Baba wa Taifa na Wazee wa Dar es salaam waliomuunga mkono wakati wa kupigania uhuru

Baba wa Taifa na Wazee wa Dar es salaam waliomuunga mkono wakati wa kupigania uhuru

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
Utangulizi

Francis Daudi ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu Ulaya ambae akimaliza masomo yake atakuja kuwa mwalimu wa historia. Tumejuana na tunabadilisha mawazo katika historia ya Tanzania. Ameniletea hii hotuba hapo chini nami nimempa fikra zangu.

HOTUBA YA MWALIMU NYERERE YA KUAGA TAIFA TAREHE 5 NOVEMBA, 1985 KABLA HAJASTAAFU URAIS ALIYOITOA MBELE YA WAZEE WA DAR ES SALAAM

Baraza la Wazee wa TANU 1955
(Picha kwa hisani ya Msakala Mohamed Tambaza)

[9:10 AM, 3/20/2018] Francis Daud:

‘"Mimi nimeanza siasa na wazee wa Dar es Salaam; na wazee wa Tanzania. Nimeanza nao mapema sana; mapema kweli. Nilirudi kutoka masomoni, Uingereza Oktoba 1952 – miaka 33 nyuma. Wakati huo nikiwa kijana mdogo wa miaka thelathini na kidogo hivi.
MS

''Niliporudi nikakubaliana na wamisionari hapo Pugu (sekondari), nifundishe shuleni kwao. Lakini nikiwa shuleni – Chuo Kikuu – nilijua. Niliishaamua kwamba maisha yangu yatakuwa ya siasa. Niliamua hivyo: Nitafundisha kwa muda wa miaka mitatu, nione hali inavyokwenda na kuzoeana na wenzangu kabla ya kuanza maisha ya siasa.

Niliporejea nchini hapo Oktoba, nikaenda Butiama. Januari nikarudi Dar es Salaam. Nikaanza kazi. Nikataka kujua habari za African Association. Mzee Mwangosi anakumbuka. Yeye ndiye aliniambia habari za African Association. Aliisha niambia habari hizo tangu nikiwa Makerere – Chuo Kikuu – nikiwa mwanafunzi.

Pale, mimi na wanafunzi wenzangu tulikuwa tumeanzisha chama kinachoitwa Tanganyika African Welfare Association (TAWA) cha wanafunzi wa Tanganyika; mimi nikiwa katibu wao. Hapa tukaona mambo yanakwenda vizuri kidogo.

Tukaona kwanini TAWA iwe ya wanafunzi peke yao na siyo Tanganyika nzima. Kwa hiyo nikawaandikia baadhi ya watu Tanganyika. Nikasema, jamani ee, tumeanzisha chama, kwanini msianzishe huko matawi ya chama hicho?

Ndugu Mwangosi akapata barua hiyo. Alikuwa miongoni mwa waliopata barua hiyo. Akaniandikia – nikiwa Makerere – akasema: wewe kwanini unataka kuanzisha chama kipya? Kipo chama. Kipo chama cha TAA (Tanganyika African Association).

Kwa hiyo la maana siyo kuanzisha matawi, maana chama kipo na matawi yameenea; la maana ni kwamba hicho chama chenu mfute, na muanzishe tawi la Tanganyika African Association.

KUVUNJWA KWA TAWA
Hivyo ndivyo tulivyofanya. Kwa hiyo mimi nikawa katibu wa katawi ka TAA hapo Makerere. Niliporudi Tabora na kuanza kufundisha pale St. Marys (sasa inaitwa Sekondari ya Milambo), nikachaguliwa katibu wa TAA wa jimbo ambalo makao yake makuu yalikuwa Tabora. Ulipofanyika mkutano wa TAA mjini Dar es Salaam, nilihudhuria nikiwa mjumbe kutoka Tabora.

Kwa hiyo nilikuwa naijua Tanganyika African Association. Nilipokuwa ninaondoka kwenda Ulaya kusoma, nilikuwa nimeishaonja shughuli za TAA. Sasa niliporudi, baada ya kukaa Pugu siku chache, nikaja mjini Dar es Salaam. Nikauliza nani wanaongoza TAA?Nikaambiwa kuna jamaa mmoja anaitwa Abdul Sykes. Sasa ni marehemu. Abdul ndiye alikuwa katibu wakati huo.

Nilipelekwa na Kasela Bantu - ambaye naye aliteleza-teleza na hatunaye hapa (kwenye mkutano). Kasela Bantu alikuwa mwalimu mwenzangu. Tulifundisha pamoja Milambo. Nilipokuja Dar es Salaam, nikakuta anafanya kazi Redio (Tanganyika Broadcasting Corporation). Ni Kasela Bantu aliyenipeleka kwa Sykes.

Wakati huo mambo yalikuwa yanasinzia kidogo. Kwa muda mfupi mwaka ule, tukafufua-fufua, hasa kutoka Januari. Kufika Aprili, TAA ikafufuka. Tukafanya mkutano hapo Anautouglou. Kwenye mkutano huu wakanichagua…''

UCHAMBUZI WA HOTUBA YA MUAGO YA BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE

Francis,

Hotuba hii mimi inanishangaza kwa jinsi Mwalimu Nyerere alivyoacha kutaja majina ya hao wazee anaowashukuru. Huwezi kuwaadhimisha watu wasio na majina, maana yake na tafsiri yake ni kuwa huwajui au umesahau majina yao. Hawa wazee wanafahamika na kila mtu alichangia kwa namna yake kiasi Mwalimu Nyerere hawezi hata kidogo kuwasahau. Wapo aliojuananao kwa shughuli za TANU na siasa tu na kuna wale aliojuananao zaidi katika udugu kwa kuwa wao ndiyo waliompokea kama mgeni wao na akawa sehemu ya ndugu katika ukoo. Hapa sitawataja akina Sykes kwa kuwa historia yao na Baba wa Taifa sasa ni mashuhuri inafahamika. Lakini kuna watu kama Shariff Abdallah Attas na mkewe Bi. Chiku Kikusa, mama yake Maalim Sakina na Maalim Fatna Baba wa Taifa alionekana zaidi kana ndugu. Maalim Sakina na Maalim Fatna ndugu hawa wawili wote walikuwa walimu katika shule ya Al Jamiatul Islamiyya Fi Tanganyika. Shariff Attas alijuana na Nyerere si zaidi katika siasa bali kama mgeni wa Abdul Sykes.

Shariff Abdallah Attas

Shariff Attas alikuwa akifanya kazi Soko la Kariakoo ambako Nyerere alianza kufika pale 1952 kila akija mjini kutoka Pugu mwisho wa juma. Abdul Sykes alikuwa ndiye Market Master na Shariff Attas akiwa Dalali Mkuu wa Soko. Kupitia kwa Abdul Sykes ndipo Nyerere akajuana na Shariff Attas na watu wa nyumbani kwa Shariff na jamaa zake wote kama Maalim Fatna, Bi. Chiku Kisusa mama yao mzazi Maalim Sakina na Maalim Fatna. Lakini hawa wote niliowataja ndiyo wakajakuwa wanachama wa kwanza wa TANU mjini Dar es Salaam. Hata ukiangalia picha hiyo hapo chini huyu mama utamuona yuko na Baba wa Taifa Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam akimsindikiza Mwalimu Nyerere safari yake ya kwanza UNO, 1955.

Kulia Mzee Mshume Kiyate, Julius Nyerere, Mzee Max Mbwana na
Mzee Mwinjuma Mwinyikambi, 1962

Kulia ni Bi, Tatu Kisusa, Bi, Titi Mohamed, wa nne Julius Nyerere
na wa mwisho ni Bi. Tatu Bint Mzee

Hapo sokoni Karikakoo ndipo Mwalimu Nyerere akajuana na Mzee Mshume Kiyate. Sasa huyu Mzee Mshume Kiyate wakajuana zaidi katika siasa na udugu ukaja baadae. Mzee Mshume alikuwa mmoja wa wajumbe katika Baraza la Wazee wa TANU na alikuwa mmoja wa wafadhili wakubwa wa chama hadi uhuru ulipopatikana na hili hakuna asiyelijua. Haiyumkini ikawa mtu kama Mzee Mshume KIyate akatajwa kwa ujumla wa ‘’wazee,’’ pasi na kulitaja jina lake. Katika hotuba hii Mwalimu Nyerere kamtaja Sheikh Mohamed Ramiyya lakini hakueleza alimjua vipi Sheikh Ramiyya kwani yeye hakuwa mkazi wa Dar es Salaam. Sheikh Ramiyya alikuwa akiishi Bagamoyo na waliomchukua Baba wa Taifa kumpeleka Bagamoyo kumjulisha kwa Sheikh Ramiyya walikuwa Mzee Idd Tosiri na Mzee Idd Faiz Mafungo na wote hawa watatu, Sheikh Ramiyya, Tosiri na Faiz ni ndugu Wamanyema na wazee wao walitokea Belgian Congo. Hawa walitoa mchango mkubwa katika TANU. Ilistahili siku ile Baba wa Taifa awataje kwa majina yao. Hii mosi.

Pili, tuje kwa Abdul Sykes.

Kulia Idd Faiz Mafungo, Sheikh Mohamed Ramia, Julius Nyerere
na Haruna Taratibu

Abdul alikuwa wakati ule Nyerere alipopelekwa kwake kukutananae, Abdul alikuwa Kaimu Rais na Katibu wa TAA. Rais alikuwa Dr. Vedasto Kyaruzi lakini kwa sababu ya uongozi huu wa Abdul na Dr. Kyauzi kuiingiza TAA katika masula mazito ya siasa walipoingia madarakani 1950, Dr. Kyaruzi akapewa uhamisho akapelekwa Kingolwira Prison akawe daktari wa wafungwa na ilipoonekana kuwa uhamisho ule haukumzuia kuja Dar es Salaam mwisho wa juma kuja kuonana na Abdul Sykes kendeleza harakati za TAA, Dr. Kyaruzi akahamishiwa Nzega. Hii ndiyo ikafanya sasa nafasi ya rais iwe wazi haina mtendaji na Abdul akakaimu nafasi ile kwa miaka takriban mitatu bila ya kuitisha uchaguzi. Ulipofika mwaka wa 1953 ulipofanyika uchaguzi wa mwaka Nyerere na Abdul wakagombea nafasi ya urais. Hili si Nyerere wala wanahistoria wetu wamelieleza popote.

Nyerere katika hotuba yake hii kwa Wazee wa Dar es Salaam anasema,’’ Tukafanya mkutano hapo Anautouglou. Kwenye mkutano huu wakanichagua…’’ Katika hotuba hii Mwalimu Nyerere kamtaja Abdul Sykes kuwa ni mmoja wa vijana wenzake waliokuwa katika siasa mwingine akisa Dossa Aziz lakini hakusema kuwa aligombea na Abdul Sykes nafasi ya urais wa TAA katika uchaguzi wa mwaka wa taehe 17 April 1953 pale Ukumbi wa Arnautoglo. Wala hakusema kuwa alishinda uchaguzi ule kwa kura chache sana. Hii ni muhimu sana kwani In Shaa Allah nitaeleza huko mbele kuwa hii ilikuja kuwa ndiyo sababu TAA ilikufa baada ya yeye kuchukua uongozi.

Kushoto Dossa Aziz, Julius Nyerere, Abdul Sykes na Lawi
Sijaona, Ukumbi wa Arnautoglo katika tafrija ya kumaga Nyerere
safari ya pili UNO 1957

Tatu, si kweli kuwa TAA ilikuwa imesinzia kwa sababu 1950 ilikuwa imeunda TAA Political Subcommittee ikiwa na wajumbe hawa wafuatao: Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo, Hamza Mwapachu, Stephen Mhando, John Rupia, Dr. Vedasto Kyaruzi na Abdul Sykes. Kamati hii ilitengeneza mapendekezo ya katiba kwa Gavana Edward Twinning. Haya mapendelezo ndiyo Mwalimu Nyerere aliyasoma katika hotuba yake UNO mwaka wa 1955. Haiwi chama kilichosinzia kikaja na mapendelezo mazito kama haya ambayo yalifika hadi UNO. Licha ya hili mapendekezo haya ndiyo yalijadiliwa katika mkutano uliounda TANU na wanakamati wake wawili Abdul Sykes na John Rupia wakiwa kati ya wajumbe 17 wa mkutano ulioasisi TANU mwaka wa 1954.

Kulia Sheikh Said Chaurembo na Liwali Ahmed Saleh,
1956

Lakini ukweli ni kuwa chama kilisinzia Mwalimu Nyerere alipochaguliwa kuwa Rais wa TAA na ikabidi zifanyike jitihada ili kukihuisha upya chama. Muhimu ieleweke kuwa TAA haikudorora kwa kuwa kiongozi alikuwa hana uwezo, la hasha, TAA ilidorora kwa kuwa Nyerere alikuwa hafahamiki hili la kwanza la pili ni kuwa kwa wakati ule Nyerere hakuweza kutia katika chama kile ambacho Abdul alikuwa akifanya kwa muda wote alipokuwa kiongozi wa juu. Ukweli ni kuwa ikiwa halmashari ya TAA itakutana nyumbani kwake basi kikao kitamalizika vizuri kwa pengine kula na kunywa pale nyumbani au Princess Hotel. Hulka hii iliendelea hadi wakati wa TANU. Mwalimu Nyerere alikuwa mgeni Dar es Salaam na hakuwa na fedha wala na nyumba ambayo angeliweza kufanya haya. Nyumba ya Abdul ambayo kabla yake ilikuwa nyumba ya baba yake, Kleist Sykes, ilikuwa kituo cha harakati dhidi ya ukoloni. Toka miaka ya 1920.

Nne, mwaka wa 1952 TAA ikishirikiana na Meru Citizens Union ilifanikisha kumpeleka Japhet Kirilo na Earle Seaton UNO katika "petition" ya Mgogoro wa Ardhi ya Wameru na ilikuwa Abdul Sykes akiwa Katibu na Kaimu Rais wa TAA ndiye aliyemwomba Earle Seaton asaidie kutoa ushauri kwa Meru Citizens Union katika mgogoro ule kwani Seaton alisaidia sana TAA Political Subcommittee katika kuandika mapendekezo ya katiba yaliyokwenda kwa Gavana Twinning 1950, mapendekezo ambayo kama ilivyoelezwa huko juu, ndiyo yaliyotengeneza hotuba ya Mwalimu Nyerere UNO 1955.

Kushoto Earle Seaton na Julius Nyerere baada ya uhuru Seaton
akiwa mfanyakazi wa serikali ya Tanzania

Tano, si kweli kuwa hawa wazee walikuwa hawajui nafasi ya Waingereza katika Tanganyika kwani Visiting Mission za UNO zilikuwa zikipita Tanganyika na TAA ikishiriki katika mazungumzo na taarifa zao zikiandikwa katika gazeti la Zuhra lililokuwa likiendeshwa na Ramadhani Mashado Plantan kama mhariri. Hii ndiyo ilikuwa sauti ya Waafrika wa Tanganyika. Nyerere mwenyewe kaandikwa kwa mara ya kwanza jina lake na habari zake ndani ya gazeti hili mwaka wa 1953. Haiwezekani katika hali ya siasa kama hii ikawa kuwa wazee hawakujua waanzie wapi kudai uhuru. Ukiachia TAA Political Subcommittee 1950 ambamo walikuwa watu wazima kama Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo na John Rupia, zipo pia barua za 1933 walizoandikiana Rais wa African Association Mzee bin Sudi na Katibu, Kleist Sykes zikizungumza kuhusu uhuru wa Tanganyika.

Kwa ajili hii basi si kweli kuwa watu hawakujua namna ya kutaka kujitawala. Abdul Sykes alianza harakati za kuunda TANU akiwa Burma katika Vita Vya Pili Vya Dunia (1938 -1945) na msingi wa kuasisi TANU aliujenga kupitia 6th Battalion ya King African Rifles (KAR) Burma Infantry. Shajara ya Abdul Sykes inaonyesha kuwa mazungumzo ya mwisho ya azma ya kuunda chama cha siasa yaliyafanywa Kalieni Camp India tarehe 25 Desemba 1945 mkesha wa Xmas wakisubiri meli kurejeshwa Tanganyika baada ya kumalizika vita.

Mimi naamini hotuba ya Baba wa Taifa ilitolewa akiwa yeye mwenyewe hajui mengi kabla ya wakati wake. Naamini kabisa kuwa yawezekana pia Mwalimu Nyerere hakuwa anamjua Abdul Sykes vizuri na historia ya baba yake Kleist, katika siasa za ukombozi wa Tanganyika na kuundwa kwa African Association 1929 lau kama aliishi na watoto wake, Abdul, Ally na Abbas kwa karibu sana hadi uhuru ulipopatikana mwaka wa 1961. Lakini vilevile utafiti umeonyesha pia kuwa baada ya uhuru ziliingia sababu nyingine zilizofanya historia ya TANU ielezwe kwa namna alivyoieleza Baba wa Taifa ikiwaweka pembeni baadhi ya wazalendo. Itoshe tu kwa kuhitimisha kusema kuwa hata hao wazee ambao Mwalimu Nyerere hakuwataja kwa majina, alijulishwa kwao na Abdul Sykes na Dossa Aziz. Iwe iwavyo si rahisi kusahau kuwa Msajili wa Vyama Vya Siasa alikataa kuiandikisha TANU kwa kuwa chama hakikuwa na wanachama Nyerere alipofikisha maombi ya TANU kwake. Si wengi wanajua hili lakini Ilikuwa Mzee Said Chamwenyewe ndiye aliyetumwa Rufiji na Abdul Sykes akaandikishe wanachama wa mwanzo wa TANU ambao Baba wa Taifa alifikisha orodha yao ile kwa Msajili wa Vyama Vya Siasa na TANU ikaandikishwa.
 
Jivi hapo wazee bado wapo hai???
Nataka nikawasalimie na kufanya nao mahojiano
Mjukuu wa Chifu,
Acha hao wazee.

Hao vijana wa wakati ule wa mwisho niliyekuwa namfahamu alikuwa Ally Sykes
na yeye ameshafariki.

Tuliobaki ambao tuliwaona hao wazee na vijana wa wakati ule mimi ni mmojawapo
na sasa nina miaka 66.
 
  • Thanks
Reactions: Pep
broo mo'd katk ubora wako,pamoja na mafanikio aliyopata mwl bado alikuwa mwanadamu na hulka za kibinadamu hazikumwacha,tumuombee mema huko aliko.
 
broo mo'd katk ubora wako,pamoja na mafanikio aliyopata mwl bado alikuwa mwanadamu na hulka za kibinadamu hazikumwacha,tumuombee mema huko aliko.
Nnangale...
Usiwe na haraka yalikuja mambo ya kusikitisha kuanzia 1963 baada ya Muslim Congress ya 1962 na 1963...

Ukisoma kitabu cha Abdul Sykes utayakuta humo.
 
Nnangale...
Usiwe na haraka yalikuja mambo ya kusikitisha kuanzia 1963 baada ya Muslim Congress ya 1962 na 1963...

Ukisoma kitabu cha Abdul Sykes utayakuta humo.
sawa kaka ningependa kusoma kisa chote cha mwl kuwaacha nje ya utawala washirika wake wa mwanzo na kuhire watu wengine kwenye ku-run serikali.
 
Siasa za ubepari ndizo siasa zinazothamini utu wa mtu mmoja mmoja. Individual rights and personal recognition.

Siasa za kijamaa zina tabia ya kulundika watu kwa mafungu. Ndiyo maana ya Ujamaa. Communal living. Collectivism. Jamiii inawekwa juu ya mtu mmoja, kijiji juu ya nyumba.

Mtu mmoja anapokea sifa kwa niaba ya wote.

Ukitaka mtu mmoja mmoja aangaliwe, katika siasa za kijamaa, unaweza kuitwa mbinafsi. Unaendekeza habari zako/ zake mtu binafsi, kuliko maendeleo ya wote.

Kwa mjamaa kushukuru watu kwa mpigo, kwa kutaja wachache tu wakawa wawakilishi wa wengi, hilo halishangazi kabisa.

Linaloshangaza ni kuona wasomi wa historia wanavyotaka Mjamaa, ambaye itikadi yake ni kuangalia watu kwa mafungu na kutojali sana mtu mmoja mmoja, athamini mtu mmoja mmoja na kumshukuru mtu mmoja mmoja kama bepari.
 
Kiranga,
Haikuwa hivyo...

Huu ni mkasa mrefu na una mengi.

Bahati mbaya mimi nimeishi ndani ya historia hii lau nilikuwa mdogo leo nikiangalia nyuma mengi yanafunguka na kuwa wazi na hadhir.

Kwani wewe uliyajua haya?
Naamini ndiyo kwanza unayasikia.

Yapo mengi, mengi sana yaliyotokea mara tu uhuru uliopopatikana.

Ndiyo hayo niloyokujakuandika na kuchapa kitabu kizima na kufungua mlango wa historia mpya ya uhuru.

Wengi wamevutiwa na elimu hii mpya.
 
Mzee wangu hujanijibu hoja yangu.

Habari za lawama kwa Nyerere kukosa kuwataja waliomsitiri, zinaendana na ustaarabu na itikadi za kuthamini mtu mmoja mmoja.

Nyerere ni mjamaa. Wajamaa hawana tabia ya kumuangalia mtu mmoja mmoja. Wanaangalia jamii collectively, mtu mmoja anawakilisha wengi.

Sasa kwa nini mnamlaumu Muarabu kwa kutojua kuandika Kiingereza wakati si lugha yake?

Kwa nini mnamlaumu mjamaa anayethamini the collective kuliko the individual kwa sababu hakutaja vilivyo individuals, kawataja collectively kama wazee, na katoa majina machache ya wawakilishi tu?

Hujanijibu hoja hii.
 
Nimekujibu ila jibu silo ulilolipenda.

Wala mimi sikumlaumu Baba wa Taifa nilichofungulia kauli yangu ni kusema, ''Nashangaa.''

Mbele katika maelezo yangu nikasema kuwa Baba wa Taifa hakuwa anaijua historia ya African
Association kabla ya wakati wake na hili ni tatizo kubwa katika kutafiti historia ya TANU na uhuru
wa Tanganyika.

Nyaraka nyingi ziko mikononi mwa watu binafsi hakuna anaeyeijua historia hii kwa ukamilifu wake
ila wachache sana na wengi wametangulia mbele ya haki.

Mwaka wa 1981 ndani ya jopo la Chuo Cha Kivukoni walipokuwa wanaandika historia ya TANU jopo
lilikataa kupokea baadhi ya nyaraza za zamani sana za African Association zilizoletwa na mwanajopo
Hassan Upeka aliyeajiriwa na TANU 1956 kama Afisa Usalama.

Huyu Hassan Upeka ni mmoja wa watu walioasisi Maktaba ya CCM Dodoma na anazijua nyaraka
za African Association vilivyo na yeye ndiye alikuwa akizitunza kuanzia enzi ya TANU wakiwa New
Street.

Tunaweza tukaja katika hoja ya ujamaa kuminya historia.

Nitakupa rejea moja uipitie ikiwa utaweza kuipata ya Mjamaa mkubwa sana duniani - Khrushchev.
Soma kitabu chake, '' Khrushchev Remembers,'' yeye kaandika ''memoirs,'' zake soma na fananisha.

Kuna mengi ningeweza kukueleza katika hizo hoja ulizotoa lakini hayo hapo juu yanatosha.
Kuna mengi wewe huyajui katika historia hii.

Historia hii ya TANU na uhuru wa Tanganyika ni historia yangu pia.
Mmoja katika hao ''wazee,'' ni babu yangu.
 
Unachoshangaa kipi sasa?

Unashangaa Mjamaa hajatoa umuhimu kwa watu binafsi na kawashukuru kwa mpigo wakati itikadi ya ujamaa inamtaka awaangalie watu kwa mpigo na asiwaangalie mmoja mmoja kama watu binafsi?

Unashangaa mjamaa kufanya itikadi ya ujamaa inavyomtaka kufanya na kutofanya ubepari unavyomtaka kufanya?

Unashangaa Muarabu kuongea Kiarabu na kutojua Kiingereza?

Kruschev hakuwa mjamaa, alikuwa Mkomunisti aliyeuchukia Ukomunisti baada ya Stalin. Kruschev ndiye aliyeweka misingi ya kuvunjika kwa USSR ambayo Gorbachev akaja kuimaliza. Sasa kumlinganisha Kruschev, a reformed Communist, na Nyerere, a Fabian Socialist, kama wote ni wajamaa, ni kutoelewa kwamba unachanganya mambo, hilo la kwanza.

Halafu lapili, hoja si Kruschev, ni Ujamaa. Inawezekana kabisa hata Kruschev angekuwa mjamaa wa jina akaendekeza kutajana majina, na Nyerere akaishi kwa kanuni za Ujamaa za kushukuru kwa mpigo, mfano wa Nyerere ndio ungeonesha Mjamaa halisi.

Huwezi kusema kuiba kunaruhusiwa na Wakatoliki kwa sababu Papa kaiba, inawezekana Papa kaiba kwa sababu kapotoka, ukiwa na Mkatoliki Padre hataki kuiba, kwa sababu Katekisimu na Biblia vimekataza kuiba, hutakiwi kusema huyu mbona anakataa kuiba wakati Papa ameiba? Unatakiwa kusema mbona Papa anaiba wakati Biblia na Katekisimu vinakataza kuiba?.

Vivyo hivyo, misingi ya Ujamaa haitaki ubishoo wa kutajataja majina yooote ya watu, inasisitiza collective kuwa muhimu kuliko individual, hivyo atatajwa mzee mmoja au wawili tu hapo, wengine watashukuriwa collectively kama "wazee" tu.

Sasa ukishakubali kwamba misingi ya Ujamaa inasisitiza kuangalia watu kwa mafungu kama collective, na Nyerere alikuwa Mjamaa, itabidi ukubali tu kwamba alipowashukuru watu jumla jumla alikuwa anaishi kijamaa tu.
 
Unachoshangaa kipi sasa?

Unashangaa Mjamaa hajatoa umuhimukwa watu binafsi na kawashukuru kwa mpigo wakati itikadi ya ujamaainamtaka awaangalie watu kwa mpigo na asiwaangalie mmoja mmoja kama watu binafsi?

Unashangaa mjamaa kufanya itikadi ya ujamaainavyomtaka kufanya na kutofanya ubepari unavyomtaka kufanya?

Unashangaa Muarabu kuongea Kiarabu na kutojua Kiingereza?

Kruschev hakuwa mjamaa, alikuwa Mkomunisti aliyeuchukia Ukomunisti baada ya Stalin. Kruschev ndiye aliyeweka misingi ya kuvunjika kwa USSRambayo Gorbachev akaja kuimaliza. Sasa kumlinganisha Kruschev, a reformed Communist, na Nyerere, a Fabian Socialist, kamawote ni wajamaa, ni kutoelewa kwamba unachanganya mambo, hilo lakwanza.

Halafu lapili, hoja si Kruschev, ni Ujamaa. Inawezekana kabisa hata Kruschev angekuwa mjamaa wa jina akaendekeza kutajana majina, na Nyerere akaishikwa kanuni za Ujamaa za kushukuru kwa mpigo, mfano wa Nyerere ndio ungeonesha Mjamaa halisi.

Huwezi kusema kuiba kunaruhusiwa na Wakatoliki kwa sababu Papa kaiba, inawezekana Papa kaiba kwa sababu kapotoka,ukiwa na Mkatoliki Padre hataki kuiba, kwa sababu Katekisimu na Biblia vimekataza kuiba, hutakiwi kusema huyu mbona anakataa kuiba wakati Papa ameiba? Unatakiwa kusema mbona Papaanaiba wakati Biblia na Katekisimu vinakataza kuiba.

Vivyo hivyo, misingi ya Ujamaa haitaki ubishoo wa kutajatajamajina yooote ya watu, inasisitiza collective kuwa muhimu kulikoindividual, hivyo atatajwa mzee mmoja au wawili tu hapo, wengine watashukuriwa collectively kama "wazee" tu.

Sasa ukishakubali kwamba misingi ya Ujamaa inasisitiza kuangalia watu kwa mafungu kama collective, na Nyerere alikuwa mjamaa, itabidi ukubali tu kwamba alipowashukuru watu jumla jumla alikuwa anaishi kijamaa tu.
Kiranga,
Sikushangazwa na kule kutoadhimisha historia ya TANU na uhuru.

Nimeshangaa kwa kule kuwa historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika ifutike
kwa ajili ya ''Ujamaa.''

Hayo mengine wala sina haja ya kuyasemea.

Muhimu kwangu ni kuwa nimeikataa historia hiyo ya ''Ujamaa,'' na nimeandika
historia kama ilivyostahili kuandikwa na imependwa sana.
 
Ujamaa ni ideology. Ideologies zote zina tabia ya kufuta historia na kuandika propaganda.

Huko Soviet Union kwa Kruschev, kuna watu walikosana na Stalin,wakakimbia nchi.

Stalin akatafuta mpaka picha alizopiga nao zamani, akafanya editing na kuwatoa wasionekane walikuwepo kwenye hizo picha.

Wengine walikuwa wakikosana na Stalin, anatuma watu wake wanamshika hasimu wake, wanamuua, halafu kama vile kumuua tu haitoshi, picha zote prominent zilizokuwapo ambazo huyo hasimu yumo, anaondolewa.

Censorship of images in the Soviet Union - Wikipedia

Marekani nakokuna sehemu wanataka kufuta historia ya utumwa na uonevu waliofanyiwa watu weusi isifundishwe wazi madarasani.

Ona hapa
 
Jivi hapo wazee bado wapo hai???
Nataka nikawasalimie na kufanya nao mahojiano

Hawa wazee wagumu sana kutuongoza wapi tukajiongeze historia ya Tangayika. Naamini wazee wa TANU kama Takadiri, Akida, Chaurembo, Plantan, Sykes, John Rupia na Hamza Mwapachu wameacha watoto wenye umri unaofanana na Mzee Mohamed Said au hata kumzidi walio hai.

Mfano kuna balozi Paul Rupia, Balozi Juma Volter Mwapachu pia pale Kijitonyama kuna kizazi cha Mzee Plantan. Huko Tanga, Tabora, Dodoma, Meru, Mbeya wapo watoto wa hao wazee wa TANU na ni umri wa Mzee Mohamed Said au zaidi na lazima watakuwa na ya kusimulia.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akiwavisha mgolole, Mzee Hashim Gawaza na Clement Nyoni alipotembelea Ofisi za CCM Kata ya Matogoro, Songea Mjini. Wazee hao ni waasisi wa TANU na CCM na eneo hilo ndipo Baba wa Taifa, marehemu Julius Nyerere alifika na kufanya mkutano wa siri 1957 katika harakati zake za kupigania uhuru wa Tanganyika ambapo katika mkutano huo wazee hao walishiriki na wengine watano waliotangulia mbele ya haki.

Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa NEC/CCM, Dk. Asha Rose Migiro 9katikati) akipiga picha ya kumbukumbu na wazee hao.
Mwasisi wa Tanu na CCM, Mustafa Songambele akisalimiana na Kinana alipokjutana naye katika Shina la CCM namba moja eneo la Mfaranyaki, Songea Mjini Leo.
c.c Mzee Mohamed Said
 
Unachoshangaa kipi sasa?

Unashangaa Mjamaa hajatoa umuhimukwa watu binafsi na kawashukuru kwa mpigo wakati itikadi ya ujamaainamtaka awaangalie watu kwa mpigo na asiwaangalie mmoja mmoja kama watu binafsi?

Unashangaa mjamaa kufanya itikadi ya ujamaainavyomtaka kufanya na kutofanya ubepari unavyomtaka kufanya?

Unashangaa Muarabu kuongea Kiarabu na kutojua Kiingereza?

Kruschev hakuwa mjamaa, alikuwa Mkomunisti aliyeuchukia Ukomunisti baada ya Stalin. Kruschev ndiye aliyeweka misingi ya kuvunjika kwa USSRambayo Gorbachev akaja kuimaliza. Sasa kumlinganisha Kruschev, a reformed Communist, na Nyerere, a Fabian Socialist, kamawote ni wajamaa, ni kutoelewa kwamba unachanganya mambo, hilo lakwanza.

Halafu lapili, hoja si Kruschev, ni Ujamaa. Inawezekana kabisa hata Kruschev angekuwa mjamaa wa jina akaendekeza kutajana majina, na Nyerere akaishikwa kanuni za Ujamaa za kushukuru kwa mpigo, mfano wa Nyerere ndio ungeonesha Mjamaa halisi.

Huwezi kusema kuiba kunaruhusiwa na Wakatoliki kwa sababu Papa kaiba, inawezekana Papa kaiba kwa sababu kapotoka,ukiwa na Mkatoliki Padre hataki kuiba, kwa sababu Katekisimu na Biblia vimekataza kuiba, hutakiwi kusema huyu mbona anakataa kuiba wakati Papa ameiba? Unatakiwa kusema mbona Papaanaiba wakati Biblia na Katekisimu vinakataza kuiba.

Vivyo hivyo, misingi ya Ujamaa haitaki ubishoo wa kutajatajamajina yooote ya watu, inasisitiza collective kuwa muhimu kulikoindividual, hivyo atatajwa mzee mmoja au wawili tu hapo, wengine watashukuriwa collectively kama "wazee" tu.

Sasa ukishakubali kwamba misingi ya Ujamaa inasisitiza kuangalia watu kwa mafungu kama collective, na Nyerere alikuwa mjamaa, itabidi ukubali tu kwamba alipowashukuru watu jumla jumla alikuwa anaishi kijamaa tu.
[emoji123]
 
Ujamaa ni ideology. Ideologies zote zina tabia ya kufuta historia na kuandika propaganda.

HukoSoviet Union kwa Kruschev, kuna watu walikosana na Stalin,wakakimbia nchi.

Stalin akatafutampaka picha alizopiga nao zamani, akafanya editing na kuwatoa wasionekane walikuwepo kwenye hizo picha.

Censorship of images in the Soviet Union - Wikipedia
Ujamaa ni ideology. Ideologies zote zina tabia ya kufuta historia na kuandika propaganda.

HukoSoviet Union kwa Kruschev, kuna watu walikosana na Stalin,wakakimbia nchi.

Stalin akatafutampaka picha alizopiga nao zamani, akafanya editing na kuwatoa wasionekane walikuwepo kwenye hizo picha.

Censorship of images in the Soviet Union - Wikipedia
Kiranga,
Hayo nikiyajua siku nyingi na ndiyo nikanyanyua kalamu kuandika historia ya kweli ya
TANU na uhuru wa Tanganyika.

Kuna mahali katika kitabu nimesema hayo hapo chini:

''In 1974 President Julius Nyerere granted the responsibility of recording the history of
TANU to Kivukoni Ideological College. Kivukoni College was established in the tradition
of Ruskin College of Britain.

Kivukoni was and still is a training centre for propaganda and mass indoctrination for
party cadres.

Kivukoni, therefore, was unsuitable for any serious research work.

In 1976, at the 16 th TANU conference, Nyerere again insisted on having an official
history of the Party.

Official histories always have failed in objectivity as observed by Maslov:

“Depersonification of the past is yet another drawback of the literature dealing with
the history of the CPSU.

In textbooks and research papers, historic personalities are as a rule, just inserted in
the general ‘list’ and some are not mentioned at all. “[1]

[1]For understanding problems of official histories see article by Dr Nikolai Maslov,
‘Questions of History of the Communist Party of Soviet Union.’ in Daily News, 24 th
October, 1987. For purpose of comparison see Historia ya Chama...op. cit.
 
Hawa wazee wagumu sana kutuongoza wapi tukajiongeze historia ya Tangayika. Naamini wazee wa TANU kama Takadiri, Plantan, Sykes, John Rupia, Sijaona, Lusinde na Hamza Mwapachu wameacha watoto wenye umri unaofanana na Mzee Mohamed Said au hata kumzidi walio hai.

Mfano kuna balozi Paul Rupia, Balozi Juma Volter Mwapachu pia pale Kijitonyama kuna kizazi cha Mzee Plantan. Huko Tabora, Dodoma, Meru, Mbeya wapo watoto wa hao wazee wa TANU na ni umri wa Mzee Mohamed Said au zaidi na lazima watakuwa na ya kusimulia.

c.c Mzee Mohamed Said
Bagamoyo,
Hakika watoto wa wazalendo wana mengi sana katika historia ya TANU na uhuru
wa Tanganyika.

Naanza na mimi mwenyewe:
Mohamed Said: BABU YANGU SALUM ABDALLAH

Juma Mwapachu:
Mohamed Said: FB: JUMA MWAPACHU AMZUNGUMZIA BABA YAKE KATIKA HISTORIA YA UHURU WA TANGANYIKA

Bi. Maunda Plantan:
Mohamed Said: WATOTO WA WAPIGANIA UHURU BI. MAUNDA PLANTAN, JUMA MWAPACHU, HAPPY MTAMILA NA KLEIST SYKES WANAPOWAKUMBUKA WAZEE WAO
 
Back
Top Bottom