Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,242
- 34,903
Alipokuwa mchezaji wa Yanga, Simba walimsema ni bomu (dhaifu) na hana lolote.
Amejiunga na Simba, sasa Simba wanasema wamesajiri jembe la uhakika. Nao Yanga wanasema Simba wamechukua bomu ambalo litawalipukia.
Mchezaji mwenyewe alipokuwa Yanga, alisema yeye ni Yanga na Yanga ni yeye. Hata damu yake alisema ni ya kijani.
Sasa kaenda Simba, anasema hatimaye amefika nyumbani. Anadai hata Mungu alipomuumba alimwambia yeye ni Simba.
Kuna kitu hakiko sawa. Ukiwa muongo usiwe msahaulifu. Ukikosa uaminifu uwe mwangalifu. Umaskini wa fikra unazitafuna siasa na soka la Tanzania. Kuna siku mtamsingizia tasa kuwa ana mimba (na mwenye mimba kuwa tasa).!