Baba Diamond: Usisubiri nife mwanangu, nipeleke Hospitali

Baba Diamond: Usisubiri nife mwanangu, nipeleke Hospitali

Mimi nauliza swali nataka jawabu.
Mwanamke anakuwa na mume usiku wanafanya mambo ya baba na mama.
Baada ya wiki mbili mama anamwambia baba nina mimba..baba anatika nduki huku mapovu yakimtoka oooh hio sio yangu.
Haonekani tena.
Anampoteza kabisa mwamamke.
Mwana mke analea mimba
Anazaa
Analea mtoto
Ana msomesha kwa tabu
Baba hana habari wala mtoto hamjui
Mtoto anafanya yake
Anafanukiwa anatengeneza fedha
Ati Ndio li baba linakuja ooh mie baba ako...bulshit....
Suala kuwa baba ni kutia kumwaga sperm tu ndio una qualify kuitwa baba ?
Jee huyo ni baba au mtia mimba tu ?
Baba asie kuwa na wajibu sio baba na hastahili kuitwa baba.

Kutia mimba sada hivi unaweza kuwekwa kwenye maabara unawekwa sperm na unapata mimba...sasa yule mwenye sperm zake atakuja baadae aseme mie ni baba ako nisaidie ?
Mababa mna wajibu wa kulea watoto wenu.
Unapo fanya kama hivi wewe sio baba ni dada umekimbia wajibu wako kuwa baba
Fact kabsa samani ya baba ni nini? Acha ajifunze kwa makosa aliyofanya
 
Yote kwa yote huwezi kujua mambo ya ndani waliofanyiana, lakini wakati mwingine Mungu anakupa majaribu ili uyashinde.

Pengine bila baba yake kumtelekeze Diamond asingekuwa hapa alipo, hayo ni makusudi ya Mungu.

Kwa kumrudishia fadhila Mungu ni vema akamsaidia huyo baba yake kama anavyowasaidia watu wengine wasio mhusu.

Mungu hana visasi anapenda kusamehe.
 
Wakati huyu mzee ana pesa ndefu ikawa Diamond akimfata magomeni kumsalimia tu alimfukuza akimwita chokoraa, akuwai kujua anakula nini wala anapona na nini akiugua. Leo unatafuta huruma kwenye media, malipo siku hizi ni hapa hapa duniani.
Watoto ulioona wa maana wako wapi? Diamond angeishia kwenye drugs kama wenzake wa Tandale ungemkumbuka? Mi naomba usife mapema ili uendeleee kukiona cha moto.

Hah hah na kwel asife haraka ili aendelee kuona mafanikio ya mtoto jina..kwan akifa ana faida gan maana hakuna msaada wowote wa yy kama baba ni sawa tu na MTU wa kawaida tuache kutetea uwovu
 
Kuomba msamaha anamuomba kwenye media…!!??? yeye alimkosea kwa kupitia media? Atafute wazee wamuitie mwanawe waombane msamaha sio kupitia media banah

Mkuu umenena maneno ya hekima na hivyo ndivyo inavyopaswa kuwa....Nikiangalia Source ya habari hii na timing, naona kuna zaidi.....Naona Fitna tu! Hapa ni kupakana matope na kuuza magazeti!!!! Huyu Baba yake Diamond atumie hekima asije akawa anatumiwa na wapinzani wa Kibiashara wa Diamond kumpaka matope Diamond!!! Kama kuna shida kwenye familia huwezi kuimaliza kupitia magazetini!!! Najiuliza, Leo hii Diamond anaenda kufanya Show, halafu anaona Baba yake anaongea hivyo kwenye magazeti, Je hii ndio itafanya mahusiano baina yao yawe mazuri???? Ikiwa kwamba watu wote tususie kwenda kwenye Show ya Diamond kwa sababu ya kuchukia Diamond alichamfanyia Baba yake, Je hiyo itasaidia mahusiano ya Baba na mtoto kurudi????
Baba Diamond elewa Diamond ni mtu maarufu na umaarufu unakuletea marafiki na maadui. Kama Baba; tumia hekima na tumia wazee wenye hekima kwenye familia yako, watakusaidia kutatua tatizo lililopo baina yenu. Ninaamini kabisa unaweza kurudisha mahusiano mazuri na mtoto wako, ila Tumia HEKIMA na BUSARA, vinginevyo utakuta unaharibu zaidi!
 
Kama kweli alimtelekeza Diamond asimsaidie huyo mzee, ningekuwa mimi ndio Diamond Hata akifa siendi kumzika,Diamond anamsaidia mama yake kwa sababu alimlea kwa tabu.
 
Mie kila siku mpinzani sana wa huyu dogo Diamond, LAKINI kwa hili huyu baba yake hajamtendea haki mtoto wake Diamond.
- Kwanza hujamletea ulimtupa akiwa mdogo hio tayari ni laana.
- pili mtoto wako ana show nzuri na mkwe mtarajiwa wewe baba yake unajitokeza kwenye media kurusha utumbo wako.

Huyu mzee mwache aumwe maana anazidi kumtendea sivyo ndivyo dogo.

Diamond tupa kule huyu dad sie kabisa.
 
angekuwa mgonga mawe angemrusha kwenye vyombo vya habari amsaidie? kama sio kuendelea kumtusi? amwache arushe shoo yake apate pesa ya kumhudumia mama yake aliepata mateso, aliekesha kwa ajili yake , alinusurika kufa kwa ajili yake
 
kulea hamtaki mnajua kumwaga tu,si bora muwe mnamwaga kwenye viputo
pu.mb.avu kabisa
 
kwa hiyo analipiza kisasi?du jamani binadamu hatari kwa nini asimsamehe ili nae aje asamehewe hapo mbele ya safari,wengi tuliachwa na baba zetu kwa sababu moja au nyingine na siyo lazima kujua kwa nini baba yako alipotea,tunasubiri akianza kupukutika na kurudi mitaani kama kawaida ya wasanii wa bongo ndiyo tutaongea sana

Hakika uko sahihi vitu vingine katika maisha ya wanadamu utokea kwa sababu!!!!Na ili la Nasib aka Diamond/Platnumz ni matokeo ya mambo yanayotokea Mungu akiwa na makusuido uenda si kwa Baba ya Diamond bali kwa Diamond mwenyewe...

Ebu itizame hii uenda mtafaruku wa Baba na Mama yake ulipoingia kwa namna ambayo wazazi hao wanajua mtoto akasimama kwa Mama..ila siri ya yote hayo wenye majibu ni wao wawili.Lakini kama mtoto unapokuwa na kupata ufahamu basi kwa kujua umuhimu wa Baba na Mama [Spirtually] unapaswa kuwa nguzo ya kuwafanya kila linapokuja jambo linalokuhusu wewe basi uungana japo mara moja na kumshukuru Mungu kwa wewe kuwepo Duniani...na kwa maajabu yake hawakujua kuwa LEO hii kupitia damu walizochanya wao kwa kiumbe Diamond basi amekuwa mtu maalufu Tanzania kwenye sekta ya burudani [Entertainment].

Nani anae leta fikra za Wazazi hawa kuungana pale lipokuja swala la shughuri yoyote ya Diamond..Ni Diamond mwenyewe kwa kuhakikisha anaishi vizuri na sehemu zote mbili [Zisizo ishi pamoja kama familia moja].Yani ndio kusema anajitahidi kumpa Mama matunzo mazuri kwa kadri anavyoona inafaha kwa kuwa amekuwa kipenzi chake muda wote, lakini pia kuwajibika kumuudumia Baba kwa mambo ya msingi na kuhakikisha uwanaume wa Baba kuzaa kidume anaitwa Diamond unasikika Nchi nzima,na kwa wanaume huo ndio ugonjwa yani SIFA HESHIMA....Japo baba uenda hakuwajibika kimalezi lakini kama binadamu mwenye ufahamu ni fursa ya kumuonyesha kuwa alikosea [To Prove HIM wrong] kuwa Mungu alikusudia Diamond awe kitu bora kilichowai kukaa kwenye kiuno cha Baba yake.Kadri alivyopasa kuwa karibu na Baba yake na kumuhudumia ndio BABA ya Diamond angezidi KUMTUKUZA MUNGU WAKE kuwa alifanya makosa na anatubu kwa dhati kwa yeye kutokuwajibika lasmi kwa Mwanae huyo ambae leo ni mtu maalufu Nchini na amefanikiwa kimapato.

Sasa kitendo cha yeye kumkimbia Mzee wake kwa excuse ya kuwa AKUMLEA ni UPOFU and SOON AND VERY SOON -kwa Wakristu tunasema kuna sheria kumi za MUNGU. Na moja inasema WAHESHIMU BABA NA MAMA YAKO UPATE HERI NA MIAKA MINGI DUNIA.

Sasa uenda tunafikiria MUNGU alikuwa na makusudi na Baba ya Diamond na leo hii analipwa kwa kumtelekeza Diamond wakati hatujui nini hasa kilitokea kati ya Mama Diamond na Baba yake Diamond.Lakini pia uenda MUNGU alikuwa na sababu ya kuwa atamkuza Diamond aje kuwa mtu maalufu kiumbe mwenye moyo wa KUSAMEHE na kumfanya MUNGU ajisifie kupitia Diamond kuwa aliweza kulelewa na Mama yake lakini alimsamehe Baba yake na kwa kuwa ni alama ya Taifa [Nationa Icon] AKAIBUA MWAMKO WA MAMILIONI YA VIJANA WA KITANZANIA KUWA NA MOYO WA KUSAMEHE WAZAZI WAO AMBAO WALIWATENDA WATOTO AMBAO HAWAKUWA NA SAUTIYA KUONGEA NA KUWASIKIA ZAMA HIZO.

Kwa MSAMAHA WA DIAMOND kumchukua Baba yake na kumpa matibabu yanayostahiki na kumuhudumia kwa mahitaji yake ya kimsingi na kumfanya sehemu ya familia yake muhimu basi MUNGU angekuwa amekubalika moyoni mwa Diamond na hivyo kwa ishara hiyo Taifa pia likapata vijana wenye kujifunza kusamehe-[Mfano tungeweza siku za usoni kusikia misemo toka kwa vijana kama ''x-fododo ameshindwa kumsamehe Mama yake, Diamond aliweza kumsamehe na kumkumbatia Baba yake sembuse yeye!!].

Hayo yote ni KIPIMO cha jinsi gani HATUKO DUNIANI kimakosa tuko hapa kwa sababu!!!na uenda sababu ya Diamond sio huo Usuperstar ..uenda MUNGU anaongea na Watanzania kupitia Diamond na Baba yake ambao kwetu ni kama wako kila mtaa au ni majirani zetu mtaani.

Kwa jinsi ya uzoefu wa kuona maisha tunayopita na misemo ya wahenga kama What goes around Comes around, Sikio halizidi kichwa, hakuna malefu yasiyo na ncha, usitukane mkunga na uzazi ungalipo...Diamond anaweza kumuona Baba yake is nothing kwake lakini SPIRITUAL BABA YA DIAMOND ni mkubwa zaidi ya umaalufu huu tunaomshabikia nao hapa.Kwa dini yake amtafute Sheikh Mkuu Mzee Simba [mzee mmoja muungwana sana toka viunga vya Majengo Shinyanga], amwambie Mzigo aliona dhidi ya Baba yake basi kupitia IMANI yao atamuongoza jinsi kusimama na wao kuendelea na maisha kama familia moja japo kunautengano yeye akiendelea kuwapa raha Watanzania na nyimbo zake za mapenzi.

Akiendelea kumwegamia Mama na kusikiliza mawazo ya Mama wakati kupitia mahusiano ya wanakidada kadha wa kadha kama Hawa, Wema, Penny, Jokate na leo Zari basi kidogo amepata kujifunza tabia za mamazetu pia sasa ni fursa nae pia akamsikiliza baba na kuvaa viatu vyake ata kama yeye alikuwa na makosa asamehe na kusahau ili apate KIBALI CHA MUNGU.

Kama TAIFA yashatusibu kwa Kipenzi cha Watanzania upande wa sinema za Kitanzania R.I.P The Great One...Sura hii ya Diamond haina tofauti kwa asilimia kubwa na picha hii ya The Great....Watanzania waliongea mengi lakini mazingira haya hayatokei hivi hivi kama watu hawajui IMANI ni nini, basi ni mwanzo mwema wa kujifunza na kufahamu misemo muhimu ya kiimani kama huu wa ''WATU WANGU WANA ANGAMIA KWA KUKOSA MAALIFA''.

Baada ya Show ya Zari All White Party Usiku wa Leo basi kuepusha sauti ya Baba isiongelee tumboni na umma wa Wanaume wa Tanzania wakagumia nae tumboni basi YASULUHISHWE NA AMPE HUDUMA BABA YAKE.Manake Wanaume watu wazima wanasema mheshimu Mama yako kwa kuwa kakuzaa wewe lakini na yeye Mama yako ni Mwanamke kwa Wanaume wengine...kauli hiyo ya Wanaume watu wazima ndio kusema wanasema WEMA SEPETU, PENNY AU JOKATE nao siku za usoni zisizo na jina watakuwa Mama za Watu.

VINGINEVYO ......VINGINEVYO.......VINGINEVYO...KUENDELEA KUISHI HIVYO UNAVYO ISHI NA BABA YAKO..mmmh haya tusiseme sana watu wazima wa Kiafrika usema TEMEA MATE CHINI....!!!
 
Wakati huyu mzee ana pesa ndefu ikawa Diamond akimfata magomeni kumsalimia tu alimfukuza akimwita chokoraa, akuwai kujua anakula nini wala anapona na nini akiugua. Leo unatafuta huruma kwenye media, malipo siku hizi ni hapa hapa duniani.
Watoto ulioona wa maana wako wapi? Diamond angeishia kwenye drugs kama wenzake wa Tandale ungemkumbuka? Mi naomba usife mapema ili uendeleee kukiona cha moto.

Aloo una hasira wewe... kha! Kama nakuona vile.
 
Sperm donor na BABA ni vitu viwili tofauti. Huyu ni sperm donor tu. Baba wa Diamond ni Mama Diamond! Mama Diamond ndio Baba na Mama. Hakuona sababu ya kutoa matunzo kwa Diamond na uwezo alikua nao!!! Shame on him!
"Any man can be a dad, it takes a real Man to be a father" by Barack Obama.
 
Yote kwa yote huwezi kujua mambo ya ndani waliofanyiana, lakini wakati mwingine Mungu anakupa majaribu ili uyashinde.

Pengine bila baba yake kumtelekeze Diamond asingekuwa hapa alipo, hayo ni makusudi ya Mungu.

Kwa kumrudishia fadhila Mungu ni vema akamsaidia huyo baba yake kama anavyowasaidia watu wengine wasio mhusu.

Mungu hana visasi anapenda kusamehe.


Well said @ idawa
 
..unigegede, unitie mimba, utoke nduki, mtoto akue & afanikiwe... Vinono ule weweee! majangaaa ooh majangaaaa
 
Hivi angekuwa mwanawe Bado anauza mitumba tandale angebwambia aje kukaa hapo kwake?.. Kama yy alikuwa hamtak tangu utoto Leo anafata nin maanina zake huyo mzee
 
Naomba hii iwe fundisho kwa wababa na wamama wote mliotelekeza watoto halafu mnaomba huruma ya watoto wanapofanikiwa. Hakuna laana yoyote itakayompata diamond maana hakuna gharama yoyote huyu baba katumia juu ya diamond.
Kweli kabisa,sipendi watu wanaotelekeza wake na watoto wao.Nakumbuka miaka ya nyuma kuna jamaa mmoja alitoka Marekani kuja kutafuta wazazi wake hapa na alitembelea hadi kituo alicholelewa hadi kitanda alichokuwa analala..jamaa huyo kwa kweli alipata wababa wengi sana maana walijitokeza wengi wakidai ndo baba mzazi wa mtoto.Hii inafundisha kuwa watu wapo katika mafanikio tu lakini mtu huyo huyo akiwa maskini huoni hata mdomo ukikosea na kuita jina lake...the same apply to our normal life tu ikiwa kuna mtu ni maskini katika family basi hashirikishwi katika mengi sasa ngoja mtu azichange muone,aisee sijui nitafanya kitu gani.
 
Mpwa vp! Niaje ni vp ni poa, leo utakuwa pande zp nkucheki

Hata Yesu akawaambia wanafunzi wake,"Yeyote asiye na dhambi na anyanyue mkono wake kumpiga huyu mwanamke". Nadhani nitakuwa sijakosea maneno.
Kila mtu ana dhambi,hakuna aliye msafi.

"Nlikuwepo":bolt:
 
Huyu baba anatafuta huruma aiseeee kipindi anamuacha alikua wapiii asituharibie siku ye aumwe ajiuguze tu kwani alimzaa daimond peke yake kelebu wahed😰😰😰😰😰😰😰😰😰😰
 
Back
Top Bottom