Baba wa Taifa na tatizo la Udini

Baba wa Taifa na tatizo la Udini

Political marginalization means that some groups of people are not able to PARTICIPATE democratically in the DECISIONS MAKING PROCESS
If you dont have a seat at the DECISIONS MAKING table it is very hard to get your voice HEARD
 
Mkuu una uwezo mkubwa ktk kujenga hoja,hapo nakupa saluti kuubwa.Ushauri wangu jikite kwenye weledi achana na mambo ya kuangalia ktk mitizamo ya kidini.Unakoelekea sasa utaanza kuhoji hata timu ya taifa ina waislam wangapi badala ya kuangalia uwezo,maadili,maarifa...Kama ulivyonishauri niachane na mambo ya Misri basi hebu nawe jiulize ni wakristo wangapi waliopo serikalini kwenye teuzi SMZ?Kwani uliambiwa teuzi zinafanyika ktk misingi ya uwiano kidini?Mbona hujawai kuhoji kwanini waislam wana vyuo na shule chache?
Sijui kama amekuelewa.

Sent from my TECNO CD7 using JamiiForums mobile app
 
Ukishasikiliza mazungumzo ya Mwalimu Nyerere katika hiyo video hapo juu sasa soma Hotuba yake aliyotoa Bungeni tarehe 10 Desemba, wakati Tanganyika inakua jamuhuri mwaka wa 1962.

Hotuba ya Nyerere ilijikita kwenye matatizo ya upogo kati ya Waislam na Wakristo.

Kwa nini ilikuwa lazima Mwalimu awataje Waislam katika hotuba ile?

Sababu ni jinsi Waislam walivyokuwa mstari wa mbele katika kupambana na ukoloni na namna walivyounda TANU wakamchagua kama kiongozi na kuumuunga mkono toka siku alipochukua uongozi wa TAA katika uchaguzi wa tarehe 17 April, 1953 Ukumbi wa Arnautoglo alipogombea nafasi ya urais dhidi ya Abdul Sykes aliyekuwa Act. President na Secretary wa TAA.

Kwa bahati mbaya sana hii ni historia ambayo ilifunikwa na hakuna yeyote aliyekuwa anaijua hadi nilipoandika kitabu cha Abdul Sykes na kuchapwa mwaka wa 1998.

Mwalimu anasema katika hotuba yake ya Jamhuri ndani ya Bunge la Tanganyika:

''Hakuna njia nyepesi ya kuondoa tafauti baina ya raia wetu Waafrika na wasio Waafrika; hakuna njia nyepesi ya kuondoa tofauti za elimu kati ya Wakristo na Waislam, au baina ya wachache wenye elimu na wengi wa watu wetu wasio kuwa na elimu; hakuna njia nyepesi ambayo Wamasai na Wagogo wanaweza wakalingana na Wahaya na Wachagga na Wanyakyusa.''

Hii ilikuwa kauli ya serikali ya kudhihirisha nia yake njema ya kupigania haki na usawa kwa raia wote wa Tanganyika.

Kauli hii ilikuwa ya kuwapa matumaini na kuwahakikishia Waislam na wale wote walioathirika na dhulma ya wakoloni, kuwa serikali ilikuwa inatambua shida zao na itachukua hatua zifaazo kurekebisha hali hiyo.

Tarehe 5 Novemba, 1985 wakati Mwalimu anastaafu urais, Mwalimu aliwahutubia wazee wa Dar es Salaam.

Hotuba hii ilijaa simanzi, Nyerere akikumbuka jinsi Waislam walivyompokea Dar es Salaam kwa mapenzi makubwa ingawa yeye alikuwa Mkristo.

Katika hotuba hii Nyerere kwa mar ya kwanza hadharani alimtaja Abdul Sykes.

Mwalimu alimtaja na mdogo wake Abdul, Abbas Sykes na Dossa Aziz.

Wazee hawa aliokuwa anawahutubia wengi wao walikuwa wanachama wa zamani wa TANU waliomuunga mkono wakati wa kudai uhuru.

Nyerere aliusifia mchango wa Waislam katika kipindi kile kigumu cha kudai uhuru.

Nyerere alisema neno zito sana kuwa upogo katika elimu uliorithiwa na serikali yake kutoka kwa Waingereza baina ya Waislam na Wakristo yeye ameuondosha katika kipindi cha utawala wake:

''Waislam wametupa nafasi kupitia sera yetu ya elimu, kurekebisha upogo.

Sasa nipo katika hali ya kufarahisha kwa kuwa wakati mwingine sielewi kama Mbunge mpya, Waziri, au Katibu Mkuu katika wizara zetu za serikali, ni Muislam au Mkristo au hana dini labda pale jina lake la kwanza linapotoa utambulisho.

Na hata hivyo hiyo siyo njia ya kuaminika kutoa utambulisho wa dini kwa kuwa tuna Wakristo wenye majina ya Kiislam, na Waislam wenye majina ya Kikristo.

Kuvumiliana huku nyie ndiyo sababu; nilichofanya mimi ni kuzungumzia maadili haya kwa niaba yenu.''

Swali linalokuja hapa ni kuwa ikiwa Mwalimu alisharekebisha upogo huu baina ya Waislam na Wakristo haya malalamiko ya leo kutoka kwa Waislam kuwa wanabaguliwa tunauelezaje?

Waislam hawasemi kweli?

Mgawano wa madaraka ndani ya serikali ya Tanzania baina ya Waislam na Wakristo ni 20:80.

Tumefikaje katika hali hii?

Ni muhimu sana mtu anapotaka kujadili tatizo hili la udini muhimu akaangalia historia hii kwanza kama nilivyoieleza hapo juu kwa kusikiliza mazungumza ya Mwalimu kuhusu udini na kusoma Hotuba yake ya Jamhuri ndani ya Bunge la Tanganyika mwaka wa 1962.

Tatizo hili la udini nimelijadili kwa kirefu sana katika kitabu cha Abdul Sykes.

Tatizo hili si tatizo la kupuuzwa na wala si la leo.

Tatizo hili lilianza mwaka wa 1958 na likasababisha ugomvi mkubwa baina ya Sheikh Suleiman Takadir na Julius Nyerere na Sheikh Suleiman Takadir akafukuzwa TANU.

View attachment 2096477
View attachment 2096478

Pep,
Mwalimu angeacha misingi mizuri leo tusingejikuta kwanza tunaandika upya historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Pili tusingekuwa na mjadala huu uliotukutanisha hapa.
Mwalimu angekua mdini asingerihusu mwinyi ambaye ni muislamu kuwa rais, ukweli ni kwamba mama sio Nyerere kuondoa utofauti wa makabila na udini Leo hii nchi ingekua kama Nigeria ambayo udini ni tatizo kubwa au Kenya ambao ukabila ni tatizo
 
Kwani mkuu si kazi zinatangazwa watu wanaomba na wanafanyiwa usahili ama ni hizi za kuteuliwa.
Yaani hata Kama wamefaulu wote waislamu wachukuliwe ,mana kigezo sio dini kukaa pale.
Mwishowe tutakuja mpaka darasani tutaanza kuona ratio ni ndogo so itabidi wawe wanabebwa kisa wao wapo wachache.
Kama vipi tuanze kucheki kila kabila liwe katika kila ofisi mkuu.
Tukikuta watu wame qualify hata watano Kati ya 20 position afu wote ni wamwera watolewe wawekwe wamang'ati ama wabarbaig
Hata kwenye interview na shuleni unapewa namba yaan hutumii jina huo ubaguzi anaouongolea ukoje
 
Mwalimu angekua mdini asingerihusu mwinyi ambaye ni muislamu kuwa rais, ukweli ni kwamba mama sio Nyerere kuondoa utofauti wa makabila na udini Leo hii nchi ingekua kama Nigeria ambayo udini ni tatizo kubwa au Kenya ambao ukabila ni tatizo
Science...
Unazungumza na mtu ambaye somo hili analijua vyema na ameandika vitabu kadhaa pamoja na historia ya kweli ya uhuru wa Tanganyika.

Mimi naona vibaya naona haya kuyaandika yale ambayo nayafahamu.

Tuachilie mbali habari hii lakini ikiwa wewe unataka kujua ambayo huenda huyajui ingia kwenye link hii na fanya name search: mohamedsaidsalum.blogspot.com.
 
Imeloa,
Kilipotoka kitabu cha Abdul Sykes mwaka wa 1998 kila aliyekisoma alishangazwa na aliyoyakuta ndani.

Kitabu kimependwa sana kwani watu walikuwa wanaisoma upya historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.
Mzee nimekutafuta Sana hatimae nimekupata
 
Sihitaji kukujua kwasababu hujawahi kuwa na Jambo lolote la maana, hate wewe mwenyewe unajua.

Ndio maana unachochea watu huku wewe uko nyuma.
Na mada zake humu ukiziona wa kwanza wewe kuzisoma.

Wewe upo hapa kuchochewa au kuchochea?
 
Shikamoo Mzee Said. Hongera kwa uandishi wako kwa njia ya vitabu na makala.

Hongera pia kwa kutetea usawa katika jamii.

Mzee Said nimekuwa mfanyakazi wa umma sehemu mbalimbali, kiukweli sijawahi ona sehemu ambayo ilifanyika makusudi na viongozi au sekretariati ya ajira kutoajiri mtu kwa sababu ya dini yake. Kikubwa ni sifa ya mtu wala sio dini. Ungesema kabila na ukanda hapo tungekuelewa kidogo maana kuna baadhi ya taasisi huko nyuma (sio enzi hizi za sekretariati ya ajira) zilijaa watu wa kabila au kanda fulani.

Udini kidogo umeanza kurise kuanzia 2000s tena kwa baadhi ya taasisi.

Huko nyuma ni kweli kulikuwa na gap kubwa kati ya mkristo na muislamu (sababu kubwa ilikuwa elimu, kuna upande uliwekeza zaidi elimu ya dini kuliko elimu dunia), ila kwa sasa wengi wa vijana na watoto wa kitanzania wamesoma bila kujali dini wala kabila....hata jamii za waokota matunda na mizizi pamoja na wafugaji wako wengi kwenye mfumo wa elimu na ajira.

Hivyo, Mzee wangu tambua hilo gap la elimu lilivyokuwa huko nyuma ukizingatia taasisi nyingi za elimu zilikuwa chini ya dini fulani.
Elimu ya dini ni ipi na elimu ya dunia ni ipi?
 
Mkoloni hakuona kuwa muislamu au mwarabu hakuona huyu mkristu aliona wote waafrika weusi .
Sisi ndio tumechanganyikiwa tunaangalia kwa dini. Hamna sehemu walienda kugombea uhuru kuwa uhuru wapewe waislamu au uhuru wapewe wakristu . Uhuru uliombwa wapewe waafrika watanganyika.

Mtu mzima kuingiza dini katika mazungumzo ya waafrika kuhusu kuendesha nchi ni kuchanganyikiwa

nampongeza sana baba wataifa kuliona hili na kulizuia ila bado majinga yanachochea dini ukabila.

tuache ujinga ndugu zangu watanzania
Nahisi kamma umejazwa ujinga na umekujaa.

Mkoloni ni nani?

Mwarabu ni rangi gani?
 
Mkoloni alikutawala kwasababu ulikua muislamu au mwafrika ..waarabu walichukua watumwa hapa tanzania kwasababu walikua wakristu au waafrika.

kulilia dini za watu ni kuchanganyikiwa
Unaelewa maana ya neno "dini" au unabwabwaja tu?

Mwafrika ni nani?

Unavyoandika hueleweki eleweki.
 
Naomba urudi kwa madarasa ya watoto ya dini yako, mwalimu wako atakujuza iwe padri/katekista au Sheikhe
Mwalim wangu kanifundisha vya kutosha, sana tena sana. Nna-mashaka kuwa wewe shule ulienda kusomea ujinga.

Unavyoandika unaonesha wazi kuwa huelewi maana ya neno "dini" ni nini. Kama unaelewa, eleza maana ya neno "dini" ni ipi?
 
Science...
Unazungumza na mtu ambaye somo hili analijua vyema na ameandika vitabu kadhaa pamoja na historia ya kweli ya uhuru wa Tanganyika.

Mimi naona vibaya naona haya kuyaandika yale ambayo nayafahamu.

Tuachilie mbali habari hii lakini ikiwa wewe unataka kujua ambayo huenda huyajui ingia kwenye link hii na fanya name search: mohamedsaidsalum.blogspot.com.
Link kivip nawakati mwenye macho aambiwi tazama, kama Tanzania ingekua na udini mwinyi, kikwete na Samia wasingekua maraisi
 
Link kivip nawakati mwenye macho aambiwi tazama, kama Tanzania ingekua na udini mwinyi, kikwete na Samia wasingekua maraisi
Science...
Kama unayaamini macho yako basi yatakuonyesha kitu hapo chini:

PUBLICATIONS/RESEARCH PAPERS/ARTICLES

The Life and Times of Abdulwahid Sykes 1924 –1968 The Untold Story of the Muslim Struggle against British Colonialism in Tanganyika, Minerva Press London, 1998 translated into Kiswahili as Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes 1924-1968 Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza, Phoenix Publishers, Nairobi, 2002.

The Torch on Kilimanjaro, Oxford University Press, Nairobi, 2006

Contributing author for an African anthology: The Mermaid of Msambweni and Other Stories, Oxford University Press 2007, Nairobi.

Contributing author Dictionary of African Biography (DAB), Oxford University Press 2011, New York.

Uamuzi wa Busara, Abantu Publications 2008, Dar es Salaam.

Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika No. 1, Ibn Hazm Media Centre, 2018, Dar es Salaam.

Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika No.2, Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaam

Dar es Salaam na Wazalendo Wake Mashujaa Katika Kupigani Uhuru wa Tanganyika Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaaam

Watu Mashuhuri Katika Kuulingania Uislam Tanzania, Sheikh Ilunga, Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaam

Dola, Kanisa na Tatizo la Udini Tanzania, Ibn Hazm Media Centre, 2018, Dar es Salaam

The School Trip to Zanzibar, Africa Proper Education Network 2020, Dar es Salaam

Rajabu Ibrahim Kirama, Jemadari wa Vita Kuwa Jemadari wa Uislam, Readit, 2020, Dar es Salaam

In Praise of Ancestors (1987) Africa Events (London).

Abdulwahid Sykes: Founder of Political Movement (1988) Africa Events (London).

Islam and Politics in Tanzania (1989) Al Haq International (Karachi)

The Plight of Tanzanian Muslim (1993) Change (Dar es Salaam).

Tanzania - The "Secular" Unsecular State (1995) Change (Dar es Salaam).

The Question of Muslim Stagnation in Education in Tanzania - A Muslim Riddle (Paper presented at the Conference of the Global World of the Swahili Intercultural Dialogue on the Indian Ocean Zanzibar, February 20 - 23, 2003).

Islamic Education and Intellectualism in Eastern Africa ‘Themes from the Pulpit in Tanganyika (Tanzania Mainland) 1800 – 2000’ (Paper presented at International Symposium on Islamic Civilisation in Eastern Africa Kampala, Uganda organised by the Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA), Istanbul and the Islamic University in Uganda, Mbale December 15th – 17th 2003).

Sheikh Hassan bin Ameir - The Moving Spirit of Muslim Emancipation in Tanganyika (1950 – 1968) (Paper presented at Youth Camp Organised by Zanzibar University, World Assembly of Muslim Youth (WAMY) and Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) 27th February – 4th March 2004).

Islamic Movement and the Christian Lobby in Tanzania - the Experience of the late Prof. Kighoma Ali Malima (1938 – 1995) (Paper Presented to Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) Sokoine University of Agriculture (SUA) Morogoro 11th April 2004).

Terrorism in East Africa the Tanzanian Experience (Paper Presented at the Conference on Islam, Terrorism and African Development University of Ibadan, Nigeria 8th - 10th February 2006).

Al Marhum Sheikh Kassim bin Juma bin Khamis (1940 – 1994) and the Pork Riots of 1993. (Paper Presented at the Regional Conference on Islam in Eastern Africa: Islam Encounter with the Challenges of the 21st Century 1st - 3rd August 2006, Kenyatta University, Nairobi.

Muslim Bible Scholars of Tanzania – The Legacy of Sheikh Ahmed Deedat (1918 – 2005) Paper Presented at the International Symposium on Islamic Civilisation in Southern Africa Organised by The Organisation of Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA) The National AWQAF Foundation of South Africa (AWQAF SA 1 – 3 September 2006 University of Johannesburg.

Tanzania: A Nation Without Heroes Seminar Organised by IFRA French Institute for Research in Africa and BIEA British Institute in East Africa 23rd and 24th September 2013 at IFRA Nairobi.

Awards: Several Awards

Visiting Scholar: (2011)

University of Iowa, Iowa City, USA

Northwestern University, Chicago, Illinois, USA

Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin.

OTHER COUNTRIES VISITED

Zambia, Ethiopia, Great Britain, Swaziland, Msumbiji, Zimbabwe, Zambia, Sudan, Egypt, Saudi Arabia, United Arab Emirates, Oman, Yemen, Uganda, Switzerland, Iran, France, Netherlands, Turkey and Abu Dhabi.
 
kwa CV hii kuipata inaweza kumchkua mtu angalao miaka 30

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
 
Mwalim wangu kanifundisha vya kutosha, sana tena sana. Nna-mashaka kuwa wewe shule ulienda kusomea ujinga.

Unavyoandika unaonesha wazi kuwa huelewi maana ya neno "dini" ni nini. Kama unaelewa, eleza maana ya neno "dini" ni ipi?

Neno "ujinga" limekukaa na ni mwepesi sana kuona wenzio wajinga. Haya wewe uliye mwerevu tupe somo, maana kusomea "ujinga" kunahalalisha kuona wengine ni uzuzu!!
 
Hapa hapa jf nlitoa mada ya kukujadili na kujadili mada zako nkataman ufike ufafanue wewe ni Nan na kwann unaandika hzo mada .
Waziri...
Sijakuelewa.

Mimi ni nani hapa niko nimejitambulisha kwa jina langu halisi na picha na videos zangu naweka.

Watu wananifahamu kwa majina, sura na sauti.

Niko JF kwa zaidi ya miaka 10 na nimefikia hadi kupewa tuzo kwa michango yangu.

Wewe nani mwenzangu?
 
Back
Top Bottom