Baba Diamond: Usisubiri nife mwanangu, nipeleke Hospitali

Baba Diamond: Usisubiri nife mwanangu, nipeleke Hospitali

Family matters should be solved by family kind and not through media. Mwachen jamaa amalize party yake vyema kukanwa na baba yako ni sawa na mtoto yatima ingekuwa kwa wenzetu huyo mzee angekuwa jela anatumikia kifungo
 
Ngoja aanze kutembea uchi tu karibuni ataanza,baba anaumwa we unaendekufanya anasa na mwanamke wa uzinifu tu,nakusihi diamond msikilize baba yako.

Mungu angekuwa Athumani kweli ange tembea uchi!
 
Muache afe ili iwe fundisho mxiuuu!! ,Baba na mama wanaweza kukukana ila Mungu hawezi kabisa kukukana, yeye ndiye aliyekuimba, sasa kama aliikana damu yake anategemea nini mxiuuu
 
Hawa baba wakati mwingine ni watu kusamehe tu. ila makosa wanayo. Akikuacha anazira na watoto. Ngoja iwe fundisho na kwa wengine.

Unahangaika na watoto weeee. Lleo yuko chuo ndo wa kwanza kumtafutia field.

Wanaume kosana na mke ila hii ya kusema na watoto wako chukua acheni. Sikio tu ndilo halikui. Watoto wanakua.
 
Ni ngumu sana kusamehe hali fulani, ila mtu mzima akikufata akakuomba msamaha tena muafrica wasioomba msamaha wadogo kwao , na unaemuita baba yako, have a heart a forgive. Ndivyo mungu apendavyo na aliagiza samehe mara saba sabini. Utapata thawabu mbinguni
 
Ukifanya fujo...umeambiwa usifanye hiki ww unakuwa jeuri unakaidi hutaki utapigwa tu,na mm nasema wapigwe tu.
 
Mwacheni huyu kijana. Hamjui maumivu aliyokuwa nayo moyoni kuhusu maisha aliyoishi na baba yake. Upendo hutengenezwa hauji kama uyoga. Alichofanya D. Ni kumsamehe lakini hajasahau. Lazima mtofautishe hapo. Niliwahi msikia akiongea juu ya hilo swala ktk. Kipindi kimoja kuwa aliwahi kwenda na mm yake kumuona huyo baba akiwa anaumwa lkn. Bibi yake mzaa baba aliwafukuza kwa kudai wao ndio wanamroga mwanae. Sasa afanyeje. Sasa hivi nae ana muuguza mama yake ambaye kwake nafikiri kama kuchagua ameona ni muhimu kuliko baba. Nafikiri tuliache hilo kama lilivyo ni la kifamilia zaidi. Sisi wengine tumelikuta tu hatujui hata lilianzia wapi. Pole sana D. Kwa kweli una mtihani
So sad! Kuelekea Zari show. Baba yake Diamond ambae anaumwa sana miguu ameshindwa hata kutembea ameomba mwanaeamsamehe kama baba na pia ameomba aje kumtembelea ampeleke hospitali asisubiri kufa.

Sisemi kwa ubaya, mi ni mmoja kati ya watu wanaojua maisha ya baba na mama waliotengena. Ukweli haijalishi uko level gani ugomvi wa mama yako na baba yako usiingilie hata siku moja tafadhalini...

Narudia tena, Diamond akifa leo baba yako hutopata Baba wa kukodi.

Kila la kheri..

==============

DIAMOND MWANANGU USISUBIRI NIFE!


Maskini! Wakati leo akiangusha pati ya nguvu na mpenzi wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ inayokwenda kwa jina la Zari All White Party kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar, baba mzazi wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Abdul Jumaa yu hoi kitandani huku akimtaka mwanaye huyo kuonesha msamaha wa kweli aliotangaza kwenye vyombo vya habari na kwamba asisubiri hadi afe.


View attachment 248376
Baba mzazi wa ‘Diamond Platnumz’


TUJIUNGE NA CHANZO
Habari kutoka kwa chanzo makini kilicho karibu na baba Diamond kilidai kwamba kutokana na hali tete ya mzazi huyo ambapo kwa sasa anasumbuliwa na miguu kwa mara nyingine huku ikitoka magamba na kushindwa kutembea kwa muda mrefu, amekuwa akimlaumu mwanaye huyo kupita kiasi.


Chanzo hicho kilisema kuwa mzazi huyo amekuwa akisema kama alimkosea Diamond, alishamuomba msamaha na akasema amemsamehe lakini hakuonesha mabadiliko yoyote kwake wakati alikiri hadharani kupitia vyombo vya habari.

Kiliendelea kueleza kwamba kutokana na jambo hilo baba Diamond amekuwa akiumia kwani mwanaye huyo baada ya kutangaza amemsamehe hajaonesha mabadiliko yoyote ya kumjali.


MALALAMIKO
Chanzo hicho kilidai kwamba, baba Diamond amekuwa akilalamika kuwa ameugua kwa muda mrefu lakini Diamond hajawahi kwenda kumjulia hali hata siku moja.

“Ukweli baba Diamond anaumia sana. Sasa hivi anaumwa, ameshindwa hata kutoka nje, miguu imevimba na ina muonekano wa ajabu, amekuwa akisema hajui ni kwa nini mwanaye anashindwa kulegeza moyo wake na kumsamehe wakati alishakiri kwenye vyombo vya habari.“Anasema bora akaenda sasa hivi wakasameheane kuliko asubiri hadi siku akifa ndipo aende,” kiliongeza chanzo hicho.


BOFYA HAPA KUMSIKIA BABA DIAMOND
Baada ya kupata habari hizo, gazeti hili lilitinga nyumbani kwa baba Diamond au Dangote maeneo ya Magomeni-Kagera, Dar na kumkuta akiwa katika hali mbaya kwani miguu imevimba huku ikiwa imepoteza muonekano wa kawaida na kuwa na ngozi ya ajabu.

Baada ya salamu, wanahabari wetu walimuuliza kulikoni yupo katika hali hiyo na kama Diamond alikuwa amekwenda kumjulia hali ambapo alikuwa na haya ya kusema:“Ukweli nimeugua kwa muda mrefu lakini mwanangu Diamond hajawahi kuja kuniona.

AMTUMIA MESEJI
“Hali hiyo ilinifanya juzikati kumwandikia meseji ya kukata tamaa na kumwambia kwamba anaona ameshanizika kutokana na kunisahau kwake lakini Diamond hakunijibu.

“Namshukuru Mungu kwa sababu nina kibanda changu cha kulala, silipi kodi kuna watu walishanishauri eti niwatume watu wakaongee naye lakini nilikataa kwa sababu haoni thamani yangu.


ANASUBIRI NIFE?
“Kama ni tofauti na mama yake (Sanura Kassim), tulishamaliza na kabla hajaugua alikuwa anakuja kuniona, nikimuuliza kuhusu Diamond alikuwa akiniambia alishaongea naye lakini kila siku alikuwa akisema atakuja tu kuniona mpaka leo sijamuona labda anasubiri hadi nife ndiyo aje.

“Mara ya mwisho kumuona ilikuwa ni kipindi kile alivyomvisha pete ya uchumba Wema Sepetu ndiyo alimleta kwangu kumtambulisha, tangu hapo huwa namsikia tu kwenye vyombo vya habari. Inauma sana; “Yote kwa yote haya ni maisha tu.”

DIAMOND YUPO BIZE
Ijumaa lilimtafuta Diamond ili kumfikishia habari juu ya baba yake ambapo hakupatikana hewani lakini watu wake wakaribu (Wasafi Classic Baby) walidai kwamba bosi wao huyo alikuwa yupo bize na Zari kwa ajili ya pati yao leo.

Chanzo: GPL
 
Leo naona. pichazake anahesabu Dollar kunamanufa!gan babayako hoi unahela makalioni aijalishi alikutendeanini. wapo waliokanwanababazao. leo. wanasimama kamakaka wWATOTO tufanyesehemu yamaishayetu jua. kuna. mbingu baadayahapo

Pdidy ktk ubora wako
 
Niwe open kabisa ningelikuwa Nasib Abdul hakyamungu baba huyu nisengeli msaidia hata kiduchi wacha mungu anihukumu

Mkuu tena ningelikuwa mimi ningekuwa naenda kutembelea jirani za huyu baba na kuwapa misaada lakini kwake nisingeonekana!
 
Aijalishi lakipesa. nimerudiatena usiguseugomvi wawazazi waje...kamauamini. angalia. mkeulienae nini. mbali. muulize machungu yawanawake. Aliopata DIAMOND. kufikia. hapo. utajua siriyawazazi HUMONDANI

Kirohosafi DIAMOND. msaidiebabayako. India ufahamu. Weka baraka zawatotowako

Yani amtelekeze kabisa asimsaidie dogo a hustle, eti apate mafanikio ndiyo aanze kumtambua kama mwanae then aanze kuleta lawama.
Hivi angekuwa bado maskini anemtambua kuwa diamond ni mwanae?
Eti ugomvi wa wazazi asiungilie, huo ugomvi baba mpaka akamtelekeza ina maana umemuathiri yeye pia sasa iweje isimuume.
Mzee asilalamike kusaidiwa au kutosaidiwa na mwanae imebaki utashi sio wajibu maana huyo sio baba yake alipanda mbegu hakulea jambo ambalo ni rahisi.
Ukipanda ukakosa palilia na kujali shamba usitegemee mavuno
 
Leo naona. pichazake anahesabu Dollar kunamanufa!gan babayako hoi unahela makalioni aijalishi alikutendeanini. wapo waliokanwanababazao. leo. wanasimama kamakaka wWATOTO tufanyesehemu yamaishayetu jua. kuna. mbingu baadayahapo

Kama na wewe ulikataliwa na baba yako badae ukamsamehe pole!!hakuna haja ya kulea wapuuzi wa aina hiyo mkuu!!nawaita wapuuzi tu wanaokataa watoto wao!
 
Baba aliweza kupanda mbegu kisha akakausha huyo sio baba ni mvulana, mtu mwenye busara uhakikisha anatoa huduma au hata kumwona mwanae haijalishi kuna ugomvi kiasi gani baina yake na mwenzie. naomba diamond amache tu yeye aangalie maisha ya aliyemwangaikia.

SI ndio wanajisifu wavulana kuwa hata nikimtelekeza mtoto akikua atanitafuta sasa wajue dunia imebadilika watoto wa siku hizi wanajitambua, yeye afe tu.

Wewe ni bandidu! Sio mchezo mama!
 
Wazee wengi wana tabia ya kuzingua mwanzoni thenly mwisho kijana akifanikiwa ndio wanarudi, ipo mifano mingi kama baba Kanumba, baba kigwangala, baba zitto na huyu baba Diamond, dawa ya watu wenye tabia kama hizi ni kuwakazia tu ili liwe fundisho.
 
Hawa baba wakati mwingine ni watu kusamehe tu. ila makosa wanayo. Akikuacha anazira na watoto. Ngoja iwe fundisho na kwa wengine.

Unahangaika na watoto weeee. Lleo yuko chuo ndo wa kwanza kumtafutia field.

Wanaume kosana na mke ila hii ya kusema na watoto wako chukua acheni. Sikio tu ndilo halikui. Watoto wanakua.

Kweli aunt Yaani inapain. wenginetumewajua baba. baadayakifaulu kwenda chuo. ndio. anajuakunamtoto. Utafanyaje LEOHII.ndio wanatutegemea. achatu hilosio. m mzee wangu after mom death anakwambia. unajuamamayako. angenisamehe. asingekufa...wakati mamalishamwambia hanashidanae. ilakwake. atolala ajekusalimiawatoto LEOHII anacancer.kilaanaekaona akienda asbh oceanroad natumagari na anarudishwa napaykilakitu huondio upendowa agape. Hasatukijua tunapita. aaunt
 
Back
Top Bottom