Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Nimeamshwa na hiki kipindi leo chenye mada ya "Nafasi ya baba katika malezi na makuzi ya mtoto". Nimewapenda sana hawa washiriki na hoja zao.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nimeamshwa na hiki kipindi leo chenye mada ya "Nafasi ya baba katika malezi na makuzi ya mtoto". Nimewapenda sana hawa washiriki na hoja zao.
Kiafrika NN bana hakuna mambo ua kukata umbilical cord wala kubebabeba watoto. Mila ziheshimiwe!
Kiafrika NN bana hakuna mambo ua kukata umbilical cord wala kubebabeba watoto. Mila ziheshimiwe!
Ndiyo, baba ni zaidi ya kuzaa. Baba ni malezi pia.
Malezi kuanzia mtoto akiwa tumboni mwa mama yake. Kulishika tumbo la mama yake na kusikilizia jinsi mtoto anavyocheza huko tumboni, kuchukua kitabu na kuanza kumsomea hadithi akiwa bado yuko tumboni, ndio ubaba wenyewe huo!
Anapotoka tumboni mwa mama yake na wewe unapopewa heshima ya kukata umbilical cord, ndio ubaba huo.
Mtoto akishatoka tumboni na kushiriki katika kila hatua ya ukuaji wake, huo ndio ubaba. Unamlisha, anakutapikia, unamuogesha, unambadilisha nepi, unacheza naye, unamfundisha mema na mabaya, unampeleka kliniki, na kadhalika.
Ni faraja kubwa sana kwa baba kuwa katika maisha ya mwanae. Wengine baba zetu ndiyo ma BFF wetu na wanetu ndiyo ma BFF wetu!