Baba Askofu Munga: Je, Askofu Mwamakula ni mfia imani na shujaa?

Baba Askofu Munga: Je, Askofu Mwamakula ni mfia imani na shujaa?

Huyu alipodai tuwe na Tume huru alikuwa anatafuta kiki toka kwa nani?
1613591033142.jpeg
 
Huyu ni Askofu wa kweli na anachosimamia kina baraka ya watanzania wengi.
 
Kwa mwenye akili fupi kama ZWAZWA wewe! Kudai katiba mpya na Tume huru ni kutafuta kiki. Watanzania kama wewe ni nzigo mkubwa sana.,
Kesho dikteta akikubali kuandika katiba mpya utasikia yanasifia kuwa ni msikivu mno na mpenda watu
 
Duh, Mkuu BAK, nimevunja sheria. Kwa jinsi nilivyoguswa na ujumbe wa Askofu nimeunakili ili niweze kuusoma kirahisi siku zijzo hata pale nitakapoishiwa kifurushi. Sasa sijui nitashtakiwa na nani, sijui ni wewe, Askofu au jamii Forum. Mwenye haki hiyo anihurumie bure. Kilangila.
 
Wako vizuri sana Mkuu. Imagine kama viongozi wote wa dini bila kujali imani zao wangekuwa na misimamo thabiti kama hawa katika kupinga maovu na udhalimu wa huyo anayejiita mwendawazimu, ni lazima angekaa chini na kusalimu amri.
Wako walio amua kumuabudu na kumsifu Lucifer, badala ya MUNGU na kondoo wake walio apa kuwatumikia. Kilangila.
 
Daa -be askofu
Dawa pekee ya kuiondoa ccm ni kupitia Tume Huru ya Uchaguzi na pia Katiba ya Wananchi.

Hivyo namuunga mkono huyo Askofu Mwamakula kwa ujasiri wake wa kuwasemea mamilioni ya Watanzania wapenda mabadiliko.
Daaah, kumbe Askofu Mwamakula anataka kuleta dawa itayoitoa CCM madarakani.... Ok sasa nimeelewa na nimemuelewa vzr na hata Polisi nao nimewaelewa🤔🤔
 
Ukigusa maswala ya "KATIBA MPYA" tu ujue umegusa maslahi ya Watawala wa CCM na CCM yenyewe...

Ukigusa sharubu za simba, mrejesho wake ni kurauliwa kisawasawa na simba huyo...

Kwa namna mambosasa alivyokuwa analishughulikia jambo hili la Baba Askofu Mwamakula, na kwa jinsi alivyokuwa anaropoka hovyo kwa lugha isiyo na staha wala maadili yenye nia ya kumdhalilisha Baba Askofu Emmaus Mwamakula, ni wazi kuwa amepewa "go ahead" na watawala kumshughulikia...

Lakini obviously, kwa mwenye akili timamu, na kwa mujibu wa sheria za Tanzania, Baba Askofu hakuna kosa lolote la kisheria alilofanya kwa sababu mtu kusema anahitaji katiba mpya na kuwahamasisha wengine wamuunge mkono si kosa la halijawahi kuwa kosa...

Hivyo kamanda wa polisi Kanda maalumu - DSM, afande Mambosasa anajua hili fika kuwa Askofu hana kosa lolote lakini kaamua kujitoa ufahamu ili kuwafurahisha "mabwana zake", waliomtuma ili wamlipe mshahara ajaze tumbo lake na kwenda chooni kujisaidia tu...!
Kuna kitu kiko wazi. Hakuna mtawala mwenye nguvu bila bunduki. Nguvu ya watawala iko nyuma ya washika bunduki. Tatizo hawa hutii watawala na sio raia. Saluti kwa watawala virungu kwa raia.
 
Back
Top Bottom