Baba ni zaidi ya kuzaa -Sikilizeni Clouds FM

Baba ni zaidi ya kuzaa -Sikilizeni Clouds FM

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
Nimeamshwa na hiki kipindi leo chenye mada ya "Nafasi ya baba katika malezi na makuzi ya mtoto". Nimewapenda sana hawa washiriki na hoja zao.
 
Mbona mi napata music tu?

Tusaidie majadiliano yao.

Nawapata sasa. . . . ngoja nifaidike.
 
Ndiyo, baba ni zaidi ya kuzaa. Baba ni malezi pia.

Malezi kuanzia mtoto akiwa tumboni mwa mama yake. Kulishika tumbo la mama yake na kusikilizia jinsi mtoto anavyocheza huko tumboni, kuchukua kitabu na kuanza kumsomea hadithi akiwa bado yuko tumboni, ndio ubaba wenyewe huo!

Anapotoka tumboni mwa mama yake na wewe unapopewa heshima ya kukata umbilical cord, ndio ubaba huo.

Mtoto akishatoka tumboni na kushiriki katika kila hatua ya ukuaji wake, huo ndio ubaba. Unamlisha, anakutapikia, unamuogesha, unambadilisha nepi, unacheza naye, unamfundisha mema na mabaya, unampeleka kliniki, na kadhalika.

Ni faraja kubwa sana kwa baba kuwa katika maisha ya mwanae. Wengine baba zetu ndiyo ma BFF wetu na wanetu ndiyo ma BFF wetu!
 
Kiafrika NN bana hakuna mambo ua kukata umbilical cord wala kubebabeba watoto. Mila ziheshimiwe!
 
Wazazi wote ni muhimu sana sio baba tu.
 
Ndiyo, baba ni zaidi ya kuzaa. Baba ni malezi pia.

Malezi kuanzia mtoto akiwa tumboni mwa mama yake. Kulishika tumbo la mama yake na kusikilizia jinsi mtoto anavyocheza huko tumboni, kuchukua kitabu na kuanza kumsomea hadithi akiwa bado yuko tumboni, ndio ubaba wenyewe huo!

Anapotoka tumboni mwa mama yake na wewe unapopewa heshima ya kukata umbilical cord, ndio ubaba huo.

Mtoto akishatoka tumboni na kushiriki katika kila hatua ya ukuaji wake, huo ndio ubaba. Unamlisha, anakutapikia, unamuogesha, unambadilisha nepi, unacheza naye, unamfundisha mema na mabaya, unampeleka kliniki, na kadhalika.

Ni faraja kubwa sana kwa baba kuwa katika maisha ya mwanae. Wengine baba zetu ndiyo ma BFF wetu na wanetu ndiyo ma BFF wetu!

Sawa kabisa, for some men ubaba excitement(sp) zinaishia kwa first born, but blessed are the babaz(sp) that go all the way, tena nashangaa hawashughuliki whilst they are instrumental in having that child in the first place.
 
Binafsi baba yangu plays a very important role in my life (he cut the umbilical cord) . Niko nilivyo leo sababu ya baba na mama, ila interaction yangu na mama yangu ilianza nilipofika miaka 22... before that nilikua ni mtoto wa baba zaidi. And kwangu alikua both Baba na Mama.
Leo I don't need a father to grow, but I need a strong friendship with a man I can trust in many regards, and he is there. My first adviser, my best male friend. He has ALWAYS been there for me, even when I deserved a lesson, he had faith in me when kila mtu had given up (even me).
Baba yangu did not just bring me in this world, he also helps me sail in it.
I love you Dad.
 
Baba mwema kwa watoto, aliyeshiriki kwa karibu katika malezi, hufanya watoto kuwa "watu" wanapokuwa watu wazima, wawe wa kike au wa kiume.Baba "aliyejitenga" katika malezi ya watoto huvuna majuto siku za uzee wake.Aliyeshiriki vema kulea, huvuna baraka na furaha siku za uzee wake.Chunguzeni mtabaini!
 
Ni kweli baba ni zaidi ya kuzaa kwani ni wengi wana uwezo wa kuwapa watu mimba ni walio wengi hawafai kuitwa baba kwa ajili ya mienendo na tabia zao, kwa hiyo level ya kuwa baba inakwenda na majukumu mengi sana ya kifamilia ambayo watu wengi huyakimbia.
 
hii post imenifanya nitokwe machozi natamani mtt wangu angekua na baba bora na si bora baba
 
Back
Top Bottom