Baba Diamond aomba mwanae amkatie angalau bima ya afya

Kuna siku nilimuona pale manzese yani kachoka balaa...anatia huruma sana yule mzee!![emoji52][emoji52][emoji52]
 
Mzee mpuuzi hivi aliyemwambia akiongea kwenye media ndio ataonewa huruma ni nani?

Huyu mwenyewe amezaa mitoto kibao kila mtu na mama yake na ameshindwa kutimiza majukumu yake, siku zote mtoto ukimpa upendo atarudisha upendo, ukimpa kisogo nae anakupa kisogo.

Mimi ningekuwa huyo mzee ningetafuta watu wa karibu wenye busara ambao mama Diamond anawaheshim na atafute wazee wa dini, wakae na mama Diamond, baadaye ndipo wa mwite Diamond akiri makosa yake mbele ya huo mkutano. Sasa yy kwa upuuzi wake anaenda kwenye vyombo vya habari, hata mimi ningekuwa Diamond ningekaza.

Mimi mzee wangu juzi juzi ametoka kumpatanisha binti mmoja na baba yake na baba yake baada kutimuliwa na panga na babu yake, kawatafuta wazee ambao yule babu anawaheshimu, wakafanya kikao wakaya maliza, sasa ww kulialia kila siku anakosea.

Hili nalo liwe funzo kwa wazee wanaokimbia majukumu kwani uliyetafuta naye kuni, ndiye wakuota naye moto.
 
Niye mutaalibu mambo bana, ishu iliuopo Diamond kaandaa siku yake ya Baba iyo ndio siku atamsamee na kumchua kumpeleka kwenye nyumba yake na kumfungulia biashara, pesa kwenye account, bima na gari.

Mutaaribu mambo, hii ni siri nimeitoa.
 
Baba mwenye busara na anaye jua aliteleza wapi hawezi kulia lia mbele za watu kutafuta suluhisho bila kushirikisha watu alio kosana nao.
Ambacho angefanya tangu mwanzo, angeonana na mzazi mwenzie kuyaweka sawa matatizo yao. Angemwita Nasibu (sio Diamond) nyumbani,angemuelekeza matatizo yaliyo pelekea kutengana na mama yake pasipo kuingia kiundani maana bado ni mtoto tu. Mwisho angemuomba msamaha mwanae.

Muda wa kuondoka angempa mwanae zawadi ya hata pea moja ya raba na tisheti kukumbushia zamani alivyo kuwa anamjali. Angemuomba awe anafika mara nyingi awezavyo pindi apatapo nafasi.
Kutumia vyombo vya habari mara nyingi huumiza upande wa pili. Ni sawa na mambo yangu ya ndani nije niyasikie mtaa wa pili.
Mzazi ana nafasi ya kumpata mwanae ikiwa tu atajishusha maana mwenye kosa ni yeye.
 
Niye mutaalibu mambo bana, ishu iliuopo Diamond kaandaa siku yake ya Baba iyo ndio siku atamsamee na kumchua kumpeleka kwenye nyumba yake na kumfungulia biashara, pesa kwenye account, bima na gari.

Mutaaribu mambo, hii ni siri nimeitoa.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Labda mama ake akiwa amekufaa...!!
 
"Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini."
(1 Timotheo 5: )
 
"Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini."
(1 Timotheo 5: )
Baba ake alianza kuwa mbaya....!! Diamond anamsikiliza sana mama ake hilo ndo tatzo
 
Mtu amtagi Baba Dimond please apate ABC hapa kabla Dimond ajawaomba mod wafute hii[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
"Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini."
(1 Timotheo 5: )
Sasa rafiki kama mtu aliweka mbegu kwa starehe zake kisha akasepa na hakufanya matunzo yoyote yale huyo mtu anastahili msaada wa nini sasa?
 
Naafikiana na wewe kabisa ila huyu mzee anataka sympathy kwa watu wa nje.
Wazazi wanatengana lakini kama kuna watoto basi hapo hawajaenda mbali bali wapo kimawazo kwa ajili ya watoto.
Mwanaume hashindwi kuongea na mke wake wa zamani hata kama kulikuwa na tatizo kubwa kiasi gani, kwani binadamu tunakosana na kuyamaliza.
 
Msaada kwa mtoto hauombwi, ukishawazaa, walea na wakijitegemea, waachie wao waamuwe, mzee anakosea kwenda kwenye vyombo vya habari, anaidhalilisha familia yake, yeye ahemee kwa nguvu zake na aridhike anachopata kwa jasho lake, misaada ya watoto ni majaliwa..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…