great thinker unawaza low hv
 
Usichanganye mambo. Alinizaa na kunilea ikiwa ni wajibu wake. Wajibu wangu ni kulea watoto wangu nao waje kuwalea watoto wao. Na ndio maana unashauriwa kama huna uwezo wa kulea watoto usiwazae ukitegemea watakuja kukulea wewe! We ndio wale wanaosema kila mtoto anakuja na riziki yake eeeeee we fyatua tu ushindwe kujijenga halafu uone kama kesho watakulea.
Point
 
Alikuwa anahangaika kumlea huyo Ommy.
Nisivyokuwa na baba roho imeniuma watoto mnaowaongelea vibaya wazazi wenu kumbukeni mzazi ni Mungu wa pili wadunia Waheshimu wazazi wako upate marefu maisha Duniani. Mzazi ni mzazi hata akiwa fukara .unachowafanyia wazazi wako na watoto wako watakuja kukufanyia hivyo hivyo.
Kumlea Mtoto ni jukumu la mzazi na wala sio hisani, yeye ndio aliamua kunileta duniani sikujileta mwenyewe, matunzo anayonipatia mzazi sio mkopo kwamba baadae niurudishe, ni wajibu wake..

Asilimia kubwa ya wazazi ndio chanzo kikubwa cha umasikini wa familia, wewe fikiria, hadi unakuwa mtu mzima kwenu hakuna hata nyumba ya maana ya kuishi, huyo mzazi wako unaemuonea huruma sana alikuwa bize na nini kwa miaka yote sitini aliyonayo?!, kama siyo uvivu na upuuzi tu.
 
Dah Hii kali! Yaani nitafute mali kwa ajili ya kumuachia mtoto urithi. Minajua mzazi wajibu wake ni kumsomeaha mtoto tu, mali zangu ni kwa maiaha yangu,huyo mtoto atatafuta za kwake.
Hapo ni sawa, kumuachia mtoto urithi sio lazima wala sheria, ila kwa sababu wew ndio uliemleta duniani, inamake sense kidogo kumpa walau msingi wa kuanzia maisha, asio wewe mzazi kuza mtoto halafu unaanza kusumbua ukitaka huyo mtoto akulee wewe.
 
Wazee wengine bhana pasua kichwa tu.
 
Akili ya kipuuzi kabisa mzazi wako nilazima umtunze kadiri uwezavyo haijalishi yeye alikutelekeza wewe timiza wajibu wako kufikiria kurithi ni akili ya kipuuzi na nyinyi vijana acheni kuwahukumu wazazi wa kiume hamjui mama zenu waliwafanyia nini wazee hadi kutelekezwa ngoja muwafume hao wakezenu wakichepuka kama mtaweza kuwavumilia
Urithi si lazima, ila mzazi kutaka kutunzwa na wanao ndio akili ya kipuuzi, yeye huyo dingi naekula mihogo hapo anawatunza wazazi wake?, au yeye anataka kutunzwa tu?
 
Back
Top Bottom