GE2025 Baba Levo aangukia pua, Ng’enda aibuka mshindi Kigoma Mjini kwa kura 2,168 dhidi ya 2,080

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini anayetetea nafasi yake, Shabani Ng’enda, ameibuka mshindi katika kura za maoni za Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kupata kura 2,168.

Clayton Revocatus Chipando maarudu kama BabaLevo ameshika nafasi ya pili kwa kupata kura 2,080, huku Mwandishi wa Habari Baruani Muhuza akishika nafasi ya tatu kwa kupata kura 264.

Matokeo hayo yametangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi wa CCM kwa Jimbo la Kigoma Mjini, Sadick Kadulo ambaye pia ni Katibu wa chama hicho Wilaya ya Kigoma.

1. Kirumbe Shabani Ng’enda – kura 2,168

2. Clayton Revocatus Chipando, Baba Levo– kura 2,080

3. Baruani Muhuza – kura 264

4. Dkt. Ahmad Yahya Sovu – kura 247

5. Dkt. Maulid Mohamed Kikondo – kura 180

6. Mosese John Basila – kura 12
 
Levo atapata japo UDAS....si haba
 
Kwani Majina sio kwamba yanarudi tena kamati kuu kwa ajiri ya final edit?

Dr charles kimei pale vunjo hakuwa nafasi ya kwanza 2020 ila alirudishwa kama mshindi.

Pale Rorya Jafar Chege naye hakushinda...alibebwa bebwa tu kama Hamis mwinjuma
 
Chege alishinda, tazama vyanzi vyako vya habari uone
 
Back
Top Bottom