kwa hiyo analipiza kisasi?du jamani binadamu hatari kwa nini asimsamehe ili nae aje asamehewe hapo mbele ya safari,wengi tuliachwa na baba zetu kwa sababu moja au nyingine na siyo lazima kujua kwa nini baba yako alipotea,tunasubiri akianza kupukutika na kurudi mitaani kama kawaida ya wasanii wa bongo ndiyo tutaongea sana
Hakika uko sahihi vitu vingine katika maisha ya wanadamu utokea kwa sababu!!!!Na ili la Nasib aka Diamond/Platnumz ni matokeo ya mambo yanayotokea Mungu akiwa na makusuido uenda si kwa Baba ya Diamond bali kwa Diamond mwenyewe...
Ebu itizame hii uenda mtafaruku wa Baba na Mama yake ulipoingia kwa namna ambayo wazazi hao wanajua mtoto akasimama kwa Mama..ila siri ya yote hayo wenye majibu ni wao wawili.Lakini kama mtoto unapokuwa na kupata ufahamu basi kwa kujua umuhimu wa Baba na Mama [Spirtually] unapaswa kuwa nguzo ya kuwafanya kila linapokuja jambo linalokuhusu wewe basi uungana japo mara moja na kumshukuru Mungu kwa wewe kuwepo Duniani...na kwa maajabu yake hawakujua kuwa LEO hii kupitia damu walizochanya wao kwa kiumbe Diamond basi amekuwa mtu maalufu Tanzania kwenye sekta ya burudani [Entertainment].
Nani anae leta fikra za Wazazi hawa kuungana pale lipokuja swala la shughuri yoyote ya Diamond..Ni Diamond mwenyewe kwa kuhakikisha anaishi vizuri na sehemu zote mbili [Zisizo ishi pamoja kama familia moja].Yani ndio kusema anajitahidi kumpa Mama matunzo mazuri kwa kadri anavyoona inafaha kwa kuwa amekuwa kipenzi chake muda wote, lakini pia kuwajibika kumuudumia Baba kwa mambo ya msingi na kuhakikisha uwanaume wa Baba kuzaa kidume anaitwa Diamond unasikika Nchi nzima,na kwa wanaume huo ndio ugonjwa yani SIFA HESHIMA....Japo baba uenda hakuwajibika kimalezi lakini kama binadamu mwenye ufahamu ni fursa ya kumuonyesha kuwa alikosea [To Prove HIM wrong] kuwa Mungu alikusudia Diamond awe kitu bora kilichowai kukaa kwenye kiuno cha Baba yake.Kadri alivyopasa kuwa karibu na Baba yake na kumuhudumia ndio BABA ya Diamond angezidi KUMTUKUZA MUNGU WAKE kuwa alifanya makosa na anatubu kwa dhati kwa yeye kutokuwajibika lasmi kwa Mwanae huyo ambae leo ni mtu maalufu Nchini na amefanikiwa kimapato.
Sasa kitendo cha yeye kumkimbia Mzee wake kwa excuse ya kuwa AKUMLEA ni UPOFU and SOON AND VERY SOON -kwa Wakristu tunasema kuna sheria kumi za MUNGU. Na moja inasema WAHESHIMU BABA NA MAMA YAKO UPATE HERI NA MIAKA MINGI DUNIA.
Sasa uenda tunafikiria MUNGU alikuwa na makusudi na Baba ya Diamond na leo hii analipwa kwa kumtelekeza Diamond wakati hatujui nini hasa kilitokea kati ya Mama Diamond na Baba yake Diamond.Lakini pia uenda MUNGU alikuwa na sababu ya kuwa atamkuza Diamond aje kuwa mtu maalufu kiumbe mwenye moyo wa KUSAMEHE na kumfanya MUNGU ajisifie kupitia Diamond kuwa aliweza kulelewa na Mama yake lakini alimsamehe Baba yake na kwa kuwa ni alama ya Taifa [Nationa Icon] AKAIBUA MWAMKO WA MAMILIONI YA VIJANA WA KITANZANIA KUWA NA MOYO WA KUSAMEHE WAZAZI WAO AMBAO WALIWATENDA WATOTO AMBAO HAWAKUWA NA SAUTIYA KUONGEA NA KUWASIKIA ZAMA HIZO.
Kwa MSAMAHA WA DIAMOND kumchukua Baba yake na kumpa matibabu yanayostahiki na kumuhudumia kwa mahitaji yake ya kimsingi na kumfanya sehemu ya familia yake muhimu basi MUNGU angekuwa amekubalika moyoni mwa Diamond na hivyo kwa ishara hiyo Taifa pia likapata vijana wenye kujifunza kusamehe-[Mfano tungeweza siku za usoni kusikia misemo toka kwa vijana kama ''x-fododo ameshindwa kumsamehe Mama yake, Diamond aliweza kumsamehe na kumkumbatia Baba yake sembuse yeye!!].
Hayo yote ni KIPIMO cha jinsi gani HATUKO DUNIANI kimakosa tuko hapa kwa sababu!!!na uenda sababu ya Diamond sio huo Usuperstar ..uenda MUNGU anaongea na Watanzania kupitia Diamond na Baba yake ambao kwetu ni kama wako kila mtaa au ni majirani zetu mtaani.
Kwa jinsi ya uzoefu wa kuona maisha tunayopita na misemo ya wahenga kama What goes around Comes around, Sikio halizidi kichwa, hakuna malefu yasiyo na ncha, usitukane mkunga na uzazi ungalipo...Diamond anaweza kumuona Baba yake is nothing kwake lakini SPIRITUAL BABA YA DIAMOND ni mkubwa zaidi ya umaalufu huu tunaomshabikia nao hapa.Kwa dini yake amtafute Sheikh Mkuu Mzee Simba [mzee mmoja muungwana sana toka viunga vya Majengo Shinyanga], amwambie Mzigo aliona dhidi ya Baba yake basi kupitia IMANI yao atamuongoza jinsi kusimama na wao kuendelea na maisha kama familia moja japo kunautengano yeye akiendelea kuwapa raha Watanzania na nyimbo zake za mapenzi.
Akiendelea kumwegamia Mama na kusikiliza mawazo ya Mama wakati kupitia mahusiano ya wanakidada kadha wa kadha kama Hawa, Wema, Penny, Jokate na leo Zari basi kidogo amepata kujifunza tabia za mamazetu pia sasa ni fursa nae pia akamsikiliza baba na kuvaa viatu vyake ata kama yeye alikuwa na makosa asamehe na kusahau ili apate KIBALI CHA MUNGU.
Kama TAIFA yashatusibu kwa Kipenzi cha Watanzania upande wa sinema za Kitanzania R.I.P The Great One...Sura hii ya Diamond haina tofauti kwa asilimia kubwa na picha hii ya The Great....Watanzania waliongea mengi lakini mazingira haya hayatokei hivi hivi kama watu hawajui IMANI ni nini, basi ni mwanzo mwema wa kujifunza na kufahamu misemo muhimu ya kiimani kama huu wa ''WATU WANGU WANA ANGAMIA KWA KUKOSA MAALIFA''.
Baada ya Show ya Zari All White Party Usiku wa Leo basi kuepusha sauti ya Baba isiongelee tumboni na umma wa Wanaume wa Tanzania wakagumia nae tumboni basi YASULUHISHWE NA AMPE HUDUMA BABA YAKE.Manake Wanaume watu wazima wanasema mheshimu Mama yako kwa kuwa kakuzaa wewe lakini na yeye Mama yako ni Mwanamke kwa Wanaume wengine...kauli hiyo ya Wanaume watu wazima ndio kusema wanasema WEMA SEPETU, PENNY AU JOKATE nao siku za usoni zisizo na jina watakuwa Mama za Watu.
VINGINEVYO ......VINGINEVYO.......VINGINEVYO...KUENDELEA KUISHI HIVYO UNAVYO ISHI NA BABA YAKO..mmmh haya tusiseme sana watu wazima wa Kiafrika usema TEMEA MATE CHINI....!!!