Frumence M Kyauke
JF-Expert Member
- Aug 30, 2021
- 630
- 1,262
Baba mzazi ya Diamond Platnumz, Mzee Abdul Juma ametoa wito kwa mwanawe kuelewana na mwenzake wa zamani Rajab Abdul Kahali almaarufu kama Harmonize.
Alipokuwa kwenye mahojiano na Mbengo TV hivi majuzi, mzee Abdul alimsihi Diamond ashiriki kikao na Harmonize wazungumzie tofauti zao na waelewane.
Mzee huyo ambaye alitengana na mamake Diamond, Mama Dangote miaka mingi iliyopita ameomba serikali na walio karibu na nyota wale wawili wa Bongo kuwapatanisha kuona kuwa wote wanaipeperusha bendera ya Tanzania.
"Wakae tu waelewane, hii dunia ni mapito basi. Yakitokea maneno kama haya wanaotoa hisia wawaagize waelewane wawe pamoja. Alafu tena waziri wa michezo kama yupo vilevile kuna uwezekano wa kuwaita. Mama Naseeb Sanura na Shamte kama wana uwezo wanaweza wakawaita wakaomgea, wakawaweka chini. Watoto kama watawasikiliza waongee kama ndugu waelewane" Alisema Mzee Abdul.
Mzee Abdul alisema hana kinyongo chochote dhidi ya mwanawe wala mpenzi wake wa zamani, Mama Dangote kwani alishawasamehe na kusahau yaliyopita.