Baba niruhusu nizae

fimboyaukwaju

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2020
Posts
2,977
Reaction score
3,798
Hayo ni maombi ya mdada mmoja ambae,nilimlea toka akiwa na miaka 3 hadi kumfikisha chuo kikuu,kwa ngazi ya shahada ya uzamili,sasa ana miaka 34,hajazaa,hajaolewa.

Kila akipata mwanaume hafiki nae mbali,japo ni mdada ambae hanywi pombe,havuti sigara,sio mtu wa kutoka out na nimemlea kwa dini ya kikatoliki japo mie ni muislamu,kwani ndio dini ya wazazi wake ambao kwa sasa hawako duniani

Ana kazi yake na kipato japo sio kikubwa.Kasubiri sana kupata mchumba hapati,tunaongea nae sana,nilimuomba padri wake anakosali amuombee,lakini hakuna kitu,alipata wanaume kama 3 hivi na kumbe walikuwa wanamtapeli maana wote wana wake.

Sasa jana kanipigia simu,baba niruhusu tu ni zae bila ndoa, umri unapita,aisee bila kuficha nililia sana,mwishowe nimemwambia sawa,fanya roho yako itakavyokuongoza
 
Kumbe tupo wengi.story yake inafanana na yangu kwa asilimia kubwa. mimi nilipofikisha umri huo nikaamua kuzaa bila ndoa. sasa hivi ni 36 na katoto kangu kana miaka miwili. nina mfurahia sana mtoto wangu sasa napambana kwa ajili yake. na nina amani mambo ya ndoa nilishayaweka kwenye dampo la taka sasa ni kupambana tu na maisha. unaweza subiri ndoa mwisho wa siku umri ukakuacha kabisa ndoa ukakosa na mtoto ukakosa vilevile.
 
Da! Sasa na yule anayezaa naye hataki kumuoa?
 
Baba wa mtoto hajambo? Anaendeleaje
 
Mwanaume uliyezaa naye hataki kukuoa mkuu?
 
Sikuhizi kumbe mpaka walokole nao wanaipiga na kusepa nao wamesanuka.

Huyo lazima huko chuoni imetumika sana sana ukute mpaka shisha kavuta kama dragon wewe akija kwako anajifanya innocent.

Utapeli mtupu acha akione cha moto
 
Da! Sasa na yule anayezaa naye hataki kumuoa?
nawe huijui hiyo mbinu..?
yani hapo mdada anajipatisha mimba kwa huyo mshikaji halafu baadae ndo mshikaji anabanwa mbavu!, sasa swala la kumuoa ama kutomuoa inategemea na jamaa akikubali sawa akiwa na kichwa kigumu hataoa, atakuwa tu baba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…