Baba wa Taifa na tatizo la Udini

Baba wa Taifa na tatizo la Udini

Wote tunajifunza hapa na ndio maana tunafanya mjadala kubadilishana mawazo tupate maarifa mapya

Nataka nijue nchi hii mtu asiyekuwa na dini amepewa kipaumbele gani kwenye rank za madaraka

Lakini pia ningependa kujua ni vigezo gani ambavyo vinaangaliwa sana linapokuja swala la kupeana madaraka

Hapo juu nimeona umeelezea 80:20 ambayo imehusisha wakristo na waislamu

Lakini sijakuona ukijitokeza kuwasemea kundi lililosahaulika hapo (atheists) kuwa wanabaguliwa na viongozi wa dini hizo mbili (islam&christian) badala yake umeongelea uislam kua umezidiwa na ukristo katika rank za madaraka, ila atheists ambao hawajapata hata mtu mmoja serikalini umeona ni sawa

Kwanini iwe hivyo?
Scars,
Bila kuijua historia ya uhuru wa Tanganyika utapata shida sana na kuja na hoja ambazo kwa mtu aneijua historia hii kwa kweli atabaki kucheka.

Angalia hizo picha hapo chini za harakati za kudai uhuru.
Nionyeshe mpagani hapo:

1643493003961.png

1643493083279.png

1643493224569.png
 
Asante ningependa sana kupata majibu ya hoja zangu kwa sababu sijauliza ili nisifiwe bali nimeuliza ili nijibiwe

Nina imani nitajifunza tu kwenye majawabu yako mzee wangu
Saf...
Ikiwa umekuja kujifunza karibu sana.
Nimewafunza wengi sana hapa JF na wengine wengi nje ya hapa.

Angalia hizo picha hapo juu kuna mengi ya kujifunza.
Kuna mtu kaleta hoja ya Wapagani jibu lake ndilo hilo hapo juu.

Je, umejifuza nini katika picha hizo.

Kabla ya mimi kuzileta izo picha ulipata kuziona popote katika historia ya TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika?

Sasa jiulize kwa nini?
 
Mama anabalansi shobo kwa kasi ya kutisha. Kwa kila teuzi kumi anahakikisha waislamu wanane na wagalatia wawili. Baada ya utawala huu, huku kulia lia kwa waislamu kuwa walionewa na kutengwa kufikie mwisho sasa. Mpaka mwaka 2030 mama atakapoondoka madarakani kila kitengo nyeti katika nchi hii kitakuwa kinaongozwa na mwislamu. Mshindwe wenyewe tu sasa!
 
Kwa hiyo kumbe mtu asiyekuwa na dini hana nafasi ya kupewa madaraka kwenye nchi ambayo haifungamani na dini?
Scars,
Jitulize usome historia ya uhuru wa Tanganyika.

Usiwe na haraka ya kufanya mjadala na mie.
 
Scars,
Jitulize usome historia ya uhuru wa Tanganyika.

Usiwe na haraka ya kufanya mjadala na mie.
Historia ya tanganyika tumesoma shuleni na ndio ambayo wewe unaonekana kuipinga ukidai kua kuna mambo mengi yamefichwa, ila tunapojitokeza kukuhoji ili nasi tupate kuyajua hayo yote nashangaa unaturudisha kule kule ambako mwanzo ulionesha kutokuwa na imani nako

Mimi nataka tu unijibu maswali yangu ili namimi niweze kupata hayo maarifa
 
Scars...
Najibu maswali mengi sana hapa ila ninapoona mtu anataka kunifunga kwenye ubishi namuacha kama alivyo kwa kuwa si rahisi kumjibu mtu swali lake kama yeye anavyotaka kujibiwa.

Mimi hapa nipo kusomesha historia ya kweli siko katika ubishi.

Sidhani kama neno ''kupinga,'' ni sawa katika muktadha huu.
Nilichofanya mimi nimesahihisha vitu muhimu sana katika historia ya Tanganyika.

Mathalan historia ya Kimambo na Temu (1961) na historia ya Chuo Cha CCM Kivukoni (1981)kuhusu TANU zote zinaanza na Julius Nyerere na zinarashiarashia historia ya African Association (AA).

Mimi nimeanza kitabu changu kueleza historia ya AA na historia za koo mbili mashuhuri katika Dar es Salaam ya 1950s - Plantan na Sykes.

Ikiwa unaona tabu kurejeshwa kwenye ukweli hili halina ugomvi unaweza ukabakia na historia yako kuwa Mwalimu Nyerere ndiye aliyeunda TANU peke yake.

Lakini mimi katika hili nitakupa ushahidi kuwa TANU iliundwa nyumbani kwa Abdul Sykes Mtaa wa Aggrey na Sikukuu na nitakutajia mpaka no. ya kadi ya Abdul Sykes no. 3, Ally Sykes no. 2, Julius Nyerere no. 1.

Sitoishia hapo nitakuelea kuwa na hizo kadi za TANU alinunua Ally Sykes kutoka mfukoni kwake na kadi ya Mwalimu iliandikwa na Ally Sykes.

Naiachia akili yako ijiulize ikiwa historia ni hii mbona anatajwa Nyerere peke yake miaka nenda miaka rudi?
 
Huyu mleta mada ni mtu mharibifu sana. Narudia mharibifu sana. Watu wa hovyo wakutaka kuturudisha zamani au kutupeleka kusiko na maana. very soon utasikia kuna mwandishi uchwara mwingine kajitokeza na hoja zake " Jinsi nyerere alivyosaliti walutherani" na atakuja na mapicha picha yake, this is not okay.......

Mfano wa vitu simwelewi, kama huyo adbul sykes angepewa uongozi kwani ni nini cha ajabu kingetokea?. Ilikuwa apewe wizara ya fedha ikiwa hana taaluma hiyo, kisa tu alimpa hifadhi nyerere? This is not okay ......

Mwalimu alikuwa na marafiki wengi, jamaa na ndugu wengi, wengine wa damu ,na hakuwapa vitengo, hao mbona sijaskia waikilalamika? mataifa mengine viongozi wa kwanza walijaza ndugu zao katika uongozi, kwa Nyerere hatukuona hilo..
Manake ni kwamba kigezo alichokuwa anatumia ni nani ako na the best mind sio what religion kwenye kitengo husika.

Mkuu kuendesha nchi kwa mara ya kwanza ni zaidi ya kuendesha startup from the jungle, na tukubali tuu mwalimu was the Genius. Apumzike kwa Amani.
 
Sop...
Suala si hilo.

Tatizo ni kufutwa kwa historia ya Abdul Sykes na wazalendo wengine katika historia ya TANU.

Si swala la vyeo baada ya uhuru.

Hakuna anaekataa uwezo wa Mwalimu.

Soma kitabu cha Abdul Sykes yote hayo nimeeleza.

Usiandike ukiwa umeghadhibika.

Mimi naeleza historia ya wazee wangu vipi walipigania uhuru wa Tanganyika.
 
Day...
Usipate shida kila binadamu ana uwezo wake wa kuelewa.
Hili ni jambo la kawaida sana.
Kweli Mzee wangu.ingawa mwanafunzi anapouliza maswali hutegemea majibu kwa mwalimu wake.sasa mwalimu naye anapoleta shaka ya kujibu maswali ya mwanafunzi huiacha adhira ya kuwa na shaka na mwalimu wao.

Sent from my TECNO CD7 using JamiiForums mobile app
 
Mimi nakuruhusu siyo uwe na shaka nami bali usiamini hata kuwa historia niliyoandika ina ukweli.

Tumeishi miaka tele na historia ya Kimambo na Temu na ya Chuo Cha CCM Kivukoni.

Hakuna aliyeuliza ukweli wake na maisha yaliendelea.
 
Hapana tuangalie zanzibar kwanza ambako kuna waislamu watupu kabla yatujafanya huku.

Je kwa zehemu kama zanzibar wizara zote zina waislamu wewe unadhani wamenufaika ama kupata jambo gani kubwa katika uislamu au kwa waislamu alafu ikawa uislamu wa huku bara haujalipata jambo hilo kutoka katika serikali ya bara ambako kuna wakristo wengi ?

Kwa nini umechagua waislamu na tusianze na wakristo wachaguliwe kwanza ?

Pia mzee wangu hii haitokuwa kampeni itakuwa ni kuendeleza lile linaloitwa tatizo kwa sababu raia hujawapa kampeni yoyote ya kukabiliana na jambo hilo

Simjibii Mzee Mohammed , lakini kwa Zanzibar kuna kitu kinaitwa Akhlaak, Tabia nzuri .

Kabla Zanzibar haijavamiwa na Tanganyika tabia za Wazanzibari zilikuwa nyengine kabisa kinyume na baada ya mavamizi. Wizi , heshima, na tabia njema takriban vimeondoka kwa kufuata hizi tabia za wakristo na makafiri.

Zamani ulikuwepo ujirani na kusaidiana , sasa kila mtu ki vyake.

Ukipoteza kitu , kikionekana kinarudishwa , hivi sasa ni mtihani.

Mfumo huu wa ki CCM umeharibu kila kitu na ndilo lengo la hao waliovamia kuichafua nchi
 
Huyu mleta mada ni mtu mharibifu sana. Narudia mharibifu sana. Watu wa hovyo wakutaka kuturudisha zamani au kutupeleka kusiko na maana. very soon utasikia kuna mwandishi uchwara mwingine kajitokeza na hoja zake " Jinsi nyerere alivyosaliti walutherani" na atakuja na mapicha picha yake, this is not okay.......

Mfano wa vitu simwelewi, kama huyo adbul sykes angepewa uongozi kwani ni nini cha ajabu kingetokea?. Ilikuwa apewe wizara ya fedha ikiwa hana taaluma hiyo, kisa tu alimpa hifadhi nyerere? This is not okay ......

Mwalimu alikuwa na marafiki wengi, jamaa na ndugu wengi, wengine wa damu ,na hakuwapa vitengo, hao mbona sijaskia waikilalamika? mataifa mengine viongozi wa kwanza walijaza ndugu zao katika uongozi, kwa Nyerere hatukuona hilo..
Manake ni kwamba kigezo alichokuwa anatumia ni nani ako na the best mind sio what religion kwenye kitengo husika.

Mkuu kuendesha nchi kwa mara ya kwanza ni zaidi ya kuendesha startup from the jungle, na tukubali tuu mwalimu was the Genius. Apumzike kwa Amani.

Unaungua maini na propaganda ulizopigwa. Hulaumiki ulimnywa sana Nyerere na umelewa kuliko unga wa kokaini. Ni kazi kufuta disc lakini jitahidi kusoma na utoke nje ya box
 
Kong...

Uadilifu II

Serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani Mwaka (2015), Rais alifanya uteuzi wa Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Wilaya na Wakurugenzi mbalimbali. Uteuzi wake ulikuwa kama ifuatavyo:

Mawaziri na Manaibu: 30.

Waislamu 10, sawa na asilimia 33%.

Wakristo 20, sawa na asilimia 67%.

Makatibu Wakuu na Manaibu: 50.

Waislamu 10, sawa na asilimia 20%.

Wakristo 40, sawa na asilimia 80%.

Wakuu wa Mikoa na Wilaya: 166.

Waislamu 41, sawa na asilimia 25%.

Wakristo 125, sawa na asilimia 75%.

Makatibu Tawala wa Mikoa na Wilaya: 163.

Waislamu 24, sawa na asilimia 15%.

Wakristo 139, sawa na asilimia 85%.

Wakurugenzi mbalimbali: 249.

Waislamu 45, sawa na asilimia 18%.

Wakristo 204, sawa na asilimia 82%.

Manaibu Kamishna wa Polisi: 25.

Waislamu 5, sawa na asilimia 20%.

Wakristo 20, sawa na asilimia 80%.

Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi: 33

Waislamu 7, sawa na asilimia 21%.

Wakristo 26, sawa na asilimia 79%.

Jumla Kuu ya Uteuzi:

Waislamu asilimia 20%.

Wakristo asilimia 80%.

Uteuzi huo umekuwa kama Sera kwa teuzi zinazoendelea ndani ya miaka yote mitano. Vilevile kama Mwongozo kwa wateule wenye mamlaka ya kuteuwa. Mwelekeo huo unakinzana na Katiba ya nchi ibara ya 13(4)(5), inayokataza ubaguzi wa aina zote. Kwa hakika Taifa halihitaji kiongozi wa nchi akiwa Muislamu basi ateuwe idadi kubwa ya Waislamu wenzake katika nafasi mbalimbali za uongozi wa nchi au akiwa Mkristo atumie uongozi wake kuteua idadi kubwa ya Wakristo wenzake katika uongozi nchini. Au akiwa Mzanaki ateuwe idadi kubwa ya Wazanaki wenzake katika nafasi mbalimbali za uongozi na mfano wa hayo.

kwa mtizamo wangu uteuzi hauangalii dini ya mtu bali ufanisi kwenye kazi anayokwenda kuifanya
 
Leo Junapili January 30/2022

Raisi wa JMT ni Mwislamu
Waziri Mkuu wake ni Mwislamu
Raisi wa Zanzibar ni Mwislamu
Makamu wake Ni Mwislamu
Waziri wake Kiongozi ni Mwislamu

Je bado kuna malalamiko ya ukandamizwaji wa Dini yoyote ?
Au ni lazima fulsa ziwe 50/50 ndio turidhike kuwa kuna fare play ?
 
Mfumo Na watendaji bado ni kristo
 
Back
Top Bottom