Baba wa Taifa na tatizo la Udini

Mkaza...
Tunaweza tukafanya mjadala wa adabu kila mtu akawa anatoa hoja zake.
Lugha za kebehi, ''kulialia,'' mimi nadhani haiendani na mjadala huu.

Wala hapa sijaleta udini.
Nimeweka fikra zangu iweje tukawa na hali hii ya 20:80 baada ya miaka 60 ya uhuru?

Huu si udini.
Udini ni kutumia fursa za nchi kunufaisha jamii moja yenye dini sawa na yako.
 
Ni wazi hawa Wahamiaji wote walisilimu baada ya kuanza kuishi Tanganyika. Ushahidi ni majina yao wakati wanaingia Tanganyika, na haswa huyo Afande Plantan hadi mwanae akaamua kumuita Thomas. Kwa kifupi hayo uliyoeleza hayathibitishi hoja yako kuwa Wazulu walikuwa waumini wa Uislamu huko kwao Uzuluni, bali baada ya kuondoka/kuhama huko Uzuluni na kuanza kuchanganyika na watu wa imani ya Kiislamu.

Kama hukubaliani, tuwekee hapa historia ya Uislam ndani ya himaya ya Uzulu aka Zulu Kingdom/Zululand. Jee, Waarabu waliweza kupenyeza hadi huko na kueneza dini yao?
 
Mzee Said, next time hoja ikikushinda tupotezee na ile picha yako ukinywa chai Paris. Hii inaboa.
 

Mzee Said,

Nayakumbuka mambo matatu kama mifano mnasaba wa uzi hu;

1. Bodi Taifa ya Parole hapa nchini iliteuliwa na Frderick Tluway Sumaye aliyekua Waziri Mkuu wakati wa Urais wa Marehemu Benjamin Mkapa. Sumaye aliteuwa wajumbe wote wa bodi wa imani moja bika kuwepo muislam hata mmoja. Miongoni mwao walikuwepo padri mmoja na mchungaji mmoja

Alipoulizwa kwanini kafanya hivyo akajibu kwa ukali sana kwamba watu waache kupanda mbegu za udini maana hatukukelewa hivyo na Mwalimu Nyerere. Uteuzi uliofanyika ulizingatia merits za walioteuliwa!

Siku chache baadae Marehemu Mzee Mkapa akatengua uteuzi wa bodi nzima na akaagiza iundwe upya kwa kuzingatia uwiano wa kijamii kama maeneo wanapotoka wajumbe na pia uwiano wa imani za watu kwa maana ya dini

2. Professor mmoja wa UDOM aliyekua VC alipata malalamiko kuhusu baadhi ya watu kutotendewa haki kwenye admission. Wakati huo TCU ilikua haijaundwa

Alipoamua kuitisha applications zote akakutana na maajabu! Kuna zaidi ya applicants 350 walikua wameachwa huku wakiwa wame qualify huku kukiwa na idadi ya kutosha kabisa wakiwa wamepata admission wengine wakiwa below cutoff point ya Chuo!!!

Kwa “sudfa” au coincidence wote waliokua wameachwa kwa dhulma walikua na majina ya kiislamu na wote walioku admitted walikua na majina ya kikristo!!! VC akatoa order mchakato urudiwe tena japo jambo hilo lilikua down played

3. Miaka ya karibuni kulikua na zoezi la kuwaondoa waalimu wa masomo ya arts sekondari waajiriwa wa serikali kuwarudisha shule za msingi. Zoezi husika halikuwahusu waalimu wa masomo ya sayansi na hesabu

Nilikua mkoa fulani kipindi zoezi hili linaendelea. Kukatokea malalamiko kua zoezi hilo lina sura ya ubaguzi na waathirika ni Waislamu

Ofisa mmoja Muislamu katika idara ya elimu ambaye hapo awali alikua amejaribu kuomba uhamisho kwenda mkoa mwingine kwa zaidi ya miaka miwili bila mafanikio alipokea malalamiko hayo na baada ya kujiridhisha ni genuine akayapeleka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri.

Kikaitwa kikao kati ya Mkurugenzi, Afisa Elimu, Afisa Elimu Taaluma, Ofisa Utumishi na yule ofisa aliyeipeleka issue kwa Mkurugenzi. Wahusika wote kasoro yule aliyepeleka malalamiko walikua wakristo na ilivyoonekana baada ya kikao kuanza ni kutaka kum pin huyo ofisa kwanini analeta udini kwenye utendaji wa kazi za Halmashauri na hususan hilo zoezi la kitaifa

Walianza kumpa maneno makali kabda hata hawajamuuliza kuhusu ushahidi. Walipomuuliza atoe ushahidi wa madai yake akaoonyesha majina wa wahusika waliohamishwa

Shule ina waalimu 68 kati yao Waislamu 18. Waalimu wanaotakiwa kupelekwa primary schools ni 21. Basi wakaondolewa wale wote 18 wenye majina ya kiislamu na hao wengine 3 wasiokua waislamu

Kikao bado kikasema huo sio ushahidi maana Mkuu wa Kituo(Headmaster) ana discretion ya kuchagua mradi anafata secular iliyotolewa na Wizara(TAMISEMI)

Ndipo akaangusha bomu la atomic ambalo alikua hajawaambia before! Kwamba katika wale waalimu waislamu 18 watatu ni wa Mathematics na sita ni wa masomo mengine ya sayansi na akawaonyesha!

Kikao hakikuendelea. Mkurugenzi akamwambia Afisa Elimu akarekebisehe hilo tatizo

Wiki hiyohiyo yule Afisa akapata barua ya uhamisho aliouomba kwa miaka miwili bila mafanikio!!!!!!!!
 
Sesten...
Ahsante sana ndugu yangu.
Allah akuzidishie.

Hakika umetusomesha vya kutosha.
Alhamdulilah.
 
Mzee Said, next time hoja ikikushinda tupotezee na ile picha yako ukinywa chai Paris. Hii inaboa.
Schmidt,
Hukuridhika na hilo jibu?

Bahati mbaya.
Ndiyo ulimwengu ulivyo kila mtu kapewa uwezo wake wa kuelewa.

Picha hii ya vitabu mimi naipenda sana na sababu yake ni kitu adhim.
Matoleo matatu ya kitabu changu kimoja yakiwa pamoja.

Tafuta kitabu chochote hapa nchini kilichochapwa mfululizo kama hiki changu.
Na tunakimbilia kukichapa kwa mara ya tano.

Ile picha ya Paris inanitia majonzi kwani nilipiga na rafiki yangu marehemu Salim Himid.

Allah alimjàalia akili si ya kawaida.
Anazungumza lugha tano kwa ufasaha.

Alikuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Comoro.

Ilikuwa asubuhi ananifuata hotelini kwangu tunakwenda hapo kunywa chai ya kabab na sambusa.

Nakuwekea picha nyingine ya Paris nilipiga Msikiti Mkuu mwaka wa 1993.

Naamini hutoziona picha hizo ''boring,'' hasa ukiangalia haiba yangu nilipokuwa kijana na nguo zangu nilizokuwa napenda kuvaa.

Nikipenda ''designer'' - Gucci, Yves Saint Laurent, Calvin Klein nk. nk.
Naamini picha hizi zitakufurahisha na kukufikirisha.


Central Mosque, Paris 1993

Salim Himid tuko Railway Station Paris 2011
 
Schmidt,
Hawakusilimu walipoingia Tanganyika enzi hizo German Ostafrika.
Waliingia Waislam.

Wajerumani waliwaweka askari wao katika kambi na walikuwa na hosptali ndani ya kambi ya kuwahudumia wao na famiia zao.

Mama akipelekwa kujifungua mtoto Wajerumani wanamfanyia tasjila na kumpa jina hapo hapo.

Kleist Sykes jina lake ni Abdallah.

Hili Abdallah amepewa na baba yake na Kleist wametoa Wajerumani.

Schneider Plantan jina lake ni Abdillah hii Schneider wametoa Wajerumani.

Hili Abdillah kapewa na baba yake Affande Plantan.

Ramadhani Mashado Plantan jina lake ni Ramadhani hili jina la Mashado kapewa na Wajerumani.

Hivi ndivyo ilivyokuwa.

Mimi nimelijua jina la Kleist kuwa ni Abdallah baada ya kuliona kaburini kwake Kisutu.


Kaburi la Kleist Abdallah Sykes
 
Sesten...
Ahsante sana ndugu yangu.
Allah akuzidishie.

Hakika umetusomesha vya kutosha.
Alhamdulilah.
KUKATOKEA MALALAMIKO KUWA ZOEZI HILO LINA SURA YA UBAGUZI NA WAATHIRIKA NI WAISLAM

Nayakumbuka mambo matatu kama mifano mnasaba wa uzi huu:

1. Bodi Taifa ya Parole hapa nchini iliteuliwa na Frederick Tluway Sumaye aliyekua Waziri Mkuu wakati wa Urais wa Marehemu Benjamin Mkapa.

Sumaye aliteuwa wajumbe wote wa bodi wa imani moja bika kuwepo Muislam hata mmoja.

Miongoni mwao walikuwepo padri mmoja na mchungaji mmoja.

Alipoulizwa kwa nini kafanya hivyo akajibu kwa ukali sana kwamba watu waache kupanda mbegu za udini maana hatukukelewa hivyo na Mwalimu Nyerere.

Uteuzi uliofanyika ulizingatia ''merits,'' za walioteuliwa.

Siku chache baadae Marehemu Mzee Mkapa akatengua uteuzi wa bodi nzima na akaagiza iundwe upya kwa kuzingatia uwiano wa kijamii kama maeneo wanapotoka wajumbe na pia uwiano wa imani za watu kwa maana ya dini.

2. Professor mmoja wa UDOM aliyekua VC alipata malalamiko kuhusu baadhi ya watu kutotendewa haki kwenye ''admission.''

Wakati huo TCU ilikua haijaundwa.

Alipoamua kuitisha ''applications'' zote akakutana na maajabu. Kuna zaidi ya ''applicants'' 350 walikua wameachwa huku wakiwa wame ''qualify'' huku kukiwa na idadi ya kutosha kabisa wakiwa wamepata ''admission'' wengine wakiwa ''below cut-off point'' ya chuo.

Kwa “sudfa” au ''coincidence'' wote waliokua wameachwa kwa dhulma walikua na majina ya Kiislamu na wote walioku ''admitted'' walikua na majina ya Kikristo.

VC akatoa ''order'' mchakato urudiwe tena japo jambo hilo lilikua ''down played.''

3. Miaka ya karibuni kulikua na zoezi la kuwaondoa waalimu wa masomo ya arts sekondari waajiriwa wa serikali kuwarudisha shule za msingi. Zoezi husika halikuwahusu waalimu wa masomo ya sayansi na hesabu

Nilikua mkoa fulani kipindi zoezi hili linaendelea.

Kukatokea malalamiko kua zoezi hilo lina sura ya ubaguzi na waathirika ni Waislamu.

Ofisa mmoja Muislamu katika idara ya elimu ambaye hapo awali alikua amejaribu kuomba uhamisho kwenda mkoa mwingine kwa zaidi ya miaka miwili bila mafanikio alipokea malalamiko hayo na baada ya kujiridhisha ni ''genuine'' akayapeleka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri.

Kikaitwa kikao kati ya Mkurugenzi, Afisa Elimu, Afisa Elimu Taaluma, Ofisa Utumishi na yule ofisa aliyeipeleka ''issue'' kwa Mkurugenzi.

Wahusika wote kasoro yule aliyepeleka malalamiko walikua Wakristo na ilivyoonekana baada ya kikao kuanza ni kutaka kum ''pin'' huyo ofisa kwa nini analeta udini kwenye utendaji wa kazi za Halmashauri na hususan hilo zoezi la kitaifa.

Walianza kumpa maneno makali kabda hata hawajamuuliza kuhusu ushahidi.
Walipomuuliza atoe ushahidi wa madai yake akaoonyesha majina wa wahusika waliohamishwa.

Shule ina waalimu 68 kati yao Waislamu 18.
Waalimu wanaotakiwa kupelekwa primary schools ni 21.

Basi wakaondolewa wale wote 18 wenye majina ya Kiislamu na hao wengine 3 wasiokua Waislamu.

Kikao bado kikasema huo sio ushahidi maana Mkuu wa Kituo (Headmaster) ana ''discretion'' ya kuchagua mradi anafata ''secular'' iliyotolewa na Wizara (TAMISEMI).

Ndipo akaangusha bomu la''Atomic'' ambalo alikua hajawaambia ''before. Kwamba katika wale waalimu Waislamu 18 watatu ni wa Mathematics na sita ni wa masomo mengine ya sayansi na akawaonyesha.

Kikao hakikuendelea.
Mkurugenzi akamwambia Afisa Elimu akarekebishe hilo tatizo.

Wiki hiyo hiyo yule Afisa akapata barua ya uhamisho aliouomba kwa miaka miwili bila mafanikio.
 
Ukweli ni kwamba hawa wakristo kamwe hawawezi kuusema ukweli,na wala hawatokuwa tayari kukiri uozo huu kwa sababu wao ndiyo wanufaika wa mfumo.
Muhimu ni sisi kusimama na kuendelea kuweka bayana ubovu huu bila ya kujali kejeri zao na matusi yao.
 
Belo,
Tunaweza tukafanya mjadala wa adabu na heshima bila ya kejeli na kebehi.

Mathalan ukishanisoma na ukaona kuna jambo una fikra tofauti na zangu ukaeleza.

Sasa hii "kulia," na maneno ya kukashifiana yanatoa ladha ya mjadala.

Shikamoo Mzee Mohamed Said. Huwa nikipata nafasi napitia baadhi ya mada zako. Mzee niseme tu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania idadi ya wanaojiita "Wakristo" ama "Waislam" imekuwa ikiongezeka kila uchwao ijapo "Uadilifu" na "uaminifu vinazidi kupungua kwenye jamii. Mzee Mohamed Said nadhani tungeongeza bidii katika madhabuhu kuongeza idadi ya watu wenye hofu ya Mungu na sio wanaojiita wajina fulani. Mzee Mohamed Said hizi juhudi ya kuwasemea watu wanaojiita majina fulani hazitasaidia taifa letu kabisa, "Nchi yetu inahitaji watu wenye Utu, Ubinadamu, Uadilifu na hofu ya Mungu na sio wa Dini fulani"

Natumaini sijakukwaza

Ahsante
 
Mzalendo...
Hujafanya jambo ovu.
Sote tuko katika juhudi ya kutafuta haki kwa kila mwananchi.

Sote tuna fikra zetu tunazoamini zitasaidia kuwa na jamii yenye amani na upendo baina ya watu.
 
H

Heshima yako Mkuu Mohamed Said. Mwaka wa 1976 au 77 nilipokuwa sekondari tulisoma kitabu " Kiu" kilichoandikwa na mtu mwenye jina la Mohamed Said, je huyu mtu ni wewe? Natanguliza Shukrani zangu

Huyo Mohamed Said alieandika kitabu cha KIU nahisi ni yule wa Zenj AL maaruf kama Bwana MSA
 
Udini ktk Taifa huru Tz,halikuja kwa bahati mbaya,Bali kulikuwA na mpango mkakati kabla ya Uhuru.Wewe jiulize imekuwaje huyu mtoto wa chifu wa wazanaki,kutaka kupewa na kuitwa MTAKATIFU na kanisa la Warumi,Kuna Mambo gani kawafanyia Warumi wa Tanganyika ,mpaka akapewa daraja la Mwenyeheri?
 
Ksk,
Nilikuwa msaidizi wa Dr. Harith Ghassany wakati anatafiti historia ya mapinduzi ya Zanzibar.

Kwa njia moja nimesaidia katika kufahamika kwa historia ya Zanzibar.

Nakushauri uisome historia ya Zanzibar vizuri kwanza kabla hujataka kuijadili.
Ghassany kaandika kwenye angle ya udini kama wewe.Wewe na huyo ni wafia dini.
 
Ghassany kaandika kwenye angle ya udini kama wewe.Wewe na huyo ni wafia dini.
Luku...
Tujaalie Dr. Ghassany kaandika chembelecho kwa ''angle,'' ya dini.

Kwani hairuhusiwi kuandika historia kwa mtazamo wa dini?

Mimi na Dr. Ghassany si tu ni wafia Uislam bali ni marafiki wakubwa na tunakubaliana katika mengi.

Alipokuwa anatafiti kitabu chake, ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru,'' alikua na dua yake akipenda kuisoma: ''Mwenyezi Mungu ikiwa kitabu hiki kitasababisha fitna baina ya Wazanzibari usikijaalie kitoke lakini ikiwa kitaleta mapatano baina ya Wanzazibari jaalia kichapwe.''

Mimi nilikuwa naitika, ''Amin.''


Na Dr. Ghassany, Muscat, 2015.
 

Hii ni post ya kijinga sana , Mods poat kama hizi mnazipaje airtime ?
 
Ukweli ni kwamba hawa wakristo kamwe hawawezi kuusema ukweli,na wala hawatokuwa tayari kukiri uozo huu kwa sababu wao ndiyo wanufaika wa mfumo.
Muhimu ni sisi kusimama na kuendelea kuweka bayana ubovu huu bila ya kujali kejeri zao na matusi yao.
King...
Nimeona baada ya Sesten kuweka ushahidi ule wa yanayofanyika na watendaji wa serikali dhidi ya Waislam ukumbi umekuwa kimya sana.

Nimerusha ule ushahidi wake na umesomwa kwa kupasiana na umewafikia watu wengi.
Hili sikutegemea.

Nimehamasika na nimeingia Maktaba kutafuta yale ambayo yanafanana na aliyotueleza Sesten.

Hebu someni kisa kingine hicho hapo chini:


Mwalimu Athmani Khalfan Mrindoko Mwalimu wa Shule ya Msingi

Mwalimu Athmani Khalfani Mrindoko Mwalimu wa Shule ya Msingi Lwande Handeni Kosa Lake Kusomesha Wanafunzi Qur'an na Kukataa Kuchakachua Mitihani

Mwalimu Athmani Khalfani Mrindoko alikuwa mwalimu wa shule ya msingi Lwande moja ya vijiji ambavyo mwaka wa 2013 vilivyoshambuliwa kwa tuhuma za ugaidi.

Mwalimu Athmani alikuwa mwalimu mwajiriwa na serikali kusomesha masomo ya kisekula lakini kwa mapenzi yake katika Uislam kwa kuwa walimu wa somo la dini ya Kiislam Shule za Msingi hakuna yeye alijitolea kuwasomesha wanafunzi hawa dini ya Kiislam na kuwatungia mitihani.

Kisa chake ni kisa cha kusikititisha na kuhuzunisha.

Siku za nyuma Mwalimu Athmani alifatwa na walimu wenzake akaelezwa kuwa imetoka amri juu kuwa walimu washirikiane kuwafaulisha watoto darasa la saba kwa kuwakokotolea wanafunzi majibu ya mtihani wa mwisho wa darasa la saba ili kunyanyua ufaulu wa shule na hatimaye wilaya.

Mwalimu Athmani akakataa hili kwa misingi ya Uislam kuwa hicho kitendo ni ghushi yaani udanganyifu.

Akawaeleza kuwa imani ya dini yake inakataza mambo kama hayo.
Udanganyifu huu ukakwama na sababu ikawa ni yeye Mwalimu Athmani.

Hapa ndipo zilipoanza chuki dhidi yake.

Sasa lilipotokea sakata la Lwande askari waliovamia kijiji kwa madai ya kupambana na Al Shabab Mwalimu Athmani akakamatwa, kupigwa na kufunguliwa kesi ya kujeruhi Mahakama ya Handeni.

Mwalimu Athmani sasa hivi ni masikini.

Alipoachiwa gerezani kwa dhamana alikuta nyumba yake imevunjwa na vitu vyake vyote vimeibiwa.

Huyu ndiye ''gaidi'' anaesemekana alikuwa akishirikiana na Al Shabab.
Hapakuwa na ushahidi wa ugaidi hivyo akaachiwa na kazi akaachishwa.

Mwalimu muadilifu anaesomesha watoto kitabu cha Allah na kuwafunza maadili mema kwa mfano, Mwalimu Athmani Khalfan Mrindoko akazuliwa kuwa ni ''Al Shabab,'' bila ya ushahidi.

Haya ni machache.
Yapo mengi katika dhulma hii ya kumfanya mtu akabubujikwa na machozi.

Sasa imepita karibu miaka 9 sijapata taarifa za Mwalimu Mrindoko.
 
Hii ni post ya kijinga sana , Mods poat kama hizi mnazipaje airtime ?
Island,
Hii barza inahita stahamala.

Kile unachoona wewe ni ujinga mwenzio anakiona ndiyo ujanja wenyewe.

Tabu sana kwenye wengi ukapata kile tu kinachokufurahisha wewe.

Nini hapa kimekukera?

Uchambuzi wangu wa hotuba ya Nyerere?

Ngoja nikufahamishe.

Huu ujuzi nilionao kuhusu historia ya uhuru wa Tanganyika kiasi cha kupambanua ilivyokuwa ndiyo ulioninyanyua na kuweza kusomwa na watu wengi wewe ukiwa mmoja wapo.
 
Huyu ni mhalifu tu kama vibaka wengine. A criminal and a felon.
 
Huyu ni mhalifu tu kama vibaka wengine. A criminal and a felon.
SAKATA LA KILINDI NA MAUAJI YA KILINDI NA MAUAJI YA KIJIJI CHA MADINA - HANDENI, KUPOTEA (KUULIWA) KWA RAJAB OMARI MTANA

Rajab Omar Mtana alikuwa ni mwanakijiji wa kawaida tu akiishi kijijini Lulago, Handeni kama wanavijiji wengine wanavyoishi na alikuwa na biashara yake kuuza hiliki kama mkulima wa zao hilo.

Siku moja akaja mnunuzi mfanyabiashara ya hiliki nyumbani kwake kununua hiliki na akamuuzia.

Yule mfanyabiashara alipokuwa anatoka na gari yake akasimama kwenye kizuizi cha kulipia ushuru.

Alipotakiwa kulipa ushuru akasema kuwa si hiliki yote amenunua katika kijiji hicho kwa hiyo hawezi kulipa ushuru wa hiliki yote.

Hapo palitokea ubishi na mfanyabiashara yule akagonga lile geti na akaondoka.

Hii ikapelekea kwa wakusanyi ushuru kwenda nyumbani kwa Rajab Omar Mtana kumkamata na kumweka chini ya ulinzi katika ofisi ya serikali ya kijiji hadi hapoatakapolipa ushuru ambao yule mfanyabiashara alitakiwa alipe.

Ndugu zake Rajab Omar Mtana wakenda pale ofisini kwa nia ya kumtoa ndugu yao na hapo pakatokea vurugu na mapigano.

Katika mapigano hayo, mgambo ambae ndiye aliyekuwa akishughulika na kudai ushuru akauawa.

Kisa hiki cha ushuru wa hiliki ndicho kilichozua balaa kubwa la mauaji na uchomwaji moto nyumba za Waislam wa Madina na kuvunjwa kwa misikiti na vijiji ambavyo vilikuwana idadi kubwa ya wakazi wake Waislam.

Baada ya haya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Chiku Galawa akatoa amri kuwa hapana ruhusa tena ya sehemu ile kuwa makazi kwa kisingizio kuwa hizo ni kambi za ugaidi.

Huyu bibi alisema mengi ambayo takriban yote yamedhihirika kuwa hayana ukweli mathalan kuwa kuna Al Shabab, mahandaki ya vita, silaha za kutungulia ndege nk. nk.

Alizungumza na Radio Nuur, Tanga nami nilikwenda hadi Radio kuomba nipatiwe hayo mazungumzo yake lakini Radio Nuur waliogopa kunipa juu ya kuwaeleza kuwa Bi. Chiku kazungumza radioni kwa hiyo kazungumza na dunia nzima.

Hawakuthubutu kunipa lakini nilizungumza na watu waliomsikia.

Katika Waislam waliokamatwa na kufunguliwa mashtaka mahakamani Handeni ni huyu kijana Rajab Omari Mtana.

Baada ya kukaa rumande alipata dhamana yeye pamoja na wenzake na akawa nje.

Mwezi uliopita Rajab Omar Mtana alirejea kijijini kwake.

Wakati anakaribia kuingia kijijini alisimamishwa na askari wa kijiji akapekuliwa na akanyang'anywa simu yake na fedha taslimu.

Baada ya mkasa huu walimwachia na yeye akaendelea na safari yake.
Lakini nyumba yake ilikuwa imevurugwa haifai kuishi mtu kwa hiyo alifikia kwa dada yake.

Akiwa nyumbani kwa dada yake alifatwa na watu wa serikali ya kijiji usiku akatolewa ndani na kuanza kupigwa kwa bakora na kisha kwa mapanga.

Kujitetea kijana huyu alikimbia huku akifukuzwa.
Asubuhi kulipokucha palionekana damu nyingi sana.

Taarifa ilitolewa polisi lakini hakuna kilichofanyika.

Polisi walitoa taarifa (SON/RB346/2014).

Dada yake na mumewe walikamatwa na kushitakiwa katika ''mahakama'' ya hapo kijijini na wakapigwa faini ya kila mtu shs. 20.000.

Kosa lao ni kumleta kijijini mtu asiyetakiwa.

Sasa ni mwezi mmoja Rajab Omar Mtana hajulikani alipo na inasadikiwa ameuawa na wale waliokuja kumtoa nyumbani kwa dada yake.

Ndugu yetu Rajab ametafutwa kote hadi leo hajapatikana na waliompiga na kumjeruhi wako huru nje hawajaguswa wala kuhojiwa na polisi.

Wakati Sheikh Chambuso alipokuwa akinihadithia mkasa huu ilinijia picha ya kisa cha vijana watatu waliouliwa na Klu Klux Klan Mississippi katika miaka wa 1960 wakati wa ubaguzi wa rangi Marekani.

Waliuliwa kama vile mtu kauwa paka msumbufu na hakuna lolote lililofanyika hadi zilipotiwa juhudi za ziada kutoka nje ya Mississippi ndipo wauaji wakatiwa mbaroni.

Mauaji ya Madina yamepita hivi hivi hakuna aliyesimamishwa mbele ya vyombo vya dola.

Uwezekano mkubwa ni kuwa na mauaji haya yatafata mkondo ule ule. Jambo la kusikitisha ni kuwa mauaji haya yamelenga watu wa dini moja.

Je, viongozi wetu wako hadhiri na mbegu hii wanayoiacha imee?

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…