Ndiyo, baba ni zaidi ya kuzaa. Baba ni malezi pia.
Malezi kuanzia mtoto akiwa tumboni mwa mama yake. Kulishika tumbo la mama yake na kusikilizia jinsi mtoto anavyocheza huko tumboni, kuchukua kitabu na kuanza kumsomea hadithi akiwa bado yuko tumboni, ndio ubaba wenyewe huo!
Anapotoka tumboni mwa mama yake na wewe unapopewa heshima ya kukata umbilical cord, ndio ubaba huo.
Mtoto akishatoka tumboni na kushiriki katika kila hatua ya ukuaji wake, huo ndio ubaba. Unamlisha, anakutapikia, unamuogesha, unambadilisha nepi, unacheza naye, unamfundisha mema na mabaya, unampeleka kliniki, na kadhalika.
Ni faraja kubwa sana kwa baba kuwa katika maisha ya mwanae. Wengine baba zetu ndiyo ma BFF wetu na wanetu ndiyo ma BFF wetu!