Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuna mtu hapo juu amepropose kiba amlipie huyu mzee ili apate Kiki. Nafikiri pia inaweza kumzindua akili dimondoMi sidhani kama anataka aombwe radhi! Ninachokiona ni kwamba, Bi Sandra alimlisha sumu mbaya sana mwanae dhidi ya babake! Na hii tabia wanawake wanayo sana... tabia za kuwajengea chuki watoto dhidi ya baba pale unapotokea uhasama wa kindoa!!
Huyu Mzee Abdul nae ana tatizo moja! Anapenda sana kulia lia kwenye media; tena afadhali safari ametumia serious newspaper manake media yake kubwa Shigongo Line na Shilawadu!!
Nilishangaa siku moja eti Uwazi waliripoti taarifa ya Mzee Abdul tangu anatoka Magomeni hadi anagonga mlango pale Sinza... na mapicha juu! Sasa mtu unajiuliza hawa Uwazi walifahamu vp kwamba Mzee Abdul anataka kwenda Sinza! Na matukio ya aina hiyo sio moja; ambayo yalikuwa yanaonesha kabisa kwamba, Shigongo akitaka kuuza magazeti yake; wanaenda kumpanga Mzee Abdul... in short walikuwa wanamtumia!!
For what I know, Diamond kesha msamehe babake but the question is; kama alichoongea ni kweli, sasa ni kwanini anashindwa kumsaidia!!
All in all, I can't judge Diamond manake sijui aliyopitia! Na haya mambo haya, fanya kusikia kwa wenzako!
Huenda masharti ya mganga wake ni kumpuuza baba yake. Amsaidie baba afirisike!Akifanya mahojiano na gazeti mwananchi baba mzazi wa msanii diamond platnumz ambemuomba mwanae angalau amkatie bima ya afya kwani Hali yake kwa Sasa sio nzuri. Ilinichukua muda kumshawishi na baadaye kufanya mahojiano na Abdul Juma Isack ambaye ni baba wa msanii wa maarufu wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz. Ungeweza kukata tamaa ya kuendelea kumshawishi kwa sababu ana hoja nyingi na pengine nzito.
“Sioni mabadiliko kwangu,” anasema baba huyo mwenye umri wa miaka 52 wakati akieleza sababu za kukataa kufanya mahojiano. “Tangu nianze kuhojiwa, nilikuwa nikiamini kuwa ningeweza kubadili msimamo wa mwanangu anayetajwa kuwa msanii tajiri namba moja Tanzania. “Badala yake naonekana kama nalilia kusaidiwa na mtoto wangu. Pamoja na kuwa na mtoto maarufu ndani na nje ya nchi, maisha yangu ndio kama hivi unavyoyaona. Naishi Magomeni Kagera na nyumba yangu ya kawaida tu, ambayo naamini hata siku Diamond akikwama kimaisha atakuja kuishi kwa kuwa hapa ni kwao, japokuwa simuombei hilo.”
Abdul anasema kwa muda mrefu Diamond amekuwa hafanyi mawasiliano naye na hajui sababu . “Najiuliza ni nini kikubwa namna hiyo nilichomkosea?” anahoji baba huyo. “Ninatamani siku moja nikutanishwe katika mahojiano na Diamond na mama yake ili kila mmoja atoe alilonalo moyoni.“Huyu mtoto kanipa majina mengi kutokana na yanayoongelewa mtaani kwamba nilimtelekeza, wakati hakuna ukweli wowote. Mimi niliachana na mama yake wakati akiwa kidato cha kwanza.
Kwa umri hu alikuwa anajielewa na anajua sababu za kuachana kwetu. Kama kuna jingine wanalolijua wao kwamba nimewakosea, basi tuhojiwe hata mbele za watu ili lifahamike na kuyamaliza kuliko hiki wanachofanya kwangu. “Kasababisha kila kona ninayopita nanyooshewa vidole kuwa niliwatosa. Ifike mahali haya mambo tuyaweke sawa kwa kuwa naumia sana, hawajui tu. Si kwamba, labda ni kwa kutaka msaada wao, hapana. Bali kila mtu awe ameitakasa nafsi yake na kuondokana na vinyongo.”
Baba huyo wa Diamond anasema hata mawasiliano na mzazi mwenzake ni pale anapojisikia. “Tena wakati mwingine na maneno ya karaha, lakini ana afadhali kuliko mtoto ambaye mara ya mwisho tuliwasiliana akiwa na Wema Sepetu ambaye alikuwa akija naye hapa mara kwa mara kunisalimia,” anasema.
Kwa sasa maisha si mazuri. Abdul anajihusisha na biashara ya viatu. Huchukua viatu kwa malikauli katika soko la Karume na kuvipeleka kwa wateja wake mahali walipo. “Lakini maisha kwa sasa si mazuri kwa kuwa nasumbuliwa na tatizo la miguu. Inanifanya wakati mwingine nishindwe kutembea muda mrefu,” anasema mzazi huyo.“Kama unavyoniona miguu inaniuma na wakati mwingine nashindwa kuinuka hata kitandani.
“Naona ni wakati sasa na mimi kuwa na eneo la kufanya biashara hii, lakini ndio hivyo uwezo, walau ningekuwa na gari ningeweza kuzunguka nalo hata kwa kuendeshwa ili nisiwapoteze wateja wangu, lakini sina namna.” Anasema hata uwezi wa kugharimia matibabu, hana. “Labda ningekuwa na bima ya afya ingekuwa msaada kwangu lakini ndio hivyo sina,” anasema.
Apata msaada mtandaoni
Hata hivyo, msaada wake mkubwa uko kwa mtoto wake wa hiari anayeishi London, Uingereza anayeitwa Zubeda. Walijuana na mtoto huyo katika mitandao ya kijamii baada ya kuona mahojiano yake akielezea maisha anayoishi.
Mwananchi sourceView attachment 968793
[emoji8][emoji8] [emoji8]Eeh
Kinyume
WaLimwengu hamna Jema...Msaada wa Diamond kwa baba yake HAUONEKANI kama unavyoonekana kwa mama yake..
Huyu mzee ni mpuuzi sana...[emoji16] [emoji16]
Yaani kila anapo taka kupaza sauti, ni lazima aongee na watu wa media...[emoji55] [emoji55]
Na mbaya zaidi ni kwamba anajiskaha kama hao wanao muhoji ni watafuta fursa. Yaani wanatumia jina la Diamond na kumuhoji baba yake, kisha wanaanika kwenye public ili wapate pesa....[emoji57] [emoji57]
Kwa Tanzania si ajabu Diamond anafata ushauri wa kishirikina.
Kuna dini moja yenyewe inasema JINO KWA JINO. Nadhani ndo kinachomtokea huyu dingiZa kikristu zinatupa haya mafundisho ya kusamehe saba mara sabini, SIJUI DINI ZINGINE
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Huku mtaani maisha magumu mpaka jamaa ananiuliza: “Hivi luku haina kifurushi cha chuo?
Hivi unajua taabu ya kulea mtoto pekee yako ww wakati baba yake yupo? Kama ni mwanae s ampe radhi tuone kama itakamata kama kweli hana makosa!Mzazi ni mzazi tu no matter what. Hatujui kipi hasa huyu mzee alimfanyia Diamond lakini kiubinadamu nafikiri imetosha sasa ameanza kulia siku nyingi sana mzee wa watu! Angemsamehe tu, amuwezeshe Hata kidogo then aendelee na mambo yake! Nafikiri Hata mama Diamond ni kikwazo kwa Diamond kumsamehe mzee Wake, akifikiria jinsi mama alivyopambana kwa ajili yake anashindwa kwenda kinyume na mama yake!
Anajua mwanae ana mpungambona baba yake dimpoz halalamiki kama huyu
lakini huyu diamond huwa anachukuaje passport uhamiaji bila cheti cha kuzaliwa cha baba yakeAnajua mwanae ana mpunga
Sema inaelekea aliwanyanyasa sana.....
Ova
Diamond waswazi tu nasema kamkatia mshua wake umeme na maji "Anajua mwanae ana mpunga
Sema inaelekea aliwanyanyasa sana.....
Ova
Anatumia cha mama tulakini huyu diamond huwa anachukuaje passport uhamiaji bila cheti cha kuzaliwa cha baba yake