Baba Askofu Dr. Alex Gehaz Malasusa, Mkuu wa KKKT na mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Hospital ya KCMC ! KCMC ipo ICU!

Niliwahi lazwa pale kwa wiki zaidi ya2(siku17) niliona mengi lakini kwenye kitengo nilichokuwa nimelazwa (dermatology) wako vizuri sana nawapa zote. Ila ukienda wodi zingine basi inatosha asee.
 
Fedha za GSF KCMC ni nyingi,na xinawapa viburi viongozi wa Hospital,wanajisahau.

CAG sidhani Kama anafahamu na aliwahi kukagua GSF
 
Hata Muhimbili maprofesor wa Muhas hawaoni wagonjwa baada ya serikali kuwapa Muhimbili hospitali ya Mloganzila.
 
*Careplus Health Centre, Moshi, Tanzania*ni sehemu ya hospital ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini????
Nimeuliza TU,ila ikiwezekana TAKUKURU,TISS NA Champa cha madaktari Tanzania,kitembelee kituo hiki na kukikagua,kuanzia uongozinna utawala wake, mifumo yake, eneo kilipo,huduma zake.
Mtanikumbuka.
 
Dr Sarah Urassa, kazi aliyopewa haiendani na ukubwa wa kurungenzi!
Hii amepewa ili kulinda jina la baba tu.
Ila kazi hajui na hawezi,apishe wengine wenye uwezo nayo na uzoefu nayo .
 
Kwa ivo malasusa afanye nini?
Mimi nafikiri lile fungu SERIKALI inatoa kuziwezesha Hospitali za Lutheran lielekezwe moja kwa moja kwenye Uendeshaji wa Hospitali kwani hata Selian kule Arusha hali yake ni ya kuunga unga.
Nafikiri ipo haja pia ya kuangalia bei wanazotoza ukizingatia wanapata Ruzuku ya kodi za Watanzania.
 
Hiyo ni kasumba za hospital nyingi sana ambazo zinajiita za referral ambazo zipo chini ya taasisi za kidini au binafsi
 
Miradi mingi ya KKKT hasa Dayosisi ya Kaskazini ina Hali mbaya sana... Kuanzia Mashule, Vyuo na hata hizi Hospitali..

Nakumbuka kipindi cha Uongozi wa Dr. Erasto Kweka Kila kitu kilikuwa kinaenda vizuri.. Huyu Shoo na wasaidizi wake hovyo kabisa.!
 
Hela za kkkt zinakwenda wapi?
Mbona kanisa lina waumini wengi na watoaji wazuri?
 
Sasa unamfokea nani? Kama hukubali kufokewa na nesi na wewe usilete mgonjwa acha!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…