Mantombazane
JF-Expert Member
- Sep 7, 2014
- 579
- 367
Baba wa taifa Mwalimu Nyerere alikuwa ni jasiri sana kuwanyooshea vidole viongozi wazembe na wasiojielewa huku akitumia maneno makali bila woga muda wowote wanapomkera au wanapofanya ndivyo sivyo. Alitumia maneno kama wahuni, wapumbavu, wajinga nk.
Mfano angekuwepo leo angesema bunge letu linaendeshwa kihuni na kwa maana hiyo wanaoendesha chombo hicho ni wahuni kwakuwa hawafuati sheria, taratibu na katiba ya nchi badala yake wanaoongoza kwa matakwa yao kiasi kwamba hata wabunge wasiokuwa na sifa wanaingizwa bungeni na kulipwa pesa nyingi sana za wananchi wanyonge.
Vile vile angekuwepo leo angesema bunge limejaa upambavu na ujinga mwingi hivyo kushindwa kuisimamia serikali vizuri badala yake limegeuka kama jumuiya ya chama tawala au tawi la wakereketwa na kuwa kijiwe cha mipasho isiyokuwa na tija kwa nchi.
Angekuwepo leo angekemea vikali uvunjwaji wa katiba na uhuni uliofanyika wa kuwaingiza bungeni mamluki hivyo kuitia hasara kubwa nchi hii. Sasa kwakuwa hayupo hakuna tena kiongozi mwingine aliyepo au aliyestaafu anayeweza kukemea wendawazimu huo.