Baba na Mwana watatoka lini gerezani?

Baba na Mwana watatoka lini gerezani?

kisugujira

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2012
Posts
774
Reaction score
200
WanaJF,

Hivi ni kweli anayeua kwa upanga naye atakufa kwa upanga? Kama maneno haya ni kweli basi namwomba mwenyezi Mungu yatimie kwa wale wote wanaolihujumu taifa hili kwa kuwakandamiza wanyonge na kutumia mamlaka waliyonayo kupindisha sheria,kusingizia watu na kutengeneza matukio au kesi zisizo za kweli ili wapate kufungwa magerezani!

Wanamuziki ambao ni baba na mwana,Nguza Viking na Papii Kocha mpaka sasa wanatumikia vifungo vya maisha baada ya kusingiziwa kuwalawiti watoto wanafunzi wa shule ya msingi huko Sinza! Katika kesi ambayo kwa sasa inaonekana kusahaulika taratibu kama ilivyo kawaida yetu, mwanasheria maarufu nchini Mabere Marando aliweza kuwatoa katika kifungo cha maisha watoto wawili wa Nguza Viking waliokuwa wamefungwa gerezani pamoja na baba yao!

Mpaka sasa haijulikani ni nani aliyeshinikiza na kuitengeza kesi iliyopelekea familia ya Nguza Viking kupatwa na masaibu haya ya kufungwa maisha gerezani! Ni nani mtu huyu aliyefanya yote haya? Bila shaka atakuwa ni mtu asiye na huruma na hatari sana! Kuna utata mkubwa katika kesi hii kwani mwalimu aliyesemekana kuwa ndiye aliyekuwa akiwapeleka watoto wanafunzi kulawitiwa nyumbani kwa Nguza Viking aliachiwa huru kisha baadaye alihama shule na kwenda kusikojulikana!
 
alikula mzigo wa kandamizaji sasa nayeye analiwa
 
Bado mwaka mmoja na miezi kazaa atoke, baada ya serikali ya wana nchi itakapoingia madarakani.
 
Ktk mambo amboyo utawala uliwahi kukosea moja wapo ni hili
 
ushasema walifungwa maisha sasa unauliza watatoka lini

Mkuu Safari_ni_Safari amekupa jibu la swali lako la kijinga kabisa! Jaribu kutafakari kabla ya kukurupuka na kujibu. Imekuwa ni kasumba tena iliyo mbaya kwa baadhi ya watu kutoa hoja au michango dhaifu na hovyo dhidi ya mada muhimu kwa jamii hapa JF kama ilivyo bungeni,ili kupotosha na kudhoofisha uhalisia wa mada hizo!
 
Bado mwaka mmoja na miezi kazaa atoke, baada ya serikali ya wana nchi itakapoingia madarakani.

Mungu mwenyezi awalinde awape afya njema na kuwatoa gerezani Nguza Viking na Papii Kocha kama alivyowatoa Paulo na Sila gerezani.
 
Ktk mambo amboyo utawala uliwahi kukosea moja wapo ni hili

Labda aliyeipiga pigo hili la kishetani familia hii ya Nguza Viking ni mungu mtu anayeogopwa sana kuliko Mungu! Inasikitisha sana! Ni nani awezaye kumtendea mabaya jirani yake na asipatilizwe?
 
WanaJF,

Hivi ni kweli anayeua kwa upanga naye atakufa kwa upanga? Kama maneno haya ni kweli basi namwomba mwenyezi Mungu yatimie kwa wale wote wanaolihujumu taifa hili kwa kuwakandamiza wanyonge na kutumia mamlaka waliyonayo kupindisha sheria,kusingizia watu na kutengeneza matukio au kesi zisizo za kweli ili wapate kufungwa magerezani!

Wanamuziki ambao ni baba na mwana,Nguza Viking na Papii Kocha mpaka sasa wanatumikia vifungo vya maisha baada ya kusingiziwa kuwalawiti watoto wanafunzi wa shule ya msingi huko Sinza! Katika kesi ambayo kwa sasa inaonekana kusahaulika taratibu kama ilivyo kawaida yetu, mwanasheria maarufu nchini Mabere Marando aliweza kuwatoa katika kifungo cha maisha watoto wawili wa Nguza Viking waliokuwa wamefungwa gerezani pamoja na baba yao!

Mpaka sasa haijulikani ni nani aliyeshinikiza na kuitengeza kesi iliyopelekea familia ya Nguza Viking kupatwa na masaibu haya ya kufungwa maisha gerezani! Ni nani mtu huyu aliyefanya yote haya? Bila shaka atakuwa ni mtu asiye na huruma na hatari sana! Kuna utata mkubwa katika kesi hii kwani mwalimu aliyesemekana kuwa ndiye aliyekuwa akiwapeleka watoto wanafunzi kulawitiwa nyumbani kwa Nguza Viking aliachiwa huru kisha baadaye alihama shule na kwenda kusikojulikana!

Bado kuna mazingira ya giza kuhusu kesi yake ilivyoendeshwa na ushahidi ulivyotolewa, kwa hivyo bado haiondoi wasiwasi wa wengi tulionao kuwa kuna mkono wa mtu......! Katika mambo ambayo Rais ajaye ataweza kujionesha kuwa ni mtetezi wa haki ni kuondokana na wingu kama hili, ikiwemo kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa
 
Back
Top Bottom