Mafeking
JF-Expert Member
- Aug 21, 2018
- 225
- 471
Habirini wana jamvi,
Nimeona nilete kisa hiki jamvini mimi ni kijana nimelelewa na baba MLEZI na kanisomesha Hadi form six, na alitaka niishie hapo nisiendelee mbele.
Mimi nililazimisha kwenda chuo kwasababu malengo yangu hayakuwa niishie form six maana matokeo yangu yaliruhusu kwenda kujiunga na chuo, na hapo ndipo shida, matatizo na migogoro ilipoanzia maana Hadi na apply vyuo sikumwambia sababu hakuwa na point ya yenye uzito ya mimi kutoenda chuo, mfano wa sababu zake zilikuwa "chuo ni kupoteza muda" Sasa ikifika siku ya mimi kwenda kuripoti chuo nilikchokuwa nmechaguliwa niliona ni vyema nimuage Kisha nianze safari, lakini cha ajabu yeye alinijbu " we nenda lakini usiniambie wala usinihusishe Kwa lolote"
Baada ya kufika chuo nikaona nimjulishe kama nmefika salama lakini hakunipokelea simu zangu na hakuwahi kupokea simu zangu kuanzia hapo na hakuwahi ata kunipigia simu nikaona isiwe kesi nikamjulisha mama kuwa sipokelewi simu akajibu " endelea kumpigia usiache" nikaendelea kumpigia simu bila matokeo yoyote
Ikabidi niwe napiga Kwa mama ndipo mama ampatie simu niongee nae nilkuwa naumia ila nilijikaza, na nyumban wakawa hawaelewan ugomvi kila kukicha
Kipindi tunakaribia kufunga chuo nilikuwa sitamani kabisa kurudi nyumbani kwasababu ya hiyo migogoro.
Miaka kadhaa iliyopita mama akaamua kuondoka nyumba sababu yake kubwa anasema ni kunyanyasika na baba akao doka na kuwaacha wadogo zangu watatu
Na hivi karibuni wamefikishana mahakamani mama akidai talaka na mzee nae anadai FIDIA ya kunisomesha na mimi sitaki kuingilia ugomvi wao juzi juzi tu hapo mzee aliniomba mkoa ili tumzuie mama kuhusu hiyo talaka.
Naombeni ushauri juu ya hili kudai fidia maana Toka nilivoondoka nyumba kwenda chuo sijarudi tena tangu 2018 na Sasa nipo mtaani napambana.