Baba wa Taifa akemea udini

Baba wa Taifa akemea udini

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
BABA WA TAIFA AKIKEMEA UDINI

Mjamaa wa kisasa anamnukuu Baba wa Taifa katika suala la udini msome hapo chini:

- Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa Ni kiongozi aliyepiga vita vikali kuhusu ubaguzi wa kidini au kikabila ndani ya taifa letu la Tanzania.

- Baba wa Taifa alihimiza siku zote za uhai wake pawepo mshikamano wenye umoja baina ya WATANZANIA ndani au nje ya Tanzania pasipo kubaguana kwa misingi yoyote ile iwe ukabila au udini

- Kwa kipindi Cha miaka ya hivi karibuni Taifa letu limekubwa na kasumba moja mbaya Sana kuhusu viongozi wanaoteuliwa.kwa watu[wananchi] kutazama zaidi kuhusu dini zao pasipo kutazama UTANZANIA wao waliokuwanao na sifa zao zilizowafanya wachaguliwe

- Ningependa kushauri kwa WATANZANIA wenzangu kutokutazama zaidi udini wa mtu katika teuzi za viongozi bali kuzama zaidi kuhusu sifa za kiongozi aliyetauliwa au kuchaguliwa.

- Ningependa kushauri pia kwa viongozi kuacha kasumba au kutokuwa na kasumba ya kuchagua watu kwa misingi ya dini zao bali wawachague kutokana na sifa zao zilizobora.

- Migogoro mingi ya kidini duniani uanza taratibu kwa vitu vidogo vidogo na mwisho uwa mikubwa zaidi na yenye madhara.

- Hii ni Tanzania ya watu wote wenye dini na wasio na dini.Wote wanastahili kutumikia serikali [ kuchaguliwa/ kuteuliwa]

Mwisho sikiliza kwa makini maneno ya baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akionya kwa ukali kuhusu udini ndani ya taifa letu la Tanzania. kwenye video fupi hapa chini''

Jibu langu kwa Mjamaa wa Kisasa hili hapo chini:

Mjamaa,

Tatizo hili si jepesi kama unavyodhania.

Linataka ujuzi ndilo ulizungumze na linapendeza uwasikie wale walioathirika na udini na kujikuta kila mahali wao hawapo.

Hawa ndiyo wanaujua ukweli.
Ingependeza kama hawa wangepewa nafasi ya kulizungumza tatizo hili.

Nyerere hakupata kukumbwa na tatizo la udini katika maisha yake yote.

Mwalimu kapokelewa na Abdul Sykes 1952 na watu wa mwanzo waliokuwa karibu na yeye wote walikuwa Waislam na wanafahamika kwa majina yao wake kwa waume.

Kaishi na Waislam ndani ya nyumba zao.
Hakubaguliwa si kwa kabila yake wale dini yake.

Kaungwa mkono na wana mji wa Dar es Salaam na viongozi wa Waislam kama Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Suleman Takadir, Mshume Kiyate, Mohamed Jumbe Tambaza, Shariff Abdalah Omar Attas, Iddi Faiz Mafungo, Iddi Tosiri kwa kuwataja wachache.

Majimboni hali ilikuwa ni hii hii kama ilivyokuwa Dar es Salaam.

Lindi aliungwa mkono na Sheikh Mohamed Yusuf Badi na wenzake akina Suleiman Masudi Mnonji.

Tanga aliungwa mkono na Sheikh Abdallah Rashid Sembe na akina Hamisi Heri.

Huko kote Nyerere alishirikishwa katika dua ya kumuombea yeye Mungu na kuomba uhuru.

Nyerere hana historia ya kubaguliwa na Waislam.

Dhifa ya kumuaga safari ya kwanza UNO 1955 ilifanyika katika jengo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.

Nyerere kapata kupambana na tatizo la udini mara tatu.

Mara moja kabla ya uhuru mwaka wa 1958 pale aliposhambuiwa na Shekh Suleiman Takadir Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU.

Mwaka wa 1963 Nyerere alipambana na Bi. Titi Mohamed katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya TANU.

Mwaka huo huo wa 1963 alipambana na Bilal Rehani Waikela katika mkutano wa East African Muslim Welfare Society (EAMWS) Mwalimu akiwa amealikwa kufunga mkutano huo.

Bahati mbaya haya yote hayako katka historia ya TANU na pengine kama nisingeyaeleza yasingefahamika.

Sitaeleza katika hayo matukio matatu nini khasa lilikuwa tatizo kwa kuwa mosi kisa kinatisha na pili nashindwa kueleza kwa ajili ya staha.

Lakini matatizo yote hayo hapo juu nimeyaeleza kwa kirefu katika kitabu cha Abdul Sykes.

Mwalimu hawezi kuwa mtu anaefaa kukemea udini kwa kuwa yeye ni sehemu ya historia hii.

Kwa ajili hii yeye hawezi kuwa hakimu wa hili tatizo.
Hili tatizo waachiwe wengine walisemee.

Ndugu yetu Mjamaa aliyefungua uzi huu anasema, ''Tusikilize kwa makini maneno ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akionya kwa ukali kuhusu udini ndani ya taifa letu la Tanzania.''

Swali kubwa ni kuwa ikiwa hali ilikuwa hivi hapakuwa na udini wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika huu udini anaoukemea Mwalimu Nyerere umetokea wapi na nini sababu na chanzo chake?
 
Leo siku ya Nyerere day katika kumdurusu Mwalimu Nyerere kuna maswali najiuliza Kumuenzi Baba wa Taifa:CCM, Serikali, Viongozi na Watanzania kwa Ujumla, Je Tunamuenzi Baba wa Taifa kwa Mawazo, Maneno na kwa Vitendo?, Tunamuishi?.
Nawatakia maadhimisho mema na mapumziko mema ya Nyerere Day.
P
 
huyu mzee aliona mbali sana et mtu anasherekea kukaa ikulu kwa miaka miwili hv ikulu kuna nini mbona awali haikwepo hii ?
 
Back
Top Bottom