Baba arudi nyumbani mikono mitupu baada ya kupotea kwa miaka 42

Big No mkuu, miaka 42 sio mchezo. Then anarudi na jibu rahisi tu "eti alienda kutafuta maisha"
[emoji3][emoji3],mkuu hebu soma tena kisa chake naona mleta mada kaongeza habari zaidi,hata yeye hakupenda hali hio na kama alivyosema alianzia kwenye madini baadae akaenda usukumani kuchunga mifugo,na hio kazi ndugu wenye mifugo huwa lazima 'wakuweke sawa'huchomoki ni kama wahindi tu,we fikiria mtu alikosa hata nauli mpaka alipokuja kuchomolewa na Pasta.Mi naamini haikuwa kawaida na isitoshe hata kuoa hakuoa mke yeyote ugenini.
 
Mzee inaonekana alipiga mawe hapo Maroroni halafu akatekwa na binti wa kibongo akapewa mahaba yakufa mtu mpaka akasahau malengo yaliyomleta bongo.
Mwanzo nilidhani hivyo mpaka habari kamili ilipoletwa ndio nikajua huyu alikutana na masaibu ya ulimwengu tu,maana hakuwahi kuoa huku ugenini
 
Namsubiria tu mzee kazamia huko Kenya huu ni mwaka wa 20
 
Wanga hao, kuna kufukuzwa na usiwaze kurudi, au kushikiliwa ulipo usikumbuke wapi umetoka.Ninamfahamu mmoja alishikiliwa mahali kwa madawa mpaka nyumbani kwao walipofanya nao makaratee ndio akakurupuka, yeye alirudi akitokea hospital alitoroka wodini anadai anataka kurudi kwao kichaa kimepanda kukanyaga tu ardhi ya kwao kichaa kikaishia hapohapo.Hajawahi tena kurejea kule alikolowea na hataki kabisa kupasikia.
 
Uko sahihi nimeshaona watumishi kadhaa wameshikwa hawataki hata kusikia familia zao Tabora huko mpaka familia walipofanya' yao 'na kuja kuwachukua ndio na wao akili zikarudi.

Hii dunia ina mambo sana,Kuna askari alikuwa anajifungia kwa demu haendi kazini mpaka mkuu wake anatuma vijana kufanya msako kumchukua kwanguvu.
 
Hii stori imenihuzunisha sana
 
Sema mzee Alifeli, kwahiyo katika sehemu zote alizotazamia kutafuta aliona Tanzania hahaha Dah. Cha muhimu Amekumbuka hata Kurudi nyumbani. Kuhusu bond na mambo mengine tuyaaache kama yalivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…