Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Mzee Gideon Kisira Cherowo (73) Mkazi wa Birunda nchini Kenya amemfungulia kesi Mtoto wake aitwaye Washington Chepkombe akitaka akatwe asilimia 20 ya mshahara wake ili apewe Mzee huyo kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya Familia kwakuwa Mtoto wake huyo hampi msaada licha ya kuwa na kazi nzuri na fedha nyingi.
Mzee huyo anasema alilazimika kuuza hadi ardhi yake na mali zake nyingine ili kulipia ada za masomo ya Mtoto wake huyo hadi Chuo Kikuu na akafanikiwa kupata kazi kwenye Mamlaka ya Viwanja vya Ndege lakini baada ya kupata kazi hampi msaada.
Mzee huyo amesema ana Watoto wanne lakini mwenye kazi ni Washington pekee na kusema kwa sasa yeye na Familia yake wanaishi katika nyumba ya udongo kijijini kwao huku Mtoto wao mwenye uwezo akila starehe Mjini.
"Nimepambana sana kumtafutia maisha Mtoto ili atusaidie lakini hatupi msaada kwakuwa mshahara wake ni mzuri nimefungua kesi ili 20% ya mshahara wake nilipwe Mimi"
Millard Ayo