Baba mtoto kanitelekeza

Nimecheka kweli kweli. Bado hujafikia huko?

Kwakweli nyuzi zote zinazoandikwa za kulalamika kuhusu mapenzi me hua najua walengwa ni ambao wako in their 20's.. Nimeshangaa kuona mtu mzima naye anasumbuka nayo
Watu wazima wanaohangaika na hizi ishu ni wengi mno ila wanaona aibu na sometimes wanaamua kujiua na kuua watoto sababu wakijitokeza kwenye Jamii badala ya kupata msaada watu wanaishia kuwakebehi. Ila wakisikia wamefanya madhara Kwa familia, watasema "Si angeongea!"
 
Pole. Mwanamke ukishaona mwanaume aliyekupa ujauzito anakuambia utoe basi hiyo ni green light kimbia kufa kupona.

Hakuna mwanaume anayeweza kumpa mwanamke anayempenda ujauzito kisha akamuambia autoe.

NEVER!
 
Hayo ni malalamiko ya upande wako ukijipamba, we tabia zako zipoje , wanaume wengi wakiona mwanamke mzinguaji wanakupuuza tu na kukupotezea

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli lakini mnachoshangaza, ukiona huyu akufai, unamganda ili iweje? Why wasting ur time? Ama unakua na watatu, wote pia Wana shida?
 
Ni kweli kabisa.
Pole. Mwanamke ukishaona mwanaume aliyekupa ujauzito anakuambia utoe basi hiyo ni green light kimbia kufa kupona.

Hakuna mwanaume anayeweza kumpa mwanamke anayempenda ujauzito kisha akamuambia autoe.

NEVER!
 
Amekwambia toa mimba muda bado. Ukakataa. Sasa kakutelekeza kivipi wakati umeapa kwake liwalo na nalo liwe?!
Acha kulazimisha majukumu kwa mwanaume. Umejitakia mwenyewe kuwa single maza. Pambana na Hali yako...
Kwa hiyo ni sawa kumwaga damu sababu ya kulea? Na Hakuna sehemu niliyosema ninamtegemea. Sijui ni kwanini wengi mnaongelea abortion kama kuchinja kuku. Huwezi kukionea kiumbe kisicho na hatia huruma? Utembee na dhambi ya kumwaga damu hadi siku ya kifo? Ili iweje, aendelee kubaki na mimi then nikiwa naye napata faida gani kubwa? Kwa uzazi ulivyo changamoto hivi? Mbona kuna wababa wana huruma mno, wanabeba majukumu huku wanaamua kuwa Ni mtoto aliyetelekezwa. Na uzuri mtoto akiwa Hana mzazi, anasimamiwa na Mungu.
 
Kwakweli Bora umeongea, hiyo ya kujidhuru ndo mbaya zaidi
 
Nimeanza kuamini kweli mapenzi hayana umri
Imagine watu wameoana, wanawatoto Zaidi ya watatu, baba kaamua kuoa mtu mwingine kimyakimya na kutelekeza familia 😒 hiyo utafananisha na kukimbiwa na baba mtoto ambaye hamkuwa kwenye maagano? Wababa wengi wanateseka ila watasemea wapi!
 
Unaweza kukuta hata wazazi wetu wanateseka Ila ndo hivyo Tena hawana namna inabidi watunze heshima ya familia 😌😌
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…