Baba wa Taifa na tatizo la Udini

Belo,
Tunaweza tukafanya mjadala wa adabu na heshima bila ya kejeli na kebehi.

Mathalan ukishanisoma na ukaona kuna jambo una fikra tofauti na zangu ukaeleza.

Sasa hii "kulia," na maneno ya kukashifiana yanatoa ladha ya mjadala.
Mwalimu was a genious
 
Pep,
Nakuhakikishia hutajuta.

Niulize swali lolote kuhusu harakati za uhuru kuanzia 1929 wazee wangu walipounda African Association hadi uhuru 1961 na changamoto zlizotokea kupelekea wazee wangu wote kufutwa katika historia hii.
Una hati miliki ya historia ya Uhuru wa Tanganyika?Kwa nini unataka kutuaminisha wewe kuwa unayoyasema kuhusu mada za uhuru wa Tanganyika ni kweli peke yake.Wewe peke yako ndo unafanya tafiti?Wewe peke yako ndo unaandika paper?Wasomi.wote wa historia nchi hii hawajui kitu isipokuwa wewe?Una hati miliki ya ukweli?
 
Una kazi
 
Nan...
Hapana sina hati miliki ya historia ya uhuru wa Tanganyika.

Nilichonacho mie ni ujamaa na wengine nasaba na baadhi ya wapigania uhuru wa Tanganyika.

Mathalan Mzee Kleist, Mzee bin Sudi, Ali Jumbe Kiro, Mzee Iddi Tosiri, Mzee Iddi Faiz Mafongo kwa kuwataja wachache ni babu zangu katika ujamaa na katika Umanyema ukimtoa Mzee Kleist.

Salum Abdallah mmoja katika waasisi wa TANU Tabora ni babu yangu khalis.

Mimi ni Mohamed Said Salum Abdallah mjukuu wa Salum Abdallah aliyeongoza migomo mitatu mikubwa ya Tanganyika Railways 1947, 1949 na 1960 miezi michache kabla ya Tanganyika kukabidhiwa madaraka ya ndani.

Mwaka wa 1954 akawa mmoja wa waasisi wa TANU na 1955 pamoja na Kassanga Tumbo wakaasisi Tanganyika Railways African Union (TRAU).

Mgomo huu wa mwaka 1960 ulidumu siku 82 na kuvunja rekodi ya mgomo wa siku 62 ulioitishwa na Makhan Singh, Kenya.

Kuhusu ukweli wa historia ya uhuru wa Tanganyika ambao upo katika kitabu cha Abdul Sykes sikuwa na sababu ya kuandika uongo.

Hawa ndiyo wazee wangu nilioeleza mchango wao katika kupigania uhuru.

Baadhi ya babu zangu hawa nimewadiriki wakiwa hai na wengine sikubahatika kuwaona.

Juu ya hayo simlazimishi mtu kuamini historia yao kama waasisi wa African Association (1929), Al Jamiatul Islamiyya Fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika (1933), walimpokea Julius Nyerere 1952, waasisi wa TANU 1954 na wapigania uhuru.

Kuhusu kuwa mimi ndiye peke yangu niliyefanya tafiti hili swali umelileta sipo.

Hali kadhalika kuwa mimi peke yangu ndiye mwandikaji paper na wasomi wengine hawajui kitu haya maswali yangu mie kukupa majibu.

Ulitakiwa uwaulize Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salaam Idara ya Historia.

Kuhusu hati miliki ya ukweli ni kuwa mimi ndiye mwenye hati miliki ya kitabu cha Abdul Sykes na vingine nilivyoandika kuhusu historia ya uhuru wa Tanganyika.

Bado nasisitiza kuwa simlazimishi yeyote kuamini historia niliyoandika.

Uko huru kuamini historia ya TANU iliyoandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni.


Kushoto: Iddi Faiz Mafungo, Sheikh Mohamed Ramiyya, Julius Nyerere, Saadan Abdul Kandoro na Haruna Iddi Taratibu, Dodoma 1955/56
Picha hii nimeipa jina: ''Wamanyema Wanne na Mzanaki Mmoja.''
(Picha kwa hisani ya Maktaba ya Sykes)

Mzee bin Sudi
(!896 - 1972)

Salum Abdallah (mshale) na kuliani kwake ni Kassanga Tumbo na viongozi wa TRAU

 
Kipenzi cha Mtume Muhammad (s.a.w)
 
Zanzibar pale kanisa lilichomwa moto na padri akauwawa kwa sababu za kidini. Kuna watu dini yao wanaiona ya muhimu sana kuliko dini za atu wengine; kila wakiamka wanafikiria dini tu. Ukipitia hapa JF, ndugu yangu Mohamed Said mada zake zote zinahusu dini ya uislamu na Nyerere tu.

Nyerere huingia katika mada zake kwa vile ndiye aliyekuwa wa mtu kwanza kuongoza chini hii baada ya uhuru wakati yeye siyo mwislamu. Iwapo Nyerere angefanya yale yale aliyofanya wakati wa utawala wake lakini akiwa mwislamu, usingesikia kelele na lawama za Mohammed.

Najaribu kuangalia maisha ya wakaristo yangekuwaje iwapo nchi yote hii ingekuwa kama Zanzibar; au iwapo Nyerere angeongoza nchi hii kwa maono anayotaka Mohamed.
 
Kichuguu,
Huko unakonipeleka mie siko huko.

Mimi nimeiandika kitabu kueleza historia ya kweli ya kupigania uhuru wa Tanganyika.

Leo wote tunasoma historia iliyotakiwa kuwepo miaka mingi.
 
Nyerere aliwapuuza wazee wake Mohammed kwa sababu walikuwa wabaguzi wa kidini kama Mohammed.Nyerere aliwaneutralize hawa wajinga kwa sababu walitaka kuisilimisha nchi.Nyerere alikuwa genious
 
Nyerere aliwapuuza wazee wake Mohammed kwa sababu walikuwa wabaguzi wa kidini kama Mohammed.Nyerere aliwaneutralize hawa wajinga kwa sababu walitaka kuisilimisha nchi.Nyerere alikuwa genious
Nan...
Hapana haikuwa hivyo.

Waislamu wangekuwa hivyo Nyerere asingekuwa kiongozi wa TANU.

Jitulize uisome historia ya uhuru wa Tanganyika utapata maarifa mengi sana.

Nakusihi uzuie mdomo wako kutamka matusi.

Hilo neno "wajinga," halikustahili.

Hakuna aliyebaguliwa katika TANU.
 
Sijatukana mtu ila nakumbushia tu kwamba katika hotuba zake,Nyerere aliwarefer watu wenye hoja za udini na ukabila ili kupata political regitimacy kama WAJINGA.Na indeed ni wajinga
 
Sijatukana mtu ila nakumbushia tu kwamba katika hotuba zake,Nyerere aliwarefer watu wenye hoja za udini na ukabila ili kupata political regitimacy kama WAJINGA.Na indeed ni wajinga
Nan...
Watu hao uwasemao wewe kuwa Nyerere kawaita wajinga kwa kutafuta uhalali kupitia Uislam sidhani kama ni hawa ambao mimi nimeandika historia zao wakiwa na Nyerere kuanzia alipofika Dar es Salaam 1952 hadi uhuru ulipopatikana mwaka wa 1961.

Angalia picha hizo hapo chini:


Baraza la Wazee wa TANU

Kulia: Chiku bint Said Kisusa, Bibi Titi Mohamed
Kushoto Tatu bint Mzee na katikati ni Julius Nyerere wakimsindikiza safari ya kwanza UNO 1956
Dhifa ya kumuaga ilifanyika katika jengo la Al Jamaiatul Islamiyya fi Tanganyika

Kulia: Mshume Kiyate, Julius Nyerere, Max Mbwana na Mwinjuma Mwinyikambi​

Kitabu cha Abdul Sykes kinaeleza historia ya wazalendo hawa ambao walikuwa na Mwalimu Nyerere bega kwa bega kupigania uhuru wa Tanganyika.

Unadhani Nyerere alikuwa katika hiyo hotuba yake aliwakusudia hawa na kuwaita wajinga?
 
Lengo la Uzi huu ni Nini mbona kama sielewi naona malalamiko tu ambayo hayana tija kwa taifa hili
 
Nimekuuliza swali hili mara nyingi lakini umekuwa ukinikwepa.Hawa wazee wako walipambania uhuru wa Tanganyika kama watanganyika ama waislam?
 
Nimekuuliza swali hili mara nyingi lakini umekuwa ukinikwepa.Hawa wazee wako walipambania uhuru wa Tanganyika kama watanganyika ama waislam?
Nan...
Sijakukwepa.
Nikwepe nini na kitabu kinajieleza?

Mimi si wa kujibu maswali ya ndiyo hapana.
 
ufahamishwe tu kuwa Sisi watu kubwa tumeshaanza kuhama kutoka kuwa wafuasi wa Dini yoyote, tumeamua kuwa wafuasi wa Mungu tu.

Dini tunaiweka kwenye vitu chonganishi Kwa sababu dini in it, it is people's way of living, it has nothing to do with God 's creation of human being ndio maana kila mtu huhudimiwa na Mungu kuanzia hewa na mvua bila kujali Dinii zenu

Fikiria huyu Mzee angekuwa ndio Mungu!
(God forgive) Angetupanga Kwa cha 666 kichwani huyu kibabu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…