Baba mweupe Mama mweupe watoto weusi kitaalamu inakaaje?

Mambo ya dominant v/s recessive genes. Biology ya form 4.
Wenzio wakiwa darasani, we unajificha chooni kupoteza muda.
😁
Jokes tu.
 
Hujasoma genetic?
 
Wanafanana na bibi mzaa bibi wa bibi wa bibi wa bibi wa bibi yake aliyekuwa mweupe sio kesi hata kama wewe mweusi kama wa Sudan kusini au wajaluo

Rangi hujirudia hata baada ya karne miaka 100 au 200 mwanao huyo huhitaji hata kupima DNA

Hongera sana kuzaa mweupe
 
Nimesoma hii mada nimegundua watanzania wengi huwa tunaenda Shule kupoteza muda tu na sio kuelewa! Kiukweli mtu yeyote aliyemaliza form four na akawa haelewi chochote kuhusu suala hili, huyo hakuelewa chochote huko ShuleniI labda kama alikumbia Masomo yo sayansi!.. Ukifika form four topic ya HEREDITY inaeleza vizuri sana hili jambo!.. yaani unaweza ukawa mfupi sana na mke au mme wako nae akawa mfupi sana, lakini Mungu akiwajaliaa watoto labda wanne, inawwza tokea mmoja akawa mrefu sana kama miongoni mean baby au bibi alikuwepo mrefu!
Mfano mwingine!
Unaweza ukawa mweupe sana lakini wazazi wako mmoja ni mweupe kama wewe na mwingine ni mweusi ukaja ukapata mwenzi ambaye nae ni mweupe pee kama wewe lakini nae wazazi wake wawili mmoja ni mweupe na mwingine ni mweusi. Mkizaa watoto wanne, watoto watat watakuwa weupe lakini Kuna uwezekano mmoja akawa mweusi tii kutokana na athari za urithi. NAANZA kumuelewa Lowasa aliposema, ELIMU, ELIMU, ELIMU.
 
Inawezekana kabisa Ki-genetic kufuatana Mendelian inheritance. Hiyo gene ya weupe ipo recessive kwa wazazi wote wawili lakini imekuja kuwa dominant kwa mtoto ndio maana kawa mweupe. Pia kama wazazi wamebeba gene ya rangi ikiwa katika hali ya heterozygous, yaani mchanganyiko wa nyeupe na nyeusi, wakikutana wanaweza kupata mtoto aliye homozygous mweupe au heterozygous mweupe.

Usihofu hilo ni kawaida kabisa.
 
Inawezekana kabisa Ki-genetic kufuatana Mendelian inheritance. Hiyo gene ya weupe ipo recessive kwa wazazi wote wawili lakini imekuja kuwa dominant kwa mtoto ndio maana kawa mweupe. Pia kama wazazi wamebeba gene ya rangi ikiwa katika hali ya heterozygous, yaani mchanganyiko wa nyeupe na nyeusi, wakikutana wanaweza kupata mtoto aliye homozygous mweupe au heterozygous mweupe.

Usihofu hilo ni kawaida kabisa.
 
Hiyo kalii. Yaani mtoto awe mweusi tii asiwe hata maji ya kunde?
Genetic makeup ikikupa imekupa

Unazan unapew nusu kwamba kama baba na mama warefu utapew urefu kdogo , Gen ya urefu utayochukua upande mmoja utaifat hvyo hvyo kwa kimo au rangi kamili
 
Unahakika mama ni mweupee? Maana sikuhizi kuna vidonge na sindano, mtu anakuwa mweupeee bila hata doa.
 
Mwanamke anaweza kushika kimba za WANAUME WAWILI TOFAUTI

Watoto wanazaliwa pacha ila hawafanani au wanafanania mama. Sasa case kama hizi zipo nyingi hususani mwanamke anapokutana na wanaume wawili tofauti wakati wa siku zake za hatari.

 
Mendelian Genetic inheritence Law
 
ninauhakika na ninachosema
 
Angalia viungo kama pua, masikio, kichwa, vidole, mtoto ambae huna Cha kufanana nae sio wako ni wa mkeo na mtu wake mwingine
 
Elimu ni muhimu sana,usipokuwa makini waweza vuruga familia yako kwa ujinga,hii kesi iko kwa familia yangu nina watoto wawili wa kiume ,mimi maji ya kunde na mama yao pia,watoto tunaozaa ni pure white yule wa kwanza huwezi uliza maaana kafanana na mimi sura isipokuwa rangi na wapili kafanana na mama yake sura isipokuwa rangi japo ni wa kiume.

Sasa kuna moja kuna mama mmoja akaanza kuhofu juu ya watoto wangu akimuuliza mke wangu vipi wewe unazaa watoto weupe ilikhali ninyi ni weusi,hapo alilenga kuzua taharuki,ila elimu inasaidia sikuhangaika naye.na wakati anauliza namimi nilikuwa karibu
 
Angalia viganja vya mikononi vya mkeo,nyuma utaona kama ni white kweli mkeo au calorite
 
Sisi sote tumetoka kwa nyani,

Nyani ni huyu hapa (Ni mweusi)

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…