Baba wa Taifa na tatizo la Udini

Master...
Mimi ninapoona mtu analeta kejeli, matusi na "name calling" huwa namkwepa simjibu.

Ila nakujibu wewe kutaka kukuongezea maarifa ili uelimike na ukipendezewa ujifunze adabu.

Mimi ukiniita "Kibabu," katika msamiati wetu watu wa Pwani unakuwa umekosea ikiwa nia yako ilikuwa kunitukana.

Ungeniita, "Kizee."

Ungefanya hivyo ungekuwa umenitukana kama ulivyokusudia.

Kikwetu, "Kibabu," ni jina anapewa mtoto mchanga wa kiume ambae bado hajapewa jina na akiwa mwanamke anaitwa, "Kibibi."
 
Mzee mi nadhani kubali tu,umeathiriwa sana na kutazama mambo kwa jicho la dini yako.Huo ni ugobjea ulionao na hauwezi kupona.Turuhusu tu tutambue kwamba huo ndo ulemavu ukionao.
Uko very parokial.
Mbona hauzunugumzii jamii nyingine nje ya uislam.Tufundishe korani kabisa basi tujue moja.
 
Maada karibu 50 zote unalialia

Machozi yamekauka, ila bado yumo tu. Na hakuna lolote la maana aliloweza kukamilisha. Muda ukuta. Kila kitu kina mwanzo na mwisho wake.

Tusije kuishia kutengeneza vicheko na kejeli baada ya haya maisha. Sisi binadamu, ni wepesi sana wa kusahau. Na nina uhakika, mfupa uliomshinda fisi, mbwa atapata nao tabu sana, waswahili wanasema
 

Mzee wangu unaweza kutuwekea takwimu kama hizi Kwa awamu hii? Kama hautojali pia utuwekee na Baraza la awali kabisa wakati wa Mwalimu, lililomjumuisha Mzee wetu Kawawa.
 
Insp....
Tuanze hapa.

Nini kilifanya historia ya uhuru wa Tanganyika kugeuzwa?
Unadhani nani mgonjwa.

Yule aliyeigeuza au yule aliyeiweka sawa?
Nani kilema.

Akataae ukweli au yule mwenye kuukubali ukweli?
 
Smart...
Ni hatari kuliko hatari yenyewe.

Ukiwa na watu wa dini moja wamehodhi fursa zote wakati wenzao wako nje ya hizo fursa unajenga chuki katika jamii.

Lazima hali hii iondoshwe.
Usikute Magufuli alichagua tu watu katika hizo nafasi katika tu hali ya kawaida ila nyie mnaoendekeza udini ndio mnajifanya mahodari wa kupekenyua majina kubaini waislamu wangapi wameteuliwa ni upumbavu uliotukukuka
 
Belo anasema nalialia.
Tangawezi unasema hakuna lolote la maana nililokamilisha.

Tuanze na kulialia.
Mimi silii.

Mimi nimeandika historia ya harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika kwa kiasi ambacho vitabu vilivyotangulia havikufikia kiwango changu.

Nini ushahidi wa haya nisemayo?

Kitabu changu kimefanyiwa review tatu na mabingwa wa African History: John Iliffe, Jonathon Glassman na James Brennan.

Review hizi zote zimechapwa katika Cambridge Journal of African History.

Baada ya haya nikatiwa katika miradi miwili ya kuandika historia ya Afrika.

Mradi wa kwanza Oxford University Press, Nairobi (2007).

Wamechapa kazi zangu.

Mradi wa Pili Harvard na Oxford University Press, New York (2008) kuandika Dictionary of African Biography (DAB)(2011).

Nimeshiriki katika mradi wa kuandika Nyerere Biography (2020).

Huu mradi wa tatu.

NImeshiriki katika mradi wa kuandika historia mpya kama alivyoagiza Rais Magufuli.

Mradi wa nne.

Haya ni baadhi ya mambo ambayo Mola kanijaalia kukamilisha.

Yapo mengi lakini kwa leo nimekuwekeeni hayo kukujibuni kuhusu ''kulialia'' na mimi kugeuka kuwa ''kichekesho.''



Kitabu cha Abdul Sykes pembeni ya kitabu cha Julius Nyerere
Kitabu cha Abdul Sykes kimechapwa mara nne.
(Angalia majadala tofauti kwa kila toleo)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…