Baba Diamond aomba mwanae amkatie angalau bima ya afya

wazazi wakiachana, wao ndio wanajua siri za chumbani kwao kwanini wameachana. hivi kwa tabia ya mama diamond anayoonyesha kama ile, Diamond ashukuru Mungu huyo mzee alivumilia hata akazaa naye mtoto na akamlea wakiishi na huyo bibi hadi yeye alipokuwa form one. kama uzeeni anaonyesha tabia kama zile, akiwa kijana na baba diamond alikuwaje? bure kabisa.

yeye anaweza kumchukia babake kumbe hajui siri iliyowafanya waachane, anataka babake amweleze na yote ya chumbani waliyokuwa wanayafanya hadi wakaachana? kwani yeye mbona anaacha na kuachwa vilevile? watoto wa Zari wakija kumchukia atajisikiaje? ajabu yake na yeye naye amezaa hovyo nje ya ndoa kama babake, yatakuja kumrudi.
 
Watajaza wenyewe na maisha yao. Ila niseme tu huyo baba awache kulalamika kwenye vyombo vya habari sababu suluhu haipatikani huko.
Vyombo vya habari ktk kutafuta habari za kuuzia magazeti na kupata viewer kwenye blog zao ndio uwa wanamfuata huyo mzee,but ni aibu kwa diamond kumfanyia haya baba yake mzazi,hata kama kuna tofauti kati yao amgejaribu kuificha japo kwa vijimsaada vidogo vidogo ili isifikie hatua km hiyo ya maradhi na kushindwa kupata kumudu gharama za matibabu,shame on him,angetuuliza sisi ambao Baba zetu wametangulia mbele ya haki tungemuambia thamani ya Baba ilivyo
 
dingi piga chini uyo mtoto fanya km ukuzaa tu maana unalalamika sana alafu akuna msaada wowote isitoshe wewe ni baba yule mtoto muache afanye mambo yake pigana kiume usimame imara,ipo siku umuhimu wako utaonekana
hizo ni dua za kuku!

kama mzazi anashindwa kutimiza majukumu yake asitegemee mtoto aje atimize majukumu yake kwako.

Tunatakiwa kuwazaa kuwahudumia na kuwafanya marafiki zetu(watoto) watatupenda sana na watatoa walichonacho kwa moyo pale tunapoishiwa nguvu.

Hizi habari za kukimbia majukumu halafu uzeeni nguvu huna ndo utafute watoto haya ndo majibu yake akubaliane na hali halisi aliyoitengeneza.

Kuna mpuuzi mmoja wa chatle akawa anawaambia zaeni tu ardhi mnayo bila kujali urthi ni zaidi ya ardhi.
 
Hivi unadhani Peter Manyika mwanae amekuwa golikipa by accident au by chance??
 
Za kikristu zinatupa haya mafundisho ya kusamehe saba mara sabini, SIJUI DINI ZINGINE
kama mzazi alishindwa kuwasamehe( kama walimkosea akawakimbia) hii ya mtoto kusamehe itatoka wapi ilihali mtoto wa nyoka ni nyoka.

me naomba aendelee kuonyooshwa tu hadi mwisho ili iwe elimu tosha kwa watu wapuuzi kama yeye.
 
Hata joseph aliuzwa utumwani lakini hiyo haikufanya iwe kikwazo kwake kufika juu bali ilikua ni ngazi/njia ili afike aendapo ,Sioni sababu ya mtoto kumkazia baba hivi hata kama alikosea Na naamini ipo siku diamond atajirudi tu DAMU NZITO kuliko MAZIWA
 
Kuna baadhi ya vitu ukifanyiwa na mzazi au mtu aliyekuzidi sana umri Ukiwa mdogo vinakuaafect kikubwa sana
Tulee vizuri watoto wetu vizuri
 
Hakuna mchuno kwenye njaa wewe
 
Ila hii ni roho ngumu.
Siku ya kuzaliwa kagawa zawadi na kafungua mradi wa bodaboda kwa watu wa Tandale, baba yake hamjali?

Ingekuwa mwanamke labda ningeelewa katekwa na mama yake, ila yeye ni mwanaume tena ana tabia za ufuska kuliko alivyokuwa kuwa huyo babake anashindwaje kuelewa kuna wakati mwanaume akishikwa na mwanamke mjanja yuko radhi hata kutelekeza familia.
 
kama mzazi alishindwa kuwasamehe( kama walimkosea akawakimbia) hii ya mtoto kusamehe itatoka wapi ilihali mtoto wa nyoka ni nyoka.

me naomba aendelee kuonyooshwa tu hadi mwisho ili iwe elimu tosha kwa watu wapuuzi kama yeye.
Na katika hili, UKRISTU UNASEMA, KISASI NI JUU YA BWANA... hatutakiwi kufanyiana visasi
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Shida sio diamond...

SHIDA NI MAMA YAKEE..!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…