Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Mhe. Baba Levo, ametoa ushauri kwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuwekeza zaidi katika maendeleo ya timu ya taifa, hususan kwa kuwajengea uwezo wachezaji vijana watakaoiwakilisha Tanzania katika michuano ya AFCON 2027, ambayo nchi itakuwa miongoni mwa waandaaji.
Akichangia mjadala wa bajeti ya wizara hiyo Bungeni jijini Dodoma, Mhe. Baba Levo alisisitiza kuwa maandalizi ya mashindano hayo hayapaswi kuishia kwenye uboreshaji wa viwanja na miundombinu kama barabara pekee, bali lazima yaende sambamba na uwekezaji kwa wachezaji chipukizi wenye vipaji.
Alionya kuwa bila mkakati wa makusudi wa kuandaa kikosi imara cha vijana, taifa linaweza kupata matokeo mabaya. “Tukiboresha viwanja na kujenga barabara halafu tukapeleka wachezaji wazee bila vijana tutapata aibu mbele ya Rais,” amesema