Baba Diamond: Queen Doreen ni mnafiki, nikifa asisogelee jeneza langu

Baba Diamond: Queen Doreen ni mnafiki, nikifa asisogelee jeneza langu

Wasalaam
Baada ya Queen Darleen kumfumua Baba Diamond, Baba yake mzazi huyo na yeye amemlipua Queen Darleen. Zari, Wema na Mama Diamond watajwa. .
Akizungumza na online TV moja, Queen Darleen alipoulizwa kuhusu Zari alisema ndie mwanamke pekee wa Diamond aliyeonyesha kumjali baba yao akiwataka wamalize tofauti zao
.
"Zari ni wifi mwenye roho nzuri na ndiye mtu pekee aliyekuwa anatushauri tumjali baba (mzee Abdul) japo baba mwenyewe kuumwa kwake amekuwa kama mtoto…Kwa kweli kwa sasa siwezi kusema baba yangu ni Abdul, baba yangu mimi ni Nasibu…” alisikika Queen mbeleni katika mazungumzo hayo.
.
Baba Diamond alipoulizwa na GPL kupitia Amani kuhusu kauli ya Queen Darleen alijibu kumtaka Queen Darleen asimjue tena Kama baba yake mzazi
.
“Asisogelee hata jeneza langu, yeye si amesema baba yake siyo mimi, baba yake ni Diamond basi sawa. Hata mimi simtambui. Nikiumwa, nikifanya chochote simhitaji,” alisema baba Diamond huku machozi yakimtoka
.
“Yani kabla hajawa na hilo jina, alikuwa anakuja hapa, anapika na tunakula pamoja leo hii kweli anasema mimi nina akili za kitoto, kwamba nikiumwa nakuwa sina akili? Lini mimi niliumwa nikawa kama mtoto au sina akili?, Diamond pamoja na ustaa wake wote hajawahi kuniambia maneno mazito kama hayo, hicho kiburi anakitoa wapi mtoto wa kike?”
.
"Yule mtoto mbaya sana, Yeye ndiye alikuwa anakuja hapa anasema ooh… sijui mama Diamond ndiye anayemsababishia Diamond agombane na Wema…ooh… sijui mara hivi kumbe mnafiki mkubwa, Binafsi hata mimi Zari namkubali maana natambua ana moyo wa huruma na akili kuliko huyu Queen.”
.
Uamuzi aliochukuwa kwa binti yake huyo wa kumzaa .
“Nimezichoma kabisa moto picha zake. Siwezi kuwa na mtoto halafu akanikana hadharani. Acha na mimi nimkane hadharani, hana maana. Asinisaidie kwa chochote, sihitaji msaada wake kwanza,” alisema baba Diamond Akizungumza na Globalpublishers
Mzee nae Ana shida Sana huyu.. Asiposogelea hilo kaburi atapungukiwa nini?
 
Tatizo la watoto wa kike huwa hawanaga akiri, wanafikiria kupitia midomo. Kwani kuliluwa na sababu yoyote ya kueleza changamoto wanazokutana nazo toka kwa baba yao. Ameanza kuishi kwa kakaake akiwa mkubwa tu af aseme domo ndo babaake, linaacha kuolewa linazeekea kwa bro wake. Kaongea hvyo ili aendelee kulelewa na kakaake au kakaake aone anampenda, but wanawake ni viumbe wanafiki sn Diamond asiamini maneno ya huyo msichana, hao ndo wanakuja kunyanyasa watoto km kaka umefariki. Diamond mwenyewe sio km hakutani na changamoto za familia yake yote akiwemo yeye mwenyewe Queen lkn anajua ndo familia hiyo.
 
Sifa ya baba ni kulala na mama yako wewe ukazaliwa, period. pampas haihusiki ktk uzazi. Kama queen Dorleen kaelezwa na mama yake kuwa Diamond alifanya mambo kwa mama yake ruksa .
 
Lakini haiwezi kubadilisha kuwa huyo ni baba yako mzazi nafikiri cha msingi ni kusamehe....
Kumsamehe sio lazima nishiriki yanayomuhusu, raha zake ale kwa nafasi yake na shida zake kwa nafasi yake tusitambuane. Mind you sina time ya kumvunjia heshima zaidi zaidi ntamuacha ajilize mtandaoni bila kumjibu na sitotaka mwandishi ajitie kuniuliza chochote.
 
Huyu Mzee kaharibu sasa hapo alivyopaniki.

Unapewa umbea na Watu baki na wewe unaanza kubwata papo hapo, angetulia na kujibu kwa busara.

Vipi kama angetabasamu tu na kusema "ni utoto tu unamsumbua Mwanangu yule, akitulia na kutafakari aliyosema atajirekebisha"

Ila hao GPL nao ni wachonganishi tu, wanachojali wao ni kuuza news hata kama huku nyuma nyie mtasambaratika.
 
Kutembea nje kusaidie kujifunza ustaarabu pia
 
Darleen kakosea sababu diamond ana pesa ndio umkane Baba yako ebu wakae chini wamalize tofauti zao
 
Kumsamehe sio lazima nishiriki yanayomuhusu, raha zake ale kwa nafasi yake na shida zake kwa nafasi yake tusitambuane. Mind you sina time ya kumvunjia heshima zaidi zaidi ntamuacha ajilize mtandaoni bila kumjibu na sitotaka mwandishi ajitie kuniuliza chochote.
kuwa makini atachana picha zako zote hahahahah
 
kuwa makini atachana picha zako zote hahahahah
Hahahaha maisha sio complicated, wazee kama hawa huhitaji kutumia nguvu ni kumpuuza tu. Hata akikutafuta jibu ni rahisi "sina kinyongo na wewe endelea tu kutoexist na blocks za kila sehemu juu" na ukiendelea kunifata fata ntaomba court order ya kukuzuia kunikaribia kwa namna yeyote ile.
 
Back
Top Bottom