BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Burian amesema baada ya mazungumzo ya muda mrefu, Isaka Rafael ambaye ni Baba wa Watoto Mapacha waliofariki katika Kituo cha Afya Kaliua na kuzua taharuki baada ya pacha mmoja kuondolewa na jicho na ngozi ya paji la uso macho, amekubali kushirikiana na Serikali na leo uchunguzi wa kitabibu umefanyika katika Hospitali ya Wilaya ya Urambo.
Akifanya mahojiano na CG FM ya Tabora, Dkt. Batilda amesema licha ya kufanikisha zoezi hilo muhimu la uchunguzi lakini Baba huyo ameendelea na msimamo wa kukataa kuchukua maiti kwenda kuzika akidai ni mpaka atakapokamatwa Mtuhumiwa wa tukio hilo.
Aidha RC Batilda ameiomba Familia ya Watoto hao kuwekeza imani kwa Serikali na kuisitiri miili ya vichanga hivyo wakati juhudi za kuwapata waliohusika zikiendelea.
“Namuomba sanasana na nashukuru Ndugu wa Baba wote wanaunga mkono Mtoto akazikwe naomba Kijana wetu Isaka akubali kauli ya Ndugu zake na sisi Viongozi wa Mkoa na Wilaya akubali twende tukawasitiri wale viumbe wa Mungu”
"Tunamuhakikishia suala hili tunalichukulia kwa uzito wa hali ya juu ni suala linaufedhehesha Mkoa wetu na linachafua sura ya Mkoa kwamba tunahusishwa sana na masuala ya ushirikina kwahiyo tutahakikisha wale wote waliokuwa mule ndani siku ya tukio kwenye wodi ya Wazazi, awe Mzazi au Msaidizi wa Wazazi na wale Wakunga ikiwemo Mama mzazi wa Watoto wote tutawahoji”.
---
Naitwa Kisaka Mtoisenga, mkazi wa Ushikola, Kaliua, Tabora. Tarehe 9/05/2023 saa 4 usiku mke wangu alijifungua watoto wawili mapacha kituo cha afya Kaliua. Watoto walizaliwa njiti (premature) na miezi 7 lakini tunamshukuru Mungu walizaliwa salama.
Kwa kuwa kituo cha afya Kaliua hakina uwezo wa kuhudumia watoto njiti wakatupa rufaa kwenda hospitali teule ya wilaya (Mission) yenye mashine za kuatamia watoto njiti (Incubators). Kituo hakina gari la wagonjwa, hivyo wakatuambia tukatafute usafiri.
Nikamuacha mke wangu na watoto wakiwa wazima wa afya, nikaenda kutafuta usafiri. Muda huo haikua rahisi kupata gari, nikapata Bajaji. Tulipofika wahuhudu wakasema tusubiri wawaandae watoto. Tukasubiri hadi saa 5 dereva akaanza kulalamika. Wahudumu wakasema tuendelee kusubiri. Ilipofika saa 6 dereva akataka kuondoka. Nikasema akiondoka sitapata Bajaji nyingine usiku huo. Nikawauliza wahudumu wakasema wanamalizia kuwaandaa watoto.
Nimwambia dereva nitamuongezea hela asubiri kidogo. Baadae wahudumu wakatoka na kutuambia bahati mbaya watoto wamefariki. Wakasema watatupa maiti kesho yake asubuhi.
Asubuhi wakatupatia maiti zikiwa ndani ya mabox, kwenye chumba maalumu cha upasuaji, ambacho kina giza. Wakatusisitiza tukazike siku hiyohiyo kwa haraka kwa sababu watoto njiti hawafanyiwi msiba.
Tulipofika nje kabla ya kupanda gari tukafungua mabox. Tukakuta watoto wameng'olewa macho, wamekatwa ulimi na wamechunwa ngozi kwenye paji la uso. Tukahamaki. Tukarudi kuuliza nini kimetokea, hawakutupa majibu ya kuridhisha.
Tukaenda Polisi, lakini wakatuambia tukazike tu maana wao hawashughuliki na ushirikina. Tukaenda kwa Mkuu wa wilaya, alipoona maiti akasema huo ni Ushirikina. Akatushauri tukazike tu maana hata tukienda mahakamani hatuwezi kushinda. Nikamuuliza kwanini ushirikina ufanyike hospitalini? Nikakataa kuzika.
Nikataka uchunguzi ufanyike. DC akaagiza maiti zipelekwe hospitali ya Urambo. Hadi leo zipo huko sijui nini kinaendelea. Naomba unipazie sauti Rais asikie. Watoto wangu wametendewa unyama kwenye kituo cha afya halafu nanyimwa haki kwa kisingizio cha ushirikina? Naumia sana.