Baba Diamond: Queen Doreen ni mnafiki, nikifa asisogelee jeneza langu

Baba Diamond: Queen Doreen ni mnafiki, nikifa asisogelee jeneza langu

Mimi nilimuelewa sana tatizo situation iliyopo na kutoa maneno hayo ndio inafanya watu wamfungukie huyo bi mdada.

Hizi kauli hua sio nzuri kabisa utashangaa yanarudi kwenye ukoo kuumbe bibi mzaa bibi aliwahi kuongea.
Baba kamwaga mboga kabisa
 
Wasalaam
Baada ya Queen Darleen kumfumua Baba Diamond, Baba yake mzazi huyo na yeye amemlipua Queen Darleen. Zari, Wema na Mama Diamond watajwa. .
Akizungumza na online TV moja, Queen Darleen alipoulizwa kuhusu Zari alisema ndie mwanamke pekee wa Diamond aliyeonyesha kumjali baba yao akiwataka wamalize tofauti zao
.
"Zari ni wifi mwenye roho nzuri na ndiye mtu pekee aliyekuwa anatushauri tumjali baba (mzee Abdul) japo baba mwenyewe kuumwa kwake amekuwa kama mtoto…Kwa kweli kwa sasa siwezi kusema baba yangu ni Abdul, baba yangu mimi ni Nasibu…” alisikika Queen mbeleni katika mazungumzo hayo.
.
Baba Diamond alipoulizwa na GPL kupitia Amani kuhusu kauli ya Queen Darleen alijibu kumtaka Queen Darleen asimjue tena Kama baba yake mzazi
.
“Asisogelee hata jeneza langu, yeye si amesema baba yake siyo mimi, baba yake ni Diamond basi sawa. Hata mimi simtambui. Nikiumwa, nikifanya chochote simhitaji,” alisema baba Diamond huku machozi yakimtoka
.
“Yani kabla hajawa na hilo jina, alikuwa anakuja hapa, anapika na tunakula pamoja leo hii kweli anasema mimi nina akili za kitoto, kwamba nikiumwa nakuwa sina akili? Lini mimi niliumwa nikawa kama mtoto au sina akili?, Diamond pamoja na ustaa wake wote hajawahi kuniambia maneno mazito kama hayo, hicho kiburi anakitoa wapi mtoto wa kike?”
.
"Yule mtoto mbaya sana, Yeye ndiye alikuwa anakuja hapa anasema ooh… sijui mama Diamond ndiye anayemsababishia Diamond agombane na Wema…ooh… sijui mara hivi kumbe mnafiki mkubwa, Binafsi hata mimi Zari namkubali maana natambua ana moyo wa huruma na akili kuliko huyu Queen.”
.
Uamuzi aliochukuwa kwa binti yake huyo wa kumzaa .
“Nimezichoma kabisa moto picha zake. Siwezi kuwa na mtoto halafu akanikana hadharani. Acha na mimi nimkane hadharani, hana maana. Asinisaidie kwa chochote, sihitaji msaada wake kwanza,” alisema baba Diamond Akizungumza na Globalpublishers
Shida ya familia za kimaskin zinapopata ahuen ya kimaisha n kudharauliana tu.
 
hahahaha baba anasema Zari ana roho nzuri kuliko queen doreen.....
Huyu Mzee mnafiki sana leo Zari kawa mzuri baada ya kusikia kwa Queen D. kwamba alikuwa mshauri mzuri hukusu yeye, mbona alisema anampenda na kumtambua Hamisa kama mkwe wake, tena akataka mwanae amuone Hamisa.
 
Wanaomshambulia huyu mzee ni manyang'au ya JF wasio na watoto. Yaani jinsi kumlea mtoto ulivyomgumu vile uhangaike naye mpaka awe mtu mzima, mara ukose usingizi kwa ajili yake, mara ukose hata nguo ya kuvaa kwa kumtunza halafu anakuwa mtu mzima na kijiumaarufu anasema wewe siyo baba yake na kwamba baba yake ni kaka yake. Hiyo kauli ya Quuen kwamba yeye anaweza akasema diamond ndiyo baba yake ni kauli ya kijinga na kudhalilisha diamond anaweza kuona uchi wa mama yeke?.
Aliyekurupuka nani kati ya sisi na wewe? Wewe kama ulitunzwa na baba na mama shukuru Mungu ila si kwa hii familia inayoongelewa hapa, kwa kukusaidia tu huyu Mzee umejitokeza baada ya kuona jina la mwanae Diamond (Nasib) linavuma na mama anakula matunda ya mwanae ndio wanahabari wakamchomolea wapi sijui na kumuombea msaada wa matibabu, ikishasoma hii utamjua nyang'au wa JF ni nani?
 
Wazazi huwa tunakosea sana tunaposhindwa kutimiza majukumu yetu kwa watoto wetu hata kwa kile kidogo tulichojaaliwa kupata

Kwa wale tuliosoma shule za bweni tutakumbuka baadhi ya maswahibu waliyokuwa wanatusumulia wenzetu waliotelekezwa na baba zao, huku wakiapa asilani kulipiza kisasi siku wakifanikiwa

Watoto wanaathirika sana kisaikolojia wanapotelekezwa na wazazi wao. Hiki ndicho kinachoitafuna hii familia ya mzee Abdul. Mimi na wewe tuliobahatika the hatika kushea kipande cha mkate, ugali chumvi na kufulia mapapai kama sabuni na baba zetu mpaka tukafikia umri wa kujitegemea, tutawashangaa sana hawa kizazi cha Abduli kumtelekeza baba yao. Tunasahau kabisa kwamba ni mzee Abduli mwenyewe aliwaumbia huu mtazamo wangali wadogo

Tusijikite katika kuhukumu. Tujifunze kwa hawa waliotutangulia kuliona jua, kisha tuchukue hatua madhubuti
 
Hii familia ingepewa kipindi reality show with Abdul Naseeb family tkajionea drama na wao walipwe mpunga wao

Hahaha na kweli kama cha Kardashian full vituko ,ngoja wakina Tiffa nao wakue waongeze chachandu ya vituko vya familia
 
Hahaha na kweli kama cha Kardashian full vituko ,ngoja wakina Tiffa nao wakue waongeze chachandu ya vituko vya familia
Wale mama yao anawalea na class flan huu Utandale utawapita kidogo
 
Mimi nazani Huyu dada amesema baba Yake ni Nasibu kwa kuwa ndiye anaeweza kumsaidia mara apatapo shida!
Tena angeweza Hata kusema kuwa Nasibu ndiye baba Yake na ndiye mama Yake zaidi angeweza kusema ndiye Mume wake pia!
Ni kawaida watu huwa wanasema hivyo kuonesha ni namna gani ya uzito wa kumtegemea Mtu !
Na hakumanisha dharau kwa baba Yake mzazi!
Wazee wengine sijui kwa nini hawaishagi kuwa na nongwa?!
Wanapenda kuangukiwa na kuombwa misamaha Kama wao ni miungu!
Fainali uzeeni!
Wazee wengine noma sana aisee ?!
 
Back
Top Bottom