BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
Na baba Askofu Stephen Munga
JE, ASKOFU MWAMAKULA NI MFIA IMANI NA SHUJAA?!
Kwa muda sasa tulikuwa tukimsikia Baba Askofu Emmaus Mwamakula akiandaa matembezi ya hiari kwa ajili ya kudai Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya. Haya ni matakwa ya watu wengi kulingana na maoni yaliyomo katika taarifa ya Tume ya Warioba. Kwa hiyo kwa Watanzania, anachokisema Askofu Mwamakula sio jambo jipya na wala sio matakwa yake bali anakariri maoni ya wengi.
Jana ilisikika kwamba Baba Askofu amechukuliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano. Ni matumaini yangu, kama waonavyo watu wengine, kwamba polisi watatenda kwa haki pasipo kuvunja sheria au kukiuka misingi ya haki za binadamu wanaposhughulikia jambo la Baba Askofu Mwamakula. Tunashukuru kwamba Baba Askofu ameachiliwa kwa dhamana.
Nia yangu hasa ni kutafakari kwa kifupi falsafa muhimu ninayoiona katika juhudi za Askofu Mwamakula. Huu ni ufafanuzi wangu kwa jinsi ninavyomuelewa Baba Askofu kupitia maandiko yake. Askofu Mwamakula ni msomi wa theologia na falsafa kwa hiyo naamini kwamba hapa tunavinjari pamoja katika ukurasa mmoja. Mawazo niwekayo hapa sio hekaya bali ni jambo la msingi katika mijadala katika historia ya Wafia Imani (matyrs) ambao pia huitwa mashujaa wa imani. Nakiri kwamba nilichoandika hapa ni tone tu katika bahari ya maarifa juu ya elime ya Wafia Imani na mashujaa.
Mara kadhaa nilivyokuwa namsoma Baba Askofu Mwamakula nilikuwa najiuliza: Je, ni kwa roho gani anafanya haya? Mbona hana hofu wala wasiwasi? Mbona amejiingiza katika misioni ngumu na ya hatari hivi? Majibu sahihi ya maswali kama hayo anayo Baba Askofu Mwamakula moyoni mwake. Mawazo yangu hapa ni maelezo ya ulinganifu kati ya niliyoyasoma kwa Askofu Mwamakula na maarifa nijuayo kutoka historia juu ya mambo yafananayo na hayo.
Mfia imani ni mtu yule anayechagua kujitoa kafara ya maisha yake. Huyu anakubali maumivu na mateso badala ya kuachilia msimamo/mtazamo wake juu ya kitu anachosadiki kuwa ni kitakatifu au cha thamani kuu. Sifa kubwa ya kundi lao ni kwamba watu wa jinsi hiyo hawamaliziki kwa mateso na vifo. Mateso na vifo ndio kichocheo cha kuwaongezea nguvu, msimamo na ushirikiano. Tena Upo usemi kwamba damu yao inayomwagwa ndio mbegu ya kuzalisha mashahidi wengi zaidi.
Mfia imani ni shujaa. Ushujaa wa mfia imani umo katika kiapo cha kutimiza wajibu au utume/misioni yake. Kwa hiyo kwa shujaa kuutoa uhai wake ni utumishi kwa kutimilika kwa kiapo cha wajibu wake.
Mfia imani na shujaa hufa kila mmoja peke yake. Wafia imani ni wingi wa mfia imani mmojammoja. Mashujaa ni wingi wa shujaa mmojammoja. Kila mmoja hufa kwa kiapo chake. Hata wakifa hamsini kwa mara moja kila mmoja peke yake ni shujaa. Tena katika hao hamsini kifo cha kila mmoja kina nguvu na uzito mkubwa sawa na wote kwa pamoja.
Mwiko na adui mkubwa wa mashahidi wafia imani ni woga. Vilevile mwiko na adui mkubwa wa mashujaa ni woga. Nimesoma historia lakini sijawahi kusikia mfia imani mwoga na shujaa mwoga. Mtu mwoga kwa kawaida hukimbia mateso na kifo. Kukimbia huko kwaweza kuwa kwa njia ya kukana imani au kusaliti kwa kutoa siri za misioni na kundi. Ndio sababu Bwana Yesu aliangaliza kwamba waoga hawataingia mbinguni.
Wafia imani na mashujaa sio waoga. Hii haina maana kwamba mashujaa wachezee uhai wao na kujiachilia ovyo kwa mateso na vifo. La hasha! Makundi haya yote ni mawakili wa uhai wao kwa kiwango cha juu. Bali inapofikia hatua ya kwamba hakuna vinginevyo ndipo huchagua kifo na mateso baadala ya kukana imani na kusaliti kiapo cha utumishi.
Ikiwa anayofanya Askofu Mwamakula ni roho ya imani yake; na kwamba katika kiapo chake cha kichungaji afanyalo ni wajibu wake; basi hatanyamaza. Hili silo jambo la kuigiza kwani hakuna maigizo katika viapo vya utume. Pia katika mazingira ya jinsi hiyo shujaa yu tayari kufa peke yake kwa sababu ya imani na kiapo. Ndivyo alivyokufa Yohana Mbatizaji; ndivyo alivyokufa Bwana Yesu; na ndivyo walivyokufa Manabii, Mitume na Wafuasi waaminifu wa Kristo. Hawa wote walikufa huku watu wachache wakikubaliana nao bali walio wengi wakiwashutumu na kuwalaumu.
Msukumo wa ndani juu ya malengo ya kampeni hii anayo Baba Askofu Mwamakula. Ameifanya hii kuwa ni misioni yake ya kupigania mambo yale mawili. Namuombea Baba Askofu Mwamakula ili awe na afya njema kimwili na kiroho katika kipindi hiki kigumu kwake. Nawaombea na watu wengine wote waliomo katika mazingira kama hayo ya Askofu Mwamakula. Pia naliombea Jeshi la Polisi ili litimize wajibu wake kwa ufanisi na kutenda haki. Nawapongeza wale wote waliosimama na Askofu Mwamakula na kupaza sauti zao. Bila shaka walifanya hivyo kwa mioyo ya upendo na kiu ya haki. Pia naamini kwamba walipaza sauti wakijua kwamba mamlaka husika, hususan jeshi la polisi, zitasikiliza na kuchukua hatua kama walivyofanya.
Amani iwe kwenu.