Hivi alipomtelekeza wakati huo akiwa mtoto, je angekufa kwa kukosa huduma au angekuwa teja au mvuta bangi hiyo risala leo hii angemtolea nani?
Siungi mkono hoja acha baba avune alichopanda iwe funzo kwa wababa wengine sharo baro kama yeye.
mi na wewe hatujui sababu za kutengana kwao, pengine walipotezana kila mmoja hajui mahali alipo mwenzie baada ya kutengana na walipotafutana wakashindwa kujuana mahali kila mmoja alipo??? ingekua mama ndo kamtelekeza mwanae af akalelewa na baba, ungesema ayo maneno??
Kweli aunt Yaani inapain. wenginetumewajua baba. baadayakifaulu kwenda chuo. ndio. anajuakunamtoto. Utafanyaje LEOHII.ndio wanatutegemea. achatu hilosio. m mzee wangu after mom death anakwambia. unajuamamayako. angenisamehe. asingekufa...wakati mamalishamwambia hanashidanae. ilakwake. atolala ajekusalimiawatoto LEOHII anacancer.kilaanaekaona akienda asbh oceanroad natumagari na anarudishwa napaykilakitu huondio upendowa agape. Hasatukijua tunapita. aaunt
So sad! Kuelekea Zari show. Baba yake Diamond ambae anaumwa sana miguu ameshindwa hata kutembea ameomba mwanae amsamehe kama baba na pia ameomba aje kumtembelea ampeleke hospitali asisubiri kufa.
Sisemi kwa ubaya, mi ni mmoja kati ya watu wanaojua maisha ya baba na mama waliotengena. Ukweli haijalishi uko level gani ugomvi wa mama yako na baba yako usiingilie hata siku moja tafadhalini...
Narudia tena, Diamond akifa leo baba yako hutopata Baba wa kukodi.
Kila la kheri..
==============
DIAMOND MWANANGU USISUBIRI NIFE!
Maskini! Wakati leo akiangusha pati ya nguvu na mpenzi wake, Zarinah Hassan Zari The Boss Lady inayokwenda kwa jina la Zari All White Party kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar, baba mzazi wa mwanamuziki Nasibu Abdul Diamond Platnumz, Abdul Jumaa yu hoi kitandani huku akimtaka mwanaye huyo kuonesha msamaha wa kweli aliotangaza kwenye vyombo vya habari na kwamba asisubiri hadi afe.
View attachment 248376
Baba mzazi wa Diamond Platnumz
TUJIUNGE NA CHANZO
Habari kutoka kwa chanzo makini kilicho karibu na baba Diamond kilidai kwamba kutokana na hali tete ya mzazi huyo ambapo kwa sasa anasumbuliwa na miguu kwa mara nyingine huku ikitoka magamba na kushindwa kutembea kwa muda mrefu, amekuwa akimlaumu mwanaye huyo kupita kiasi.
Chanzo hicho kilisema kuwa mzazi huyo amekuwa akisema kama alimkosea Diamond, alishamuomba msamaha na akasema amemsamehe lakini hakuonesha mabadiliko yoyote kwake wakati alikiri hadharani kupitia vyombo vya habari.
Kiliendelea kueleza kwamba kutokana na jambo hilo baba Diamond amekuwa akiumia kwani mwanaye huyo baada ya kutangaza amemsamehe hajaonesha mabadiliko yoyote ya kumjali.
MALALAMIKO
Chanzo hicho kilidai kwamba, baba Diamond amekuwa akilalamika kuwa ameugua kwa muda mrefu lakini Diamond hajawahi kwenda kumjulia hali hata siku moja.
Ukweli baba Diamond anaumia sana. Sasa hivi anaumwa, ameshindwa hata kutoka nje, miguu imevimba na ina muonekano wa ajabu, amekuwa akisema hajui ni kwa nini mwanaye anashindwa kulegeza moyo wake na kumsamehe wakati alishakiri kwenye vyombo vya habari.Anasema bora akaenda sasa hivi wakasameheane kuliko asubiri hadi siku akifa ndipo aende, kiliongeza chanzo hicho.
BOFYA HAPA KUMSIKIA BABA DIAMOND
Baada ya kupata habari hizo, gazeti hili lilitinga nyumbani kwa baba Diamond au Dangote maeneo ya Magomeni-Kagera, Dar na kumkuta akiwa katika hali mbaya kwani miguu imevimba huku ikiwa imepoteza muonekano wa kawaida na kuwa na ngozi ya ajabu.
Baada ya salamu, wanahabari wetu walimuuliza kulikoni yupo katika hali hiyo na kama Diamond alikuwa amekwenda kumjulia hali ambapo alikuwa na haya ya kusema:Ukweli nimeugua kwa muda mrefu lakini mwanangu Diamond hajawahi kuja kuniona.
AMTUMIA MESEJI
Hali hiyo ilinifanya juzikati kumwandikia meseji ya kukata tamaa na kumwambia kwamba anaona ameshanizika kutokana na kunisahau kwake lakini Diamond hakunijibu.
Namshukuru Mungu kwa sababu nina kibanda changu cha kulala, silipi kodi kuna watu walishanishauri eti niwatume watu wakaongee naye lakini nilikataa kwa sababu haoni thamani yangu.
ANASUBIRI NIFE?
Kama ni tofauti na mama yake (Sanura Kassim), tulishamaliza na kabla hajaugua alikuwa anakuja kuniona, nikimuuliza kuhusu Diamond alikuwa akiniambia alishaongea naye lakini kila siku alikuwa akisema atakuja tu kuniona mpaka leo sijamuona labda anasubiri hadi nife ndiyo aje.
Mara ya mwisho kumuona ilikuwa ni kipindi kile alivyomvisha pete ya uchumba Wema Sepetu ndiyo alimleta kwangu kumtambulisha, tangu hapo huwa namsikia tu kwenye vyombo vya habari. Inauma sana; Yote kwa yote haya ni maisha tu.
DIAMOND YUPO BIZE
Ijumaa lilimtafuta Diamond ili kumfikishia habari juu ya baba yake ambapo hakupatikana hewani lakini watu wake wakaribu (Wasafi Classic Baby) walidai kwamba bosi wao huyo alikuwa yupo bize na Zari kwa ajili ya pati yao leo.
Chanzo: GPL
Kama aliweza kumpa gari mtu asiye ndugu yake!
Anapaswa kumsaidia babaye!
Na hata kama Huyo si babaye,kesha mwomba msaada,KAMA ANA TAARIFA HIZO amsaidie.
Si wanasemaga wao ni vioo!
Yote kwa yote huwezi kujua mambo ya ndani waliofanyiana, lakini wakati mwingine Mungu anakupa majaribu ili uyashinde.
Pengine bila baba yake kumtelekeze Diamond asingekuwa hapa alipo, hayo ni makusudi ya Mungu.
Kwa kumrudishia fadhila Mungu ni vema akamsaidia huyo baba yake kama anavyowasaidia watu wengine wasio mhusu.
Mungu hana visasi anapenda kusamehe.
Pamoja na hayo,hv huyo baba hana watoto wengine?
Huyu baba anatafuta huruma aiseeee kipindi anamuacha alikua wapiii asituharibie siku ye aumwe ajiuguze tu kwani alimzaa daimond peke yake kelebu wahed😰😰😰😰😰😰😰😰😰😰
Kha!! .....huu mwandiko,unatumia citizen calculator???
Kha!! .....huu mwandiko,unatumia citizen calculator???