Baba mlezi ananidai fidia kwa kunisomesha

Baba mlezi ananidai fidia kwa kunisomesha

Anadai Hadi chuo
Sasa si ndio na wewe pakujiinulia hapo.

Mtu alikutosa kwa maneno na matendo we unashindwaje kujiepusha nae. Mtamkie achukue time zake asiwaze kma aliwahi kuwa na mtoto wa kambo kama wewe
 
Kwa akili hii ndio maana sikutaka kuendelea kupoteza hela zangu ili usome chuo,

Nilishaona mwisho wako ilikua ni hiyo form six tu,

Kunitangaza humu hakuwezi kuubadili msimamo wangu.
 
Mimi hapo sijaona changamoto ni hiba huru tu za wanandoa ila wewe ndo kachumbali yao. Fanya mishe zako achana nao wote wanajuana.
 
Mnaooa single mother, mkumbuke akiwa na mtoto wa kiume kataa, kimbia au ujiandae na vita mbeleni.
Maana katakuja kuwa kikwazo kwenye maisha yako baadaeb, ukimsoma na kuchambua kwa makini utagundua huyu kijana yupo upande mmoja na mama yake.
na wewe wacha utabiri mbaya, lete uthibitisho wa hayo unayoyasema. Sasa ulitaka mtoto akae upande gani ikiwa baba mwenyewe anaonyesha chuki?
 
Mlipe mmalizane, Bodi ya mkopo lazima ulipe Usikasirike Mlipe ila mwambie utamlipa utakapo pata lakini nasisitiza Mlipe hata ukipata 500 ukiona inafaa kumpa We MPE.

Mwanadamu anaetaka malipo ya kitu alichokufanyia kama kinalipika we mpe kisha baki zako kwa amani.
 
Mnaooa single mother, mkumbuke akiwa na mtoto wa kiume kataa, kimbia au ujiandae na vita mbeleni.
Maana katakuja kuwa kikwazo kwenye maisha yako baadaeb, ukimsoma na kuchambua kwa makini utagundua huyu kijana yupo upande mmoja na mama yake.
Sio kweli mkuu mimi sina upande wowote ila sijataka kuingilia ugomvi wao ila kilicho nishtua ni kwamba aliposema alipwe fidia Kwa kunisomesha tena mahakamani.
 
Habirini wana jamvi,
Nimeona nilete kisa hiki jamvini mimi ni kijana nimelelewa na baba MLEZI na kanisomesha Hadi form six, na alitaka niishie hapo nisiendelee mbele.

Mimi nililazimisha kwenda chuo kwasababu malengo yangu hayakuwa niishie form six maana matokeo yangu yaliruhusu kwenda kujiunga na chuo, na hapo ndipo shida, matatizo na migogoro ilipoanzia maana Hadi na apply vyuo sikumwambia sababu hakuwa na point ya yenye uzito ya mimi kutoenda chuo, mfano wa sababu zake zilikuwa "chuo ni kupoteza muda" Sasa ikifika siku ya mimi kwenda kuripoti chuo nilikchokuwa nmechaguliwa niliona ni vyema nimuage Kisha nianze safari, lakini cha ajabu yeye alinijbu " we nenda lakini usiniambie wala usinihusishe Kwa lolote"

Baada ya kufika chuo nikaona nimjulishe kama nmefika salama lakini hakunipokelea simu zangu na hakuwahi kupokea simu zangu kuanzia hapo na hakuwahi ata kunipigia simu nikaona isiwe kesi nikamjulisha mama kuwa sipokelewi simu akajibu " endelea kumpigia usiache" nikaendelea kumpigia simu bila matokeo yoyote
Ikabidi niwe napiga Kwa mama ndipo mama ampatie simu niongee nae nilkuwa naumia ila nilijikaza, na nyumban wakawa hawaelewan ugomvi kila kukicha

Kipindi tunakaribia kufunga chuo nilikuwa sitamani kabisa kurudi nyumbani kwasababu ya hiyo migogoro.

Miaka kadhaa iliyopita mama akaamua kuondoka nyumba sababu yake kubwa anasema ni kunyanyasika na baba akao doka na kuwaacha wadogo zangu watatu

Na hivi karibuni wamefikishana mahakamani mama akidai talaka na mzee nae anadai FIDIA ya kunisomesha na mimi sitaki kuingilia ugomvi wao juzi juzi tu hapo mzee aliniomba mkoa ili tumzuie mama kuhusu hiyo talaka.

Naombeni ushauri juu ya hili kudai fidia maana Toka nilivoondoka nyumba kwenda chuo sijarudi tena tangu 2018 na Sasa nipo mtaani napambana.
huna sababu youote ya kulipa fidia,na mwambie waziwazi kuwa hutamlipa fidia na hana popote pa kukupeleka,ama kuhusu ugombi wake na mkewe,ambae ni mama yako,waachie wao
 
Huyu kijana na mama yake ndio uthibitisho
Hapa nimepata somo usikubali kuoa single mother mtoto/watoto wa mkeo hawawezi kukumbuka daima, na wakikua huyo mke na watoto wake wataibua vita dhidi yako.
 
Back
Top Bottom