Baba mchungaji na Mama mchungaji

Baba mchungaji na Mama mchungaji

Kula bata na mama mtumishi.achana na maneno ya wanadamu.hawaishiwi maneno hawa.kula kuku.nami nipo njiani ni kuenjoy na mama toto tu saiv
aaah hawana habari. Nimependa mguu wa mama Mchungaji
 
Walokole washamba sana,na beach pia mnataka watu waende na magauni?,angekuwa amevaa kinguo cha kubana na anamshepu hapo mngekuwa na haki ya kuongea.Tatizo la bongo hatujui kuwa kila vazi lina wakati na eneo linapopaswa kuvaliwa.ndo maana wadada nguo za kutokea out usiku wanavaa kwenda kufanyia shopping kariakoo.
Sio ushamba mkuu. Wanakaririshwa huko kwenye mafundisho yao. halafu wanaogopa kuhoji chochote. Mambo ya ajabu kabisa. Utakuta binti anavaa gauni la mwaka 90 halafu anajiona mtakatifuuu...
 
Pamoja na kwamba umekosea andiko halijasema mavazi ya kiume. Ila imeandikwa ""yampasayo mwanaume". Vazi gani ni la kiume kati ya hayo aliyovaa huyo binti? Hiyo ya juu ni ya kiume? Hiyo pence ni ya kiume? Kama ndivyo, jaribu kwenda ukanunue pensi kama hiyo wewe uivae kama ni mwanaume halafu ujione namna uume wako utakamailika.

Nenda kachukue jeans trouser ya kike, ama skin jeans za akina mama uvae utembee nayo uone vile unakuwa mwanamme halisi.

Nenda kachukue trouser suit ya kimama, uvae uendenayo kunakotakiwa kuvaa suti ujione namna gani uanaume wako ulivyo.

Acheni kuhalalisha mila zenu mzigeuze ziwe maagizo ya Mungu.

Watu wengi wanaangamia kwa kukosa maarifa.

Sipendi kuongelea mavazi hasa ya hawa mama zetu ambao wanaonewa kwakila namna.

Maoni yanakaribishwa
Well said mkuu. Anayedhani hicho kikaptula ni cha kiume akainunue aivae mdo aje hapa aongee. mavazi ni suala la kitamaduni. Nenda nchi za wenzetu utakuta almost kila mwanamke anavaa suruali mpaka makanisani na ni kitu cha kawaida.
 
Mkuu, nakubaliana na perspective yako..japo kwenye Ukweli tuseme tu. Kuhusu hako ka kaptula ka huyo mwanamke hakafai kwa mtu anayemuogopa Mungu. Hayo ni mavazi ya kikahaba period. mwanamke Hayuko decency.

We all know, Ujana nao tabu sana. Hayo ni maigizo ya ujanani. Wakikua wataacha.
Inaonekana wewe hujawahi toka nje ta Tz. Nenda hata hapo south afrika ingia kanisa unaloliheshimu. Utakuta wanawake kibao wamevaa nguo za aina hiyo.

Suala la mavazi ni tamaduni za jamii. Sasa usilazimishe mavazi za huko kweni ziwe za kuvaliwa na kila mtu.
 
Kwa jinsi walivyovaa Biblia Takatifu inatufundisha kuwa utaweza kuwatambua kama ni nkweli wachungaji wa Kanisa la Mungu au watumishi wa kitapeli. Hivi vitu havijifichi. Mtumishi wa Mungu haachi maswali na hata akijifanya kwamba hamfahamu Mungu atajulikana tu kuwa ni mtumishi wa Mungu. Kumbuka Petro alipojaribu kusema hamfahamu Yesu na akaanza kuondoka ila waliokuwepo wakasema kuwa hata anavyotembea inadhihirisha yeye ni mtu wa Kristo. Je kwa muonekano wa Masanja, yeye ni mtumishi wa Mungu aliye hai????
Anaweza akawa mtumishi wa Mungu lakini asiyempendeza Mungu kwa vitu vichache na kweli sisi ni barua lazima tusomeke ndani na nje maana maandiko yanasema tusiifuatishe namna ya dunia hii na tusiipende lazima tuwe tofauti kwanzia muonekano mpk ndani ya mioyo yetu.Mbinguni si pa rahisi kama tunavyodhani ndugu zangu wote.Hii tunakumbushana tu tuew makini.
 
Mungu haangalii Mwili bali Roho
Nikusahihishe kidogo soma biblia vizuri inasema Miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu sio roho zetu tu pia na miili so tuwe makini wapendwa. 1Korintho 6:19.
 
Kwa jinsi walivyovaa Biblia Takatifu inatufundisha kuwa utaweza kuwatambua kama ni nkweli wachungaji wa Kanisa la Mungu au watumishi wa kitapeli. Hivi vitu havijifichi. Mtumishi wa Mungu haachi maswali na hata akijifanya kwamba hamfahamu Mungu atajulikana tu kuwa ni mtumishi wa Mungu. Kumbuka Petro alipojaribu kusema hamfahamu Yesu na akaanza kuondoka ila waliokuwepo wakasema kuwa hata anavyotembea inadhihirisha yeye ni mtu wa Kristo. Je kwa muonekano wa Masanja, yeye ni mtumishi wa Mungu aliye hai????
Kwa mungu anayerandaranda duniani leo Masanja naye ni mchungaji, kila mtu anaweza kuwa mchungaji leo. Hebu tembelea makanisani leo uone mambo yanayoendelea! Ukifikiria sana unaweza kutafuta dunia yako mwenyewe, acha tu tusubiri siku ya hukumu!
 
Mkuu unachembe'chembe za uwestern!! maana bongo mko wachache wanaume wengi yao chura. Makofi kwa models [emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
Mamodel utawajua tu.....ngoja nami nikazane na gym niwe model.......
 
Mamodel utawajua tu.....ngoja nami nikazane na gym niwe model.......
Usiende gym bana, sisi wengine tunakuhitaji hivyo hivyo ulivyo. mamodel hawana hata nyama ya kupapasa. Mifupa nje nje.
 
Usiende gym bana, sisi wengine tunakuhitaji hivyo hivyo ulivyo. mamodel hawana hata nyama ya kupapasa. Mifupa nje nje.
Ah inanipa limit ya nguo...mie madela tu kwa kwenda mbele nashndwa kuvaa vikaptula kama huyo.......
 
Walokole washamba sana,na beach pia mnataka watu waende na magauni?,angekuwa amevaa kinguo cha kubana na anamshepu hapo mngekuwa na haki ya kuongea.Tatizo la bongo hatujui kuwa kila vazi lina wakati na eneo linapopaswa kuvaliwa.ndo maana wadada nguo za kutokea out usiku wanavaa kwenda kufanyia shopping kariakoo.
Hivi mkuu huja wahi kwenda beach halafu ukakuta watu wamepiga hijab zao furesh tuu!?

Japo siungi mkono kumlazimisha mtu avaeje, ila hao wanao lalamika nao wana sababu zao.
 
makanisa ya kiroho na changa moto zake,sasa hivi naona hata katoliki wanavutwa kwa kasi na makanisa ya kiroho wameamua kulegeza baadhi ya kanuni pia..!!!
 
Back
Top Bottom